Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

3 May 2021

KANDA YA PWANI YAMTAKA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI KUSHUGHULIKIA WAFUNGWA WA KISIASA


Watembelea familia ambazo wapendwa wao wapo mahabusu ili kuwafariji na pia kutoa wito kwa serikali ya awamu ya sita kutazama suala la makamanda wa CHADEMA waliopo gerezani kila kona ya nchi ya Tanzania.
 
“Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa Wafungwa wa Kisiasa 23, sio kweli Rais hajazungumza suala hilo, pili Nchi yetu haina Wafungwa wa Kisiasa, Watanzania wapuuze taarifa hizo”———Gerson Msigwa @gersonmsigwa , Msemaji Mkuu wa Serikali akiwa Dar es salaam leo

“Hiki Chombo cha Habari cha Nchi jirani nisingependa kukitaja tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo, tayari Ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wamepotosha”———Msigwa
 
27 March 2021
Mbozi Songwe,
Tanzania

MBUNGE CHADEMA VITI MAALUM SONGWE: Aja Kivingine Kabisa, Agawa Computer na Printer kwenye GEREZA




Mbunge wa CHADEMA anukuu maandiko takatifu yanayosema "Nalikuwa gerezani lakini hukuja kuniona" mwisho wa nukuu.

Hivyo kuna umuhimu kuwatembelea mahabusu na wafungwa kuwajulia hali waliopo gerezani.

Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefanya mema , anamalizia kusema maneno hayo ya hekima mbunge wa chama cha kisiasa cha CHADEMA nchini Tanzania.

Mbunge huyo wa CHADEMA ambaye pia aliwahi kurundikwa gerezani anasema anajua changamoto za kuwa ndani huku ukiwa bila ya sauti ya kuwatetea.

Mbunge huyo amesema yupo tayari kutumika kama daraja kusaidia kutatua changamoto za waliopo mahabusu au gerezani.
 
16 April 2021
Bungeni
Dodoma, Tanzania

Mbunge wa CHADEMA : Miaka 5 ya mahusiano ya serikali na upinzani yaibuliwa Bungeni, mfano kesi za mashaka, faini kubwa, vifungo vyawakumba wapinzani


serikali yawaomba viongozi wa Upinzani na wale wote waliokimbia Tanzania kwa sababu zozote kurejea Nchini ili kuijenga Nchi, hata hivyo Vyama vya Upinzani vyalilia Umoja na Serikali Bungeni; Mbunge Stella Fiyao wa chama cha CHADEMA alielezea yafuatayo.....
Source : BM TV TANZANIA
 
Hapa nakubaliana na kigogo2014 kwamba mama and walio juu yake maana kila anachoagiza wanakipinga na kuja na maagizo yao, mbona kwa Magufuli hakuna aliyekuwa anathubutu kuinua mdomo akishatamka jamo lake?!

Kwakweli kama Mama Samia ataendelea kukumbatia hawa wateule was marehemu atajikuta nchi haitawaliki!!
 
15 Apr 2021
Njombe, Tanzania

MWENYEKITI BAVICHA AKICHANGISHA MCHANGO KWA AJILI WA WAFUNGWA WA KISIASA




Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Mh. John Pambalu, amesema Bunge limegeuka Baraza la usuluhishi, ameyasema hayo Leo akizungumza na vijana wa Mkoa Njombe, kwenye muendelezo wa Ziara ya kuwaona wafungwa wa kisiasa magerezani wakiwa pamoja na Mratibu wa Bavicha Taifa Mh. Twaha Mwaipaya

Source : CHADEMA MEDIA TV
 
28 Apr 2021

"We still need to advocate for new laws that recognize Human Rights defenders ,"Olengurumwa



Protection Internationa Kenya -Side Event An Analysis of the status of Human Rights Defenders protection mechanisms in Tanzania and beyond

Source : WATETEZI TV
 
10 May 2021
Kilimanjaro, Tanzania

BAVICHA MKOA WA KILIMANJARO WAANZA ZIARA YA KUWATEMBELEA WAHANGA WA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA 2020


 

8 May 2021​

GERSON MSIGWA ATAKIWA KUACHA KUUPOTOSHA UMMA NA WADAU WA JUMUIYA YA KIMATAIFA JUU YA UWEPO WA WAFUNGWA WA KISIASA


Awamu ya sita inataka kujisahihisha lakini wahafidhina masalia wa awamu ya 5 wanataka kuzuia mabadiliko chanya ya wana CCM Asilia wanaoshikilia hatamu za uongozi wa sasa ktk serikali inayoongozwa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kufikia azma njema ya Tanzania yenye umoja wa kitaifa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom