Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,426
7,737


Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba Rais Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa Mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.

Akieleza jambo hilo, Gerson Msigwa amesema:

"Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi. Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa 23. Siyo kweli. Rais hahajazungumza suala hilo. Pili, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa. Watanzania wapuuze taarifa hizo".

"Hiki chombo cha Habari cha nchi jirani, nisingependa kukitaja, tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo. Tayari ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wmepotosha".



Pia, soma: Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?
 
Serikali, kupitia msemaji wake muda fupi uliopita imekanusha habari zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha Kenya kuwa Rais Samia kaagiza wafungwa 23 wa kisiasa waachiwe huru.

Msemaji huyo kasema kuwa:

1. Tanzania haina wafungwa wa kisiasa.

2. Rais Samia hajatoa agizo kama hilo ambalo kimsingi linaingilia shughuli za mahakama.

Shame on Citizen TV.
 
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba raia Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.
What are these Kenyans up to!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom