Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba Rais Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa Mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.


Pia, soma: Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?
Ila ina wakimbizi wa kisiasa...!!!
Hivi wahanga kama kina Ben Saanane waliposhikiliwa kabla ya kupotezwa walipaswa kuitwaje?
 
Mbinyo wa kikanda umesaidia serikali sikivu ya awamu ya sita kuzichagiza ofisi za Mwendesha Mashitaka Mkuu na ile ya Mwanasheria Mkuu kuwabana waendesha mashitaka na mawakili wa serikali wenye kesi zisizo na mashiko wafikirie kuzifuta.
 
hehee he is rottening in hell. ameacha maumivu kwa watu ila sasa anaumia zaidi na magenge yake huku yanatawanyika. Nchi sasa inaamani
Unateseka bure tu!

Nchi bado iko mikononi mwa ccm,

System ni ile ile..
Ilani ni ile ile...


Kilichobadirika ni bavicha kuungana na uvccm kuidemkia ccm

Ccm mbele kwa mbele
 
Mh! hata ya uonevu yaliyo wazi? Hapo Kuna walakini Kama ni wazo la Mama. Kuna yaliyo wazi hayahitaji utaalamu. Mfano Mdude Chadema... tekwa potezwa, Mara kaonekana. Bambikwa kesi Mara Kashonda. Bambikwa madawa.
mdude chadema ni nyoko kabisa unamjua vizuri wewe mwache avune alichokuwa anapanda
 
..ulitegemea msemaji wa serikali akiri kwamba Mama Samia ameamuru waliokamatwa kwa sababu za kisiasa waachiwe?

..its about time ccm iache kutumia vyombo vya ulinzi na mahakama kisiasa. Waache vyombo hivyo vitekeleze majukumu yake bila upendeleo.
Kwa hiyo serikali ya kipenzi chako inadanganya?

Utakuwa umekosa uteuzi wewe…si bure!
 
3 May 2021
Bukoba, Tanzania

ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA NA WENZAKE 6 WAACHIWA HURU "HALI YANGU SIO NZURI"



Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imewaachia huru washitakiwa saba akiwemo aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia tiketi ya Chadema Jimbo la Bukoba Mjini 2020 Chief Kalumuna ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa nane yakiwemo ya kusababisha fujo,kutotii,kusababisha uharibifu wa mali siku ya kuwaapisha mawakala na wagombea tarehe 21 mwezi wa 10 mwaka 2020.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Bukoba Joseph Lwambano amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuthibitishwa hivyo inaonyesha washitakiwa hawakuhusika.

Akiongea nje ya mahakama mshitakiwa namba moja Chief Kalumuna ameeleza furaha yake baada ya kuachiwa huru.

Tarehe 13 May 2021 chief Kalumuna atarudi tena kusimama mahakamani kwa tuhuma ya mambo yaliyotokea tarehe 28 October 2020. Hivyo awaomba wote kumuombea siku hiyo ya kesi nyingine inayomkabili.

Source : millard ayo

N.B

Kutoka Maktaba Uchaguzi wa 2020

 

Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba Rais Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa Mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.

Akieleza jambo hilo, Gerson Msigwa amesema:

"Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi. Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa 23. Siyo kweli. Rais hahajazungumza suala hilo. Pili, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa. Watanzania wapuuze taarifa hizo"

"Hiki chombo cha Habari cha nchi jirani, nisingependa kukitaja, tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo. Tayari ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wmepotosha"



Pia, soma: Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?

Waziri wa Sheria na Katiba yupo wapi?
 
Back
Top Bottom