Dar walia na maji huku Serikali ikisema... Tumefikisha maji vijijini kwa asilimia 65 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar walia na maji huku Serikali ikisema... Tumefikisha maji vijijini kwa asilimia 65

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 27, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Chanzo cha maji Ruvu juu

  NI kawaida kwa wananchi hasa wa nje ya Dar es Salaam kuvutika mikoa yao inapokuwa mwenyeji ha wa shughuli mbalimbali za kitaifa.

  Wengi wamekuwa wakijitokeza kujifunza, na kujionea mambo mbalimbali na pia kupata fursa ya kuwaona viongozi ambao pengine ingekuwa vigumu kufanya hivyo kuwapata katika ofisi zao.

  Lakini hali ilikuwa tofauti katika maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo yalifanyika kuanzia Machi 16 na kufikia kilele chake Machi 22, mwaka huu katika Viwanja vya Mwendapole, Kibaha mkoani Pwani.

  Mabanda ya wizara, idara, taasisi na wadau wengi wa sekta hiyo katika viwanja hivyo ambayo yalikuwa zaidi ya 10, hayakupata wageni wengi kama ilivyotarajiwa.

  Msemaji wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Nyabaganga Taraba anasema kumekuwa na dhana miongoni mwa wananchi kuwa wiki ya maji haina faida yoyote. Anasema dhana hiyo ni potofu kwani ina umuhimu kwa kuwa huibua mambo mengi kupitia maoni kutoka kwa wadau. Pia ni fursa kwa wizara na watendaji wakuu kujipima.

  Wiki ya maji kwetu ina faida maana huwa inaibua mambo mengi ambayo yanatolewa na wadau ambayo hutoa fursa kwetu kujipima wapi tumekosea, wapi tunapaswa kujirekebisha na wapi tunatakiwa kuboresha huduma zetu kwa kiwango kinachotakiwa,anasema Taraba.

  Anasema wiki hiyo hufanyika katika kila mkoa na hivyo kuwapa fursa ya kuwa karibu na wananchi katika kipindi hicho.

  Taraba anasema wizara yake inaamini kuwa kama wananchi hawatakuwa na elimu sahihi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji hata kama wakipelekewa mabomba mpaka majumbani hayatatunzwa na matokeo yake yataishia kuharibika.

  Ndiyo maana miradi mingi ya maji iliyojengwa miaka ya 1970 hivi sasa imeharibika kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa kikamilifu katika kuisimamia. Serikali kuu ndiyo iliyokuwa na jukumu la kupanga, kutekeleza na kuisimamia,anasema Taraba.

  Hivi sasa kupitia sera hizo ambazo zilionekana kuwa zina mapungufu, Serikali iliandaa Sera ya Maji ya mwaka 2002 ambayo ilitilia mkazo suala zima la ushirikishwaji wa wananchi katika miradi ya maji.

  "Malengo ya Wizara ni kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG), Mkakati wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi (Mkukuta), pamoja na kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2025.

  Kuna mwelekeo mzuri wa kufikia malengo ya Mkukuta na MDG. Tayari kwa mwaka huu tumeweza kufikisha maji vijijini kwa asilimia 65 na mijini asilimia 90 ingawa hatujafikia malengo yanayokusudiwa kutokana na kuchelewa kwa utekelezaji wa programu lakini tunaamini tutafikia,anasema Taraba.

  Hata hivyo, baadhi ya wananchi hasa wale wanaoishi katika maeneo ambayo hayapati huduma ya uhakika ya maji au kutopata kabisa wanasema kwamba hawaoni umuhimu wa kuingia gharama katika kuandaa wiki hiyo.

  Badala yake wanataka serikali ijikite zaidi katika kushughulikia kero ya upatikanaji wa maji kwa kuzingatia umuhimu wake kwa mahitaji ya binadamu na ulinzi wa afya na mazingira.

  Mkazi wa Mburahati, Dar es Salaam, Lucy Samky anaona kwamba tatizo la maji linazidi kuongezeka tofauti na takwimu zinazotolewa kwamba kiwango cha usambazaji na utoaji wa huduma kimeongezeka.

  Kwa ujumla juhudi za kupambana na tatizo hili ni kama hazionekani, anasema Lucy akitolea mfano wa eneo analoishi ambalo kwa miaka mingi sasa kumekuwa na tatizo la maji kiasi kwamba wakazi wake wala hawajui lolote kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa huduma maji ya serikali kwani wengi wao wanategemea visima binafsi na kununua kwa wauzaji wanaochota maeneo ya mbali ambayo hata hivyo, usalama wake haujulikani.

  Mbali ya usalama, hata bei zake ni za juu. Kwa mfano, dumu moja ni zaidi ya Sh200 kiasi ambacho kwa maisha ya Mtanzania ni kiwango cha juu, ukilinganisha na bei ya ndoo kwa Sh50 ambayo wanaopata huduma hiyo katika vyanzo vya serikali wanapata.

  Ombi langu kwa serikali ni kuwa na mkakati madhubuti katika kupambana na tatizo hilo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kusaka maji badala ya kufanya kazi za maendeo,anasema.

  Mkazi mwingine wa Tabata, Dar es Salaam ambako nako kuna shida kubwa ya maji, Habiba Kabwe anasema walifarijika kuona Wachina wakipita katika maeneo yao wakichimba na kuweka mabomba ya maji lakini licha ya kukamilika katika baadhi ya maeneo, hakuna mabadiliko yoyote yanayoonekana.

  Anauponda mradi huo akisema umewapa matumaini hewa kwani wanachokiona hivi sasa ni maji kupotelea njiani badala ya kufika katika maeneo yaliyokusudiwa.

  Mabomba mengi yamepasuka na matokeo yake maji hayafiki majumbani na hata wale waliokuwa na mabomba siku za nyuma hivi sasa hayatoi maji kabisa,anasema Habiba.

  Lakini wahenga walisema kufa kufaana, shida ya maji ni neema kwa baadhi ya vijana kama Hamis Mrima wa Ubungo Riverside. Anaombea kila leo shida hiyo isikome akisema kwamba inachangia upatikanaji wa ajira kwa vijana.

  “Wewe fikiria, hivi kama maji yangekuwa yanapatikana kila siku sisi wauza maji tungekuwa tunaishije? Acha yasiwe yanapatikana hivyo na sisi tutajua namna ya kuyasaka na kuyapata.

  Tutayauza na maisha yatakwenda mbele. Sina kazi lakini sasa napata kila siku si chini ya Sh10,000, Mungu anipe nini!” Kijana huyo ambaye ameanza kazi hiyo tangu mwaka 1999, ameoa na ana watoto na pia ameanza kujenga nyumba ya kuishi kutokana na biashara hiyo.

  Taraba anasema tatizo linaloikabili Dar es Salaam linatokana na ukweli kwamba maji ni yale yale miaka nenda rudi lakini watu wanazidi kuongezeka siku hadi siku huku akidokeza kwamba miradi ya maji ina gharama kubwa na inahitaji vitu vingi ikiwa ni pamoja na utashi wa kisiasa, uwekezaji wa kifedha na ushirikiano wa wananchi.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18778
   
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  "Tumefikisha maji vijijini kwa asilimia 65"

  Propaganda hizi unless waseme
  "Tumefikisha mabomba vijijini kwa asilimia 65"
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nakumbuka mwaka 1985 nilisikia kwenye taarifa ya habari eti ifikapo mwaka 2000 raia wote watapata maji, mpango ukiitwa maji kwa wote ifikapo mwaka 2000, miaka kumi sasa hapa hapa dar tena sinza vatican watu wanaoga maji ya kisima, sasa kule lingusenguse au twatwatwa kijiji cha wamasai kilosa maji si ni msamiati tu
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Uwasikie kwa aina za mipango ndo utachoka:
  -Tuna Mpango-Mkakati wa kunanihii
  -Serikali inasimamia Mpango-Endelevu wa nanihii
  -Tumeweka Mpango-Boresho wa ukarabati etc!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ukweli ni kwamba kwa umaskini wetu njia pekee ya kuondokana (au kuahirisha hadi hapo tutakapokuwa na uchumi imara) na matatizo ya maji na matatizo mengine ya ukosefu wa miundombinu etc, ilikuwa ni kwa serikali kukataza watu kuanzisha makazi kwenye sehemu ambazo ni haziishiki kwa maana kuna unfavourable conditions..kama ukame etc

  Nchi yetu ni kubwa sana na sielewi kwanini watu watake kwenda kujifutika ndanindani huko na kusambaa kila kona halafu baadae wanalalama eti hatuna maji au barabara au umeme.
   
Loading...