Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
622
1,000

Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba Rais Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa Mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.

Akieleza jambo hilo, Gerson Msigwa amesema:

"Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi. Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa 23. Siyo kweli. Rais hahajazungumza suala hilo. Pili, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa. Watanzania wapuuze taarifa hizo".

"Hiki chombo cha Habari cha nchi jirani, nisingependa kukitaja, tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo. Tayari ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wmepotosha".Pia, soma: Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,734
2,000
Serikali, kupitia msemaji wake muda fupi uliopita imekanusha habari zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha Kenya kuwa Rais Samia kaagiza wafungwa 23 wa kisiasa waachiwe huru.

Msemaji huyo kasema kuwa:

1. Tanzania haina wafungwa wa kisiasa.

2. Rais Samia hajatoa agizo kama hilo ambalo kimsingi linaingilia shughuli za mahakama.

Shame on Citizen TV.
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,101
2,000
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba raia Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.
What are these Kenyans up to!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom