Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Tufanye rejea

20 May 2019

MDUDE Alivyomwaga 'MACHOZI' Hadharani "NINA KOSA GANI"

Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mdude Nyagali ameelezea namna alivyotekwa mpaka kuokolewa.

Akizungumza Leo tarehe 20 May 2019 na waandishi wa habari katika ofisi za Makao makuu ya Chama hicho Jijini Dar es Salaam Mdume amesema kuwa utekwaji wake unahusiana na siasa na kubainisha kuwa hana mpango wa kuhama Tanzania na wala haofii kifo.

Aidha amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa anaendelea vizuri japo bado anaendelea kupata matibabu. Mdude alivamiwa kisha kuchukuliwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake Mbozi Mkoani Songwe Siku ya Jumamosi Tarehe 4 Mei 2019 na kupatikana usiku wa May 8 mwka huu

Source : Global TV online
 
Rejea :

9 May 2019

BREAKING: MDUDE Akiwa HOI Kitandani,
KAONGEA Haya!

SAA chache baada ya mawakili watatu kuwafungulia kesi maofisa wa polisi na vikosi vya usalama kuhusu madai ya kutekwa nyara na kuzuiliwa kinyume na sheria kwa mfanyabiashara na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali ‘Mdude Chadema’, amepatikana ametupwa katika Kijiji cha Makwenje, kata ya Inyala mkoani Mbeya, akiwa hai usiku wa kuamkia leo.

Mdude anadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake Vwawa, Mbozi mkoani Songwe siku nne zilizopita‬. Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Masonga, amesema: “Mdude amepatikana katika Kata ya Inyala Mkoani Mbeya, usiku akiwa katika hali mbaya ingawa anajitambua na anazungumza kwa mbali, amepigwa sana na amevimba, amekutwa na kadi ya chama chake (Chadema) na kitambulisho cha mpiga kura.”

Source : Global TV online
 
Tufanye rejea

20 May 2019

MDUDE Alivyomwaga 'MACHOZI' Hadharani "NINA KOSA GANI"

Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mdude Nyagali ameelezea namna alivyotekwa mpaka kuokolewa.

Akizungumza Leo tarehe 20 May 2019 na waandishi wa habari katika ofisi za Makao makuu ya Chama hicho Jijini Dar es Salaam Mdume amesema kuwa utekwaji wake unahusiana na siasa na kubainisha kuwa hana mpango wa kuhama Tanzania na wala haofii kifo.

Aidha amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa anaendelea vizuri japo bado anaendelea kupata matibabu. Mdude alivamiwa kisha kuchukuliwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake Mbozi Mkoani Songwe Siku ya Jumamosi Tarehe 4 Mei 2019 na kupatikana usiku wa May 8 mwka huu

Source : Global TV online

Aiseeee
 
Rejea :​

13 May 2020​

Lissu : Nasikia polisi wanataka kumpa kesi ya madawa kulevya Mdude Nyagali​

May 13, 2020 10:51 am EAT

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema amesikia jeshi la polisi wanampa Nyagali Mdude kesi ya dawa ya kulevye ili asipate dhamana.
Mdude ambaye ni mwanachama wa Chadema anashikiliwa na jeshi la polisi tangu Mei 10, 2020.
Lissu aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter huku akisema kuwa kushtakiwa watu kwa makosa ya uongo hakujawahi kuzuia harakati za kudai haki mahali popote duniani.
“Sana sana mnamuongezea chuki dhidi ya huyo mnayefikiria mnamsaidia,” aliandika Lissu.
Nasikia Jeshi la Polisi la Tanzania ya Magufuli wanampa Mdude Nyagali kesi ya madawa ya kulevya ili asipate dhamana. Kushtaki watu kwa makosa ya uongo hakujawahi kuzuia harakati za kudai haki mahali popote duniani. Sana sana mnaongeza chuki dhidi ya huyo mnayefikiria mnamsaidia.
— Tundu Antiphas Lissu (@TunduALissu) May 12, 2020
 
28 June 2021
Mbeya, Tanzania

Mdude : Natoa Shukurani kwa Mungu wangu mkubwa kuliko vyote

Siku 414 za kukaa gerezani kwa tuhuma za kesi ya jinai zimefika mwisho baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Mbeya kumuona mtuhumiwa Mdude hana hatia baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la Mdude
 
28 June 2021
Mbeya, Tanzania

MANENO YA KWANZA YA MDUDE NYAGALI BAADA YA KUACHIWA HURU NA MAHAKAMA.

28 June 2021
Mbeya, Tanzania

WAKILI WA MDUDE AFUNGUKA WALIVYO SHINDA KESI DHIDI YA JAMUHURI.

Wakili msomi Faraja Mangula aliyeisimamia kesi hii hadi hitimisho leo, asema haki imetendeka kama Mahakama ilivyoamua leo kwa kuwa tangu mwanzo aliamini mtuhumiwa hakuwa na hatia na leo mahakama imethibitisha hili kwa kina ktk hukumu ya yake.

Nao uongozi wa CHADEMA kanda ya Nyanda za Juu Kusini umesema bado kuna makada 47 wa CHADEMA ambao bado kesi zao zinaendelea katika mkoa wa Songwe hivyo wanaendelea na juhudi za kuzifuatilia kesi hizo hadi haki ipatikane.
 
Back
Top Bottom