Dar: Wafikishwa Kortini kwa kukutwa na Mihuri ya Serikali

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,101
Mkazi wa Kigamboni, Elias Kitiku na raia wa China, Qui Hong Chen wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne ikiwemo kukutwa na mihuri ya idara ya serikali na kuishi nchini kinyume na Sheria

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salim Msemo

Akiwasomea mashtaka, wakili Msemo alidai katika mashtaka ya kwanza mshtakiwa Kitiku anakabiliwa na kosa la kukutwa na mihuri mbalimbali ya idara ya serikali, ambapo inadaiwa Juni 16, 2020 katika maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam alikutwa na mihuri ya idara ya uhamiaji ikiwemo ya kuwasili, kuondoka na viza

Katika mashtaka ya pili, Kitiku anakabiliwa na kosa la kuzalisha mihuri ya idara ya uhamiaji, ambapo inadaiwa Juni 16, 2020 katika maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam kwa nia ovu alizalisha mihuri hiyo

Katika mashtaka ya tatu yanayomkabili Qui Hong Chen ya kujifananisha na mtu mwingine, Msemo alidai Juni 26, 2020 katika maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam kwa nia ovu alijitambulisha kwa ofisa wa idara ya uhamiaji, Eliud Ikomba kuwa yeye ni Fanh Fang Liao huku akijua kuwa si kweli

Msemo alidai katika mashtaka ya mwisho, Chen anakabiliwa na kosa la kuishi nchini kinyume na sheria, ambapo alidai Juni 26, 2020 katika maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alikutwa akiishi chini kinyume na sheria.

Washtakiwa wote walikana mashtaka. Upande wa mashtaka walidai upelelezi umekamilika, hivyo waliomba kupangiwa tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali. Nao upande wa utetezi kupitia wakili wa utetezi, Steven Bwana waliomba dhamana kwa washtakiwa, kwa kuwa mashtaka yao yana dhamana kisheria.

Hakimu Kabate baada ya kusikiliza hoja za pande zote, alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa wote, ambapo mshtakiwa wa kwanza Kitiku alitakiwa kusalimisha hati ya kusafiria au kitambulisho cha taifa pamoja na kupeleka wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni mbili kila mmoja.

Mshtakiwa wa pili alitakiwa kupeleka wadhamini wawili kutoka ubalozi wa China au popote Tanzania ambao ni waajiriwa wa serikali au taasisi inayotambulika watakaosaini bondi ya Sh milioni mbili kila mmoja. Washtakiwa wote walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana.
 
Hao walikataa kutoa rushwa.

Rushwa sometimes ni nzuri sana, unaweza ukaepuka jela miaka 20 kwa kutoa elfu kumi tu.
 
Back
Top Bottom