Dar Technical na Technical College Arusha Mpo !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar Technical na Technical College Arusha Mpo !!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Yegomasika, Sep 24, 2009.

 1. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Jamani wale mliosoma Dar Tech enzi hizo kabla hawajaibatiza jina la Dar Institute of Technology mpo?. Mimi nilikuwepo pale 1986/1989. Mnamkumbuka Mzee Zoro na mambo ya cafteria, mambo ya Juche idea-Mkuu wa chuo Mr Chande baadae Mr Msoma?. Tukumbushane jamani ili tucheke kidogo.
   
 2. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wenzio wanapiga nyundo kwenye internet hawapatikani mzee,si mafundi?na wakimaliza kazi wapo hoi so i think humu hakuna DIT kabisaaaaa!mwenyewe shahidi since jana hajatokea mtu?au wewe ulibadilisha fani?
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,975
  Likes Received: 23,657
  Trophy Points: 280
  Mkuu umekosea, yeye alitaka watu wa Dar Technical we unasema wa DIT. Vitu viwili tofauti kabisa. Anamaanisha enzi zileee za mwaaalim. Kama angetaka wa DIT mbona tumejaa lukuki? Hatupigi nyundo muda wote mdau tunapata ka muda ka kusurf pia.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Yegomasika,
  Mie nilikuwa Tech. College Arusha...... Je ulitokea shule gani kuja Dar Tech?

  Washikaji zangu hapo walikuwepo kibao. Akina Mgongo, Kasanga, Msaka, marehemu Mfwangavo, Godfrey M. Ntille (kwa sasa yuko Sumbawanga), Kyebala (mshikaji wa JKT, Mhaya wa maneno meeengi!!). Haya lete habari zaidi maana Dar tech na TCA walikuwa ni MAPACHA ambao ukichokoza mmoja, unaangukiwa na wengine......
   
 5. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Yeah, enzi akina Prof. Mwadosya na Luhanga walipokuwa wanasoma pale !
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu Gabu,
  Miaka ya 86-89 kilikuwa ni kipindi cha Mwinyi. Nyerere akiwa kama mwenyekiti wa CCM tu. Enzi akina Mwandosya na Luhanga wanasoma itakuwa ni zamani sana kama sikosei miaka ya 70 mwanzoni. Kwenye Wikipedia wanasema Mwandosya kamaliza Dar es Salaam Technical College-1969 ikiwa na maana miaka 20 ya nyuma. Kama sikosei ndiyo ilikuwa miaka hiyohiyo na marehemu Patrick Balisidya akisoma umeme hapo Dar Tech na akipigia Dar Jazz.
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,975
  Likes Received: 23,657
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha mbaaaali sana. Kina Lugundi (mzee wa misosi) Mwamafupa, Belela, Mbosoli, Mollel kina marehemu Method Mogella, Mh. George Simbachawene.(Mb) nakadhalika. Nakumbuka tulikuwa tunaenda kambi ya fisi kupata machozi ya simba kwa mama Seberee afu tunamalizia na kabia kamoja pale kwa anti kutoa harufu. TCA, kweli tumetoka mbaaali sana!
   
 8. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Du Kasanga na Msaka nilikuwa nao class moja pale Dar Tech, kwa hiyo utakuwa unamfahamu jamaa mmoja alikuwa hapo TCA miaka hiyo anaitwa Kayungilo?. Huyu tulikuwa nae Oljoro JKT.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kayungilo nilisoma naye kuanzia Mazengo. Ni homeboy wa Lipumba.
  Naona ulisomea masomo ya UMEME kama sikosei maana hao jamaa walikuwa kwenye hizo field. Yeep, hilo ndiyo kundi langu, vijana wa Sikonge............
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chrispin,
  Mie nilikuwa mwaka mmoja na marehemu Method Mogella na marehemu Saleh Sonda. Sonda alikuwa na shabaha kwenye miguu yule mtu ni hatari. Mzee Lugundi na misosi yake alikuwa hana noma. Tulikuwa tunawahi mapema kupata Top Layer na "ng'ombe". Ng'ombe ilikuwa linyama likubwa na mifupa..... ukiondoka nalo watu wanaanza kupiga makelele, buuuuu....

  Nimepata habari juzijuzi kuwa kijana mmoja wa Makelele sana akienda kwa jina la Cathbert Busumano amefariki. Sina habari zaidi ya amefariki.
   
 11. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #11
  Sep 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  jamani watu wa tca arrusha mnamkumbuka quizer au keisa alikua umeme, miaka ile alikua jina lake lingine ni solomoni nkya nae amefariki alikua mshkaji wangu saaana although mi nilikua mbeya tech mtc
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,975
  Likes Received: 23,657
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenikumbusha mbali. Nakumbuka utaalamu wangu wa kuvizia ng'ombe na kuvizia Top Layer. Na vile vimkate "vimbosoli". Unawakumbuka na 'vyura'? Wale wafanya usafi ambao mzee mzima ukizidiwa unakacha klasi unawavizia wakija kudeki unamvuta mmoja chumbani unafanya vitu vyako. Au tule tupishi tuliokuwa tunaleta msosi bwenini kama unaumwa. Mzee nilikuwa nazuga kuumwa ili niletewe msosi, then namaliza kazi. Hahahahahah!
   
 13. Akami

  Akami Member

  #13
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu Awalaze mahali pema peponi wale wote waliotutangulia mbele ya haki,AMINA.
  Ndugu tukumbushe ulikuwa intake ipi hapo TCA,kwenye Vimbosoli,

  Ila kaka Crispini noma unasingizia kuumwa ili uwapate wapishi,umalize?Aibu hiyo kwa mhandisi mtarajiwa,sitashangaa nikisikia umerudia form one ili uwapate mabinti wa form one!Ila kwa Technics uko juu mkuu!
   
 14. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,975
  Likes Received: 23,657
  Trophy Points: 280
  Ntake radhi. Nshakuwa mhandisi siku nyiiiingi sana. Mpaka nshasahau ilikuwa lini.
   
 15. Thegreatcardina

  Thegreatcardina JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 396
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  duh!!!!!!!!! huyo kayungilo tulisoma nae mazengo technical sec school
   
 16. Thegreatcardina

  Thegreatcardina JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 396
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Tupo kamanda. pale mie 1992 mpaka 1996. mechanical engineering. namkumbuka sana marehemu mwl. Flowin Sapula. Dr. Zakaria Mganilwa yupo SUA sasa hivi. kuu alikuwa Mr. Msoma
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Kule ndani kulikuwa pia kuna vile vitoto vinakuja kuvizia mikate iliyoachwa mle ndani. Watu wakawa wanaviita vindege. Siku moja kitoto cha Kahurananga kikaingia na chenyewe kuwa ndege "tukakitoa mbio hadi kwa baba yake". Tukakipa heavy warning na kipande cha mkate kuwa akitaka basi awe anatusubiri chumbani kwetu.

  Kahuranganga alikuwa ni Big Brother wetu kweli kweli. Jamaa alikuwa mtu mmoja safi sana na ndiyo maana kesi ya mwanae tuliifanya kama ni kesi yetu na hatukusubiri baba aone. Kwa kupenda mziki, tulikuwa tunapata Good time akituazima ile Radio Cassete yake aliyonunua German (Telefunken). Hilo readio lilikuwa na uwezo wa kudaka waves za Microphone wireless. Ilipokuja kwaya ya Kanisa kuu la Kilutheri pale TCA kwenye mashindano ya kuimba, waliimba nyimbo mpya kabisa ambazo hata hawajazirekodi. Kumbe Kahuranga anawarekodi kwa kutumia Mic iliyokuwa imewekwa mbele yao. Wakati wa chakula cha mchana, akaanza kuipiga ile miziki ambayo ilikuwa almost Studio Quality. Jamaa waliogopa sana na kumuomba asiuze wala kugawia watu maana ndiyo Investment yao.......

  Mwaka jana nilikuwa nataka cheti changu. Baada ya pilika za hapa na pale, Sambayuka akakubali na kumpatia dada yangu aliyekuwa Arusha anitumie. Nilipokipata nikampigia simu kumshukuru.

  Yule Mpishi mwenye Matusiiii, aitwaye Mama Hamza (kibonge cha mama) alikuja kumuokoa maisha rafki yangu. Kijana aliuguwa homa ya Matumbo na akienda hospital wanampa aspirin. Mama akampa kadi yake Familia na kwenda hospital fulani barabara ya Uhuru karibu na kanisa la Walokole, kama sikosei ni private (na aghali) na kijana akafanyiwa uchunguzi na kupewa dawa. Kijana alipona na gharama zote alilipa mama Hamza na mumewe. Yule mama milele sintamsahau. Ukimuona huwezi kudhani ni mtu mkarimu namna hiyo. MUNGU AMBARIKI KOKOTE ALIPO yeye na familia yake.
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,975
  Likes Received: 23,657
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenikumbusha mbaaaaali sana. Mzee Sambayuka! Sitamsahau mzee yule. Aliwahi kutupa pepa kila mtu na swali lake. Alichofanya swali ni lile lile lakini figure zinabadilika. Kwa mfano kama kwako Force ni 10N kwa mwingine ni 100N, mwingine 1000N mwingine 0.1N nk. Basi katugaia pepa alafu katoka nje. Watu tuna piga chabo kama kawaida.

  Majibu yanapotoka tunashangaa tunatofautiana kwenye decimal points. Mwingine anapata jibu Mass ni 10kg, mwingine 100kg, mwingine 1000kg mwingine 0.1kg. Tukawa tunashangaa. Ikabidi tumuulize kichwa wa darasa alikuwa anaitwa Christopher a.k.a Ngosha. Yeye jibu lake lilikuwa 100kg. Basi darasa zima tukaona labda tumekosea kwenye makalkulesheni. Wote tukaandika jibu kama la Ngosha bila kujua kila mtu alikuwa na tarakimu zake tofauti na wengine.

  Darasa Zima tukalamba Sup akiwemo Ngosha kwa kosa la kushea majibu yake.

  Sambayukha Sitamsahau mzee yule.
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sambayuka na ufupi wake, alimtishia Mrangi mmoja Pande la mtu akiitwa Tomola kuwa " I will throw you out through the window". Huwezi amini kuwa Tomola alinywea.

  Je wamkumbuka Ngosha akiitwa JILUGU? Huyu Mwalimu alikuwa mtu wa totos sana, yeye na yule Mhaya Rweikaza. Ila Rweikaza lilikuwa na akili mbaya. Linaweza kuropoka neno hadi huwezi amini. Siku moja walimkamata mama mmoja karani alikuwa kajaajaa vizuri tu. Sijui wakawa wanasema nini? Mie nimefika nikakuta mama anajisifu kuwa "si nitataifisha tu". Basi Jilugu likamjibu "nitakundika (huku akitandika hewani kidole) hadi uwe unalia mama wee, nimekoma..." Hapo Rweikaza linampa suport.....:)
  Yeye Rweikiza siku moja narudi shuleni, nimedika kwake nakuta anasafisha kile kigari chake. Hapo dada mmoja aitwaye Merina ndiyo anakwenda mjini na huo ulikuwa mwanzo wa term. Merina akamsalimia "shikamoo mwalimu.." Huyu jamaa badala ya kujibu, akamuangalia na kusema "ehhh, umefika tu na umeshaanza...." Yule dada alimuangalia yule mwalimu bila ya kuamini anayoyasikia.

  Naona nyie hilo darasa lenu lilikuwa la WAHINDI sana. Wote mkaamua KUNYONYESHA..... teteteteee. Wakumbuka hiyo term? Na neno "KUMWAGA?" Jamaa anasafisha chumba saafi na kusubiri mtoto aje siku hiyo, mtoto haji. Jamaa jioni wanamcheka kuwa "Sumu zake zimemwagikia kwenye jabali...".

  Mjinga mwingine alikuwa yule Zuberi. Huyu jamaa kaja kufungua Disco bila mke. Na kufika pale anasema "mie hapa nina ukame.... na kama kuna mwingine huko mwenye ukame basi kazi kwake". Ilibidi aopowe mtoto mmoja wa secondary wafungue Disco.
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Huyo Kayungilo atakuwa mwingine. Anaweza kuwa ndugu yake. Nitajaribu kumuuliza Kayungilo mkubwa kufahamu kama wanafahamiana.
   
Loading...