Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,156
- 31,041
Hakuna msamaha kwa msaliti a.k.a uhaini. Imeisha hiyoMODS NAOMBA MSIUUNGANISHE HUU UZI. Huu uzi ni wa kipekee kabisa wenye mapenzi mema kwa Mdee na wenzake 18 na CHADEMA. Binafsi mimi naipenda sana chadema japo sio mwanachama. Halima Mdee na wenzake waliamua kubeti na bahati mbaya mkeka umechanika. Hivyo nawaomba wajishushe, waombe radhi na chedema pamoja na wapenzi wake tutawasamehe. Hela tamu jamani, hata mimi ningekuwa kwenye nafasi yake ningesaliti tu. Bahati mbaya amesaliti na ameshindwa kuyapata matunda ya usaliti, hivyo ni bora atubu na atasamehewa. Halima umelala jela kwa sababu ya chadema, umepigwa, umeumizwa na kudhalilishwa kwa ajili ya chadema, hivyo kosa lako moja haliwezi kuyafuta mema yote uliyokifanyia chama. Hakuna aliye mkamilifu chini ya jua. Hata Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha sembuse wewe! Halima tumekuelewa shida sio kwamba huna mapenzi na chadema, shida ni tamaa ya fedha hivyo tafadhali dada angu omba msamaha na hakika utasamehewa. Ni hayo tu dada angu.