Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,531
- 3,331
Vibanda vya wafanyabiashara wadogo 'Machinga' na mama lishe zaidi ya 30 vimeteketea kwa moto katika Soko la Karume Jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo Aprili 8, 2022.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ACP), Muliro Jumanne Muliro amekiri kutokea kwa moto huo na kusema chanzo cha moto hakijajulikana lakini uchunguzi unaendelea, japo taarifa za awali zilionyesha kuwa moto ulianza kwenye kibanda kimoja na kisha kusambaa.
"Kwa mazingira yalivyo pale, vibanda vingi vimebanana na vipo kila baada ya hatua mbili, hivyo moto unapotokea ni rahisi kusambaa, bahati nzuri ni kuwa umeshadhibitiwa, na watu wa usalama wapo eneo la tukio," amesema Muliro.
Naye, Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Elisa Mugisha amesema timu yake imeudhibiti moto huo ambao pia umeunguza mabanda ya wafanyabiashara wa mabegi.
=================================
Majira ya muda wa saa 11 alfajiri ya leo, moto umewaka na kuteketeza soko la wamachinga wauza mabegi karume.
Matukio ya picha
Moto bado unaendelea kuwaka huku vikosi vya zimamoto na uokoaji vikiendelea na harakati ya kuuzima