Dar: Wanafunzi 4 wa Chuo Kikuu cha Kampala kortini kwa kumkashifu Rais Magufuli kupitia WhatsApp

Acha kulinganisha baba na urais, ili uwe baba kuna tendo unafanya na mwenzako wa jinsia tofauti na ili uwe rais kuna utaratibu unapitia kwa mujibu wa sheria, kwa hiyo baba na urais ni vitu viwili tofauti havipaswi kulinganishwa. Baba ataheshimiwa kwa mujibu wa mila zetu na desturi na rais ataheshimiwa kwa mujibu wa katiba na sheria zetu.
 
kuna watu watatetea huu ujinga wa hawa wanafunzi.
Hivi kwa mfano wewe jinsia ya kiume unaetetea ujinga ukiitwa shoga wakati wewe sio shoga utakubali?
 
Hata maumivu ya kichwa huanza polepole. Nadhani wewe kama mzazi, mwanao akianza vijitabia vya ajabu utamuacha tu sababu "havina impact", ila baadae vitakapokomaa na kuwa sugu.......utaanza kujiuliza ulikosea wapi. Usilaumu sheria ya makosa mtandaoni, bali tabia za watu wasio na adabu wala heshima. Kama hilo ni la kawaida, basi wangeanza kutengeneza picha za wazazi wao, za aina hiyo, na wasizambaze kwenye mtandao, hata kama audience ni watu 10. Tutalaumu sana sheria, ila VIJANA SASA HIVI TABIA ZETU NI MBAYA KUPINDUKIA, kwa sababu tu tumejificha nyuma ya keyboard/smartphone, hakuna anayekuona.
Watengeneze picha za wazazi wao kwa sababu gani? Kwani wazazi wao wanaongoza nchi tena hovyo hovyo km hivi? What kind of argument is that?
 
Umewahi kujiuliza, Salim Ahmed Salim aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, akiwa na umri gani?

Akiwa na umri huo huo wa hao unaowaita watoto sasa ngoja wakajifunzie adabu huko jela na mahakamani.

Soma, hiyo profile ya Dr. Salim Ahmed Salim utaelewa kuwa sisi vijana wa leo ni janga kwa Taifa kwa hiyo ni lazima udhibiti madhubuti uwepo.

Pia, iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizi chafu na za kukemewa kwa nguvu kabisa.

Biography of Dr. Salim Ahmed Salim
Acha kuchekesha. Tangu Salim ateuliwe nani nwingine ameshawahi kuteuliwa katika umri Huo!? Zaidi ya kuteua wazee!?
 
Lakini Wengine ni haki kuwa kashfu kupitia vyombo vya habari. Ikija kwenu wakali kama pilipili
 
Watengeneze picha za wazazi wao kwa sababu gani? Kwani wazazi wao wanaongoza nchi tena hovyo hovyo km hivi? What kind of argument is that?
So, as for you, insulting and humiliating adults is the best 'argument'!? Waliosema asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu hawakukosea, those kids, badala kusoma wanafanya ujinga chuoni.....basi na funzo walipate. Na mtafungwa sana awamu hii.
 
mbona unauliza swali juu ya swali???nimekuuliza lini ulitoka kula ugali kwa baba yako????hafu tutajua tunaongelea watoto wa aina gani
Akili ndogo siku zote u concentrate na kutumia nguvu nyingi kwenye minor issues wakati huo kuna mambo mengi muhimu yanayohitaji kufanyiwa kazi.

Watu wanashindwa kuelewa popote pale duniani raisi ndio most talked about celebrity in every single day. Na usitegemee kila anaemuongela raisi basi atamuongelea kwa mlengo mzuri, hivi unafikiri ni watu wangapi wanaomuongelea raisi kwa mabaya Tanzania hii!!? tukiamua kuwakamata wote wanao mkashifu raisi mtandaoni hizo jela zote zitajaa ndani ya siku mbili na hadi wafungwa wengine mtawaamishia ikulu.

Poor tanzania.
acha washikishwe adabu kama imekukera nenda kanywe nao chai segerea
 
Hivi Mh rais na serikali yake wamekosa mambo ya msingi ya kufanya wamebaki wakikimbizana na vitoto vidogo kwenye whatsapp? Aibu sana. Hivi ni kweli hii ndio spirit ya hii sheria ya mitandao! Kuzuis watu wasumkosoe rais?
Mbona ukosoaji, kejeli na mambo ya kawaida katika dunia ya demokrasia ya vyama vingi? Rais Zuma wa Afrika ya Kusini aliwahi kuchorwa katuni akiwa uchi na genitsls zake zikininginia. Hii ilikuwa ni kukejeli tabia yake ya kupenda ngono! Sasa hakuweza kufanya chochote zaidi ya kwenda mahakamani kuombs hiyo potrait isioneshwe tena hadharani. Lakini mahakams ikasema huo ni.uhuru wa kujieleza, hauwezi kuingiliwa kwa sababu uko provided for kwenye katiba. Sssa hapa kwetu tunataka kuishi ksma tupo kwenye chama kimoja?
Hiyo ni kazi ya jeshi la polisi kushughulikia wahalifu bila kuchoka na hawa wanashikishwa adabu kupitia cyber crime act iliyo sainiwa na Mh JK 2015... kama umechukia sana kanywe nao juice uko segerea
 
I wish nione huo ujumbe.
Some things need to be let go there are more serious matters to deal with . zaidi ya kutumia resources za nchi ya watu wanaolia maisha magumu kufukuzana na wanafunzi. . .

Wat happens zikiwa ignored. . .

Naamini kiongozi wa jamii ya watu wengi hasa wa siasa na jamii yake wanapaswa kuwa na tolerance ya hali ya juu kama wanalengo la kutumia.mda wao vizuri.

Kwa mtazamo wangu ni kufanya tu watu wasiweze kutoa views na hisia zao dhidi ya utawala. . .

Hata sielewi
Kuna kitengo jeshi la polisi kuna watu wame ajiriwa kwaajili ya kupambana na watu wanao vunja sheria kupitia cyber crime act... hakuna resource inayopotea kabisa kila mtu anajua fika polisi wanafanya kazi yao na wanalipwa kwaajili ya hilo.
Wacha washikishwe adabu.
 
acha washikishwe adabu kama imekukera nenda kanywe nao chai segerea
Ni watu wangapi wanao mkashifu na kumdhiaki raisi kwanzia mtandaoni mpaka mitaani kwa siku?

Je, mngekuwa na uwezo wa kuwabaini wote wanaotenda kosa hilo mngewakamata na kuwachukulia hatua?
 
Baba mwenye nyumba huwa hakosolewi ila hupewa ushauri tu ..au wewe umewahi kumkosoa baba ako?
Huyu ni tofauti na Baba mwenye nyumba. Baba gani anachaguliwa kwa kuomba kura kuwa baba? halafu baada ya miaka 10 anatoswa na anakuja baba mwingine? huu mfano wa baba ni kwa kiasi fulani tu, kwa maana ya heshima. na hauji hivi hivi, inabidi aupiganie. Nyerere haitwi Baba wa Taifa eti kwa sababu tu ndio raisi wa kwanza. Anaitwa Baba wa Taifa kutokana na shughuli pevu aliyoifanya, upendo wa kibaba aliouonesha. huyu Magu anachakarika kiasi fulani, lakini hajafikia standard ya "ubaba". bado sana tu. na kumbuka huyu tumemwajiri sisi watanzania. na kwa katiba yetu, mamlaka ni ya wananchi. kwa hiyo tunayo haki ya kumkosoa ili akae kwenye mstari. na kama anakubali kukosolewa hata kwa kuchorwa katuni, ingemsaidia zaidi
 
Acha kulinganisha baba na urais, ili uwe baba kuna tendo unafanya na mwenzako wa jinsia tofauti na ili uwe rais kuna utaratibu unapitia kwa mujibu wa sheria, kwa hiyo baba na urais ni vitu viwili tofauti havipaswi kulinganishwa. Baba ataheshimiwa kwa mujibu wa mila zetu na desturi na rais ataheshimiwa kwa mujibu wa katiba na sheria zetu.
... Ni kitu kimoja kuwa na Katiba na Sheria mbalimbali lakini kuziheshimu hizo Sheria na kuzitii is another thing kwenye hii awamu. Recently kuna mtukufu mmoja amegomea wito halali wa mahakama and nothing happened.
 
Back
Top Bottom