Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

We unataka tuwaite mabeberu?????
Serikali isizembee kuhusu tope linalotoka ardhini, mpaka sasa wstaalam wa jiolojia wanaonekana kutokuwa na uwezo lakini wanasita kusema! Jinai siku zinavyokwenda ndivyo mashimo yanayotoa tope yanaongezeka, inawezekana kutokuwepo mpango wowote wa kupata wataalamu wenye vifaa unatokana na kitokuwepo waziri husika.

Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wanatakiwa wachukue hatua za haraka kupata wataalam toka nje kwani hili si bomba lililopasuka hii ni hali ya hatari tunaposhuhudia nyumba nzima kutitia.
 
Kuna uhusiano gani na wataalamu wa UDSM na ilo tope? Hata kama wangepewa kazi si inapaswa wafanye utafiti na kuandika report
Hivi unajua kuna tume ya Jiologia Tanzania??
 
Niliona itv hiyo picha nazani mpiga picha aliogopa kusombwa na tope maana maelezo na picha nliyoona ni mbingu na ardhi, watu wanaogopa halafu kinachoogopwa sikioni ila nikajiambia nazeeka sasa
Kwenye TV ilioneshwa nyumba ambayo imezama kabisa linaonekana bati la paa tu na baadhi ya nyumba zimebomoka, hili litakuja kuwa janga maana kila siku mashimo yanaongezeka na wakazi wa hapo wanahofu kubwa huku sisi hofu yetu ni Chadema tu.
 
Mtaalamu alikuwa anajaribu kukumbuka theory zake alizomeza chuo, yule mtaalamu wa miamba prof. muhongo bado hajatafutwa..
Yule alikuwa mpiga ramri, anaeleza kuwa chanzo ni vishindo vya magari na watu wanaopita kwenye eneo hilo! Alionekana siku ya kwanza hana hata kabisibisi ka kuchokonoa mwamba! Alipokuja tena akaleta hizo theory zake za darasa la saba! Hapo ndipo nikamuona hana uwezo ni mpiga ramri tu.
 
kuna probability dar nzima kuzama. Ilikadiliwa miaka zaid ya 200 yakua dar itamezwa na maji. Hivo hilo la kunduch ni manyunyu mvua yaja. Pia kuna kitu kingine kinachoitwa plate tectonic movement nayo inaenda kas sana. Hivo nikipata mda tutajadili pamoja ila dar ipo zone mbaya sana na si mara ya kwanza maeneo makubwa, ikiwemo visiwa kuzama kabisa.
Kwa hiyo madaraja yetu, barabara na uwanja tutakuwa tumekula hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliona itv hiyo picha nazani mpiga picha aliogopa kusombwa na tope maana maelezo na picha nliyoona ni mbingu na ardhi, watu wanaogopa halafu kinachoogopwa sikioni ila nikajiambia nazeeka sasa
Gwajima ataeza zuia tope
 
Back
Top Bottom