Dar: Waislam waungana kuombea Mvua inyeshe ili kuondoa ukame

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,498
3,465
Waumini wa dini ya kiislamu jijini Dar es Salaam wameungana kwa pamoja katika ibada ya kuombea mvua inyeshe na kuondoa hali ya ukame ambayo ni changamoto.

Hivi karibuni Mufti sheikh Abubakar Zubeir aliwataka waislamu kote nchini kufanya swala maalum ya kuomba mvua za heri

Mufti aliwataka Waislamu wa taasisi na madhehebu yote nchini kuungana na kuhudhuria kwenye Dua hii ya kitaifa iliyofanywa viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Jumapili hii saa moja na nusu Asubuhi 24/3/2019.

Mufti aliwataka viongozi wa taasisi zote za kiislamu, viongozi wa mikoa yote, wilaya na kata zote nchini kuipa umuhimu mkubwa na kufanya juu chini kuandaa swala hiyo.

Aliwataka maimamu wote nchini kuomba dua ya Kunuti kwenye swala ya Ijumaa kumuomba Mwenyeezi Mungu aliepushe taifa na janga la ukame pamoja na mafuriko.

Habari zaidi, soma=>Mufti ataka waislam kuomba mvua - JamiiForums
 
Cha kushangaza watakutana mashehe wote na waumimi wao watakesha wiki nzima ila ukame ndio utaongezeka ,watakuja wachungaji na maaskofu watakesha mwezi mzima na waumini wao hola .ila wazee wetu wazamani walikua wakipanda miliamni kuomba mvua kabla hawajashuka imejibu na wakiitaka ikome inakoma papo hapo.
Cjui afrika ni wapi tulikosea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakiomba mahoka au mizimu nyinyi mnamuomba kinafik tupunguze zinaa
Cha kushangaza watakutana mashehe wote na waumimi wao watakesha wiki nzima ila ukame ndio utaongezeka ,watakuja wachungaji na maaskofu watakesha mwezi mzima na waumini wao hola .ila wazee wetu wazamani walikua wakipanda miliamni kuomba mvua kabla hawajashuka imejibu na wakiitaka ikome inakoma papo hapo.
Cjui afrika ni wapi tulikosea

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli mvua itakuja kwa dua za mufti na kundi la bakwata nabii musa aliomba watu wake waje uwanjani kuomba mvua walipoomba mungu alimwambia musa sintopokea dua yako kwa sababu katika watu wako waliopo uwanjani kuna mtu mmoja tu mnafiki. Je leo hii mufti wa bakwata mganga sheikh wa mkoa ndio huyo na wengine wengi wanafik je mungu atakubali dua zao
 
Naam, swala ya kuomba mvua
BISMILLAHI RAHMANI RAHIYM

*SALA YA KUOMBA MVUA*
*(SWALATUL ISTISQAA)*

Ni swalah maalum ya KUOMBA NA KUMLILIA ALLAH ILI KUONDOA UKAME KWA KULETA MVUA


Mtume Swalallahu Aleihi wa Salaam alifanya swalah hii maalum katika viwanja vya wazi kwa kuomba mvua .

Mtume Swalallahu Aleihi wa Salaam alielekea Qibla na kuvaa nguo zake kwa kugeuza(yaani kuvaa nguo nje ndani) na kuswali rakaa mbili

Ni Mustahab kuswali swalah hii Asubuhi baada ya kuchomoza Jua kama muda unaoswaliwa swala za Idd mbili.


Swalah hii hufanyika katika viwanja vya wazi na sio Msikitini isipokuwa kwa dharura

*NAMNA YA KUSWALI SWALATUL ISTISQAA*

*1-* Ni swalah ya Rakaa mbili ambazo hazina Adhana wala Iqamah
Swala hii huswaliwa kwa sauti kama ilivyo swalah ya Ijumaa au Iddi mbili

*2-* Swalah hii ina takbira saba kwenye rakaa ya kwanza na Takbira Tano kwenye Rakaa ya pili,
Atasema Takbira hizo huku ana Mswalia Mtume Swalallahu Aleihi wa Salaam kila baada ya Takbiir


*3-* Baada ya Swalah imam atatoa khutba na kuleta ISTIGHFAAR KWA WINGI NA KUSOMA SANA AYAH ZA QURAN baadae husoma DUA KUBWA KWA KUMBEMBELEZA ALLAH NA KUONYESHA MAJUTO KWA MAKOSA NA MADHAMBI YETU NA KUJIWEKA WADHALILI MBELE YA ALLAH

*4-* Imam wakati wa kuomba Dua huelekea Qibla na kugeuza nguo nje ndani(avae nguo kwa kugeuza)

*5-* Watu wavae nguo kuukuu (Nguo za Kawaida) Na wala wasijipambe kwa kujipaka manukato(uturi) n.k

*6-* KUFANYA SANA ISTIGHFAAR KWA KUJUTA muda wote , watu wakiwa kwenye Muswalah ( Sehemu ya Kusalia)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom