DAR: Sheikh wa mkoa Alhad Mussa aongoza Mkutano wa Amani, Mzee Mwinyi akiwa mgeni rasmi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mkutano wa amani ulioandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini chini ya Sheikh wa mkoa Alhad Mussa Salim kama Mwenyekiti wa Kamati, umefanyika leo jijini Dar es salaam.

Mkutano huo umejadiliwa amani ya nchi sambamba na kuombea Taifa amani, pia ilikuwa fursa ya kukutana na Viongozi wa dini mbalimbali na kujenga mahusiano mema ya kibinadamu.

Akizungumza katika mkutano huo, mgeni rasmi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka Viongozi wa dini nchini kuanzisha kamati ya amani kila mkoa na ngazi ya Taifa ili kuwafundisha watu wote umuhimu wa amani kwa ajili ya kufikia maendeleo ya Taifa.

Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi alisema amani ndiyo kichocheo cha maendeleo, ikizingatiwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt. John Magufuli ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda.
FB_IMG_1523893448501.jpg
FB_IMG_1523893457496.jpg
FB_IMG_1523893442358.jpg
FB_IMG_1523893435823.jpg
 
Hivi mpaka leo hakuna asiyejua umuhimu wa amani mpaka kuhitaji kufundishwa?
 
Back
Top Bottom