Dar: Wabunge wa CHADEMA na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, wawasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,558
21,494
DWFFJqlWAAAXX9z.jpg

Dar es Salaam. Wabunge wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wameshawasili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi saa 2.

Wabunge hao wanafika mahakamani kama walivyoamriwa na mahakama kutokana na mashtaka yanayowakabili, ikiwano ya kuhamasisha maandamano na uchochezi.

Miongoni mwa waliofika mahakamani ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Esther Bulaya wa Bunda, Halima Mdee (Kawe), Esther Matiko(Tarime Mjini), Naibu Katibu Mkuu bara, John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu .

Wamefika mahakamai hapo kutokana na kesi inayowakabili namba 112 ya mwaka huu

Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ataongoza kesi hiyo huku Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi akijibu hoja zilizowasilishwa jana na Wakili wa utetezi Peter Kibatala.

Chanzo: Mwananchi

Soma: Mbowe na viongozi 6 wa CHADEMA wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa mashitaka 8, wanyimwa dhamana hadi Machi 29

Soma: KISUTU, DAR: Mahakama yawapa dhamana Viongozi 6 wa CHADEMA bila kuwepo mahakamani. Kutoka gerezani Aprili 3, 2018...

Soma: Mbowe na wenzake waomba shauri lao kuhamia Mahakama Kuu. Mh. Ester Bulaya ameunganishwa katika kesi yao
 
Hao ndo wachafuzi wa Amani ya Nchi hii kwa urafi wao wa kutaka kuchukua nchi.Kilimanjaro na Arusha ni watu hatari kuwakabidhi nchi hao
 
Hao ndo wachafuzi wa Amani ya Nchi hii kwa urafi wao wa kutaka kuchukua nchi.Kilimanjaro na Arusha ni watu hatari kuwakabidhi nchi hao

Nafikir hiyo mikoa ipo kenya kama tunawabagua kwa nini tuiite mikoa ya iliyopo tz?

Wakenya wapo sahihi kuunadi mlima kilimanjaro kama wa kwao mana nyie kwa nyie mnafarakana dhambi ya ubaguz ni mbaya sana ikipenya ni sawa na mbwa anaeumwa ugonjwa wa kichaa
 
Kama taifa tujitafakari kwann tumefika hapa,lasivyo naona giza mbele.

MUNGU ibariki Tanzania
 
Hao ndo wachafuzi wa Amani ya Nchi hii kwa urafi wao wa kutaka kuchukua nchi.Kilimanjaro na Arusha ni watu hatari kuwakabidhi nchi hao
Wewe umelaaniwa kwa sababu ukishakula nyama ya mtu basi inakuwa ni tabia. Nani kakuambia Kilimanjaro na Arusha. wewe umetokea mkoa gani mzuri kiasi cha kushaushi upewe nchi. Kwa taarifa yako kama ungejua, watanzania wengi wanaichagua CCM na siyo mtu. Kwa hiyo hata sasa unayemzania ni kiongozi mzuri, ni sawa kwa sababu anakuwezesha kuishi mjini. Na sijui unatumia nini kusema arusha na moshi. Escrow ni ya wapi? Epa ya mkoa gani? Richmond ya mkoa gani? wala rushwa wote waliofikishwa mahakamani ni wa mikoa gani? Wewe ukome kuleta ubaguzi hapa kwenye nchi yenye misingi ya umoja wa kitaifa.
 
Wachàga mtasubiri sana kwenye hii nchi mna ukabila ambao mnashindwa kuuficha tunao hata huku makazini tunawachora tu.
 
Back
Top Bottom