Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,441
- 7,780
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba Rais Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa Mahakama.
Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.
Akieleza jambo hilo, Gerson Msigwa amesema:
"Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi. Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa 23. Siyo kweli. Rais hahajazungumza suala hilo. Pili, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa. Watanzania wapuuze taarifa hizo".
"Hiki chombo cha Habari cha nchi jirani, nisingependa kukitaja, tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo. Tayari ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wmepotosha".
Pia, soma: Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?