Dar: Sasa ni zamu ya madalali kuisoma namba!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,903
2,884
Kiama cha madalali mkoa wa Dar es Salaam kimewadia. Madalali Dar es Salaam wanachangia kuwaongezea wakazi ugumu wa maisha kutokana na kupandisha kodi za vyumba. Hivyo serikali mkoa wa Dar itawalazimisha kuunda chama na kuwasajili.
 
Ana nyumba za kuwapangishia wanaohitaji ili wasiende kwa madalali? Huyu jamaa bwana ajikite kwanza kusafisha jiji maana linatia aibu kwa uchafu mambo ya nyumba za watu hayawahusu, wasiotaka madalali wasubiri nuymba za NHC.
Usipende ubishi. Amekuambia madalali watakuwepo, ila atawaundia chama ili waweze kuendana na hali halisi ya maisha, na sio kujipangia tu bei.
 
Real Estate Agenct Act inakuja.....ni suruhisho tosha....na si tu itakua suruhisho kwa DSM tu bali tanzania nzima
 
Dalali ndio anapanga bei au mwenye nyumba?! Eti chama cha madalali.
Itakuwa hujawahi kupanga, au kupangisha nyumba. Mimi nina nyumba saivi napangisha, unaweza kutafuta hilo tangazo hapa jf, nahitaji 150,000 kwa mwezi, ila jana nimewakabidhi madalali, wameniambi wakija na mteja juu ya hapo nisikatae maana wao wanatafuta hela. Nadhani umeelewa
 
Itakuwa hujawahi kupanga, au kupangisha nyumba. Mimi nina nyumba saivi napangisha, unaweza kutafuta hilo tangazo hapa jf, nahitaji 150,000 kwa mwezi, ila jana nimewakabidhi madalali, wameniambi wakija na mteja juu ya hapo nisikatae maana wao wanatafuta hela. Nadhani umeelewa
Nimekuelewa ndio maana nimesema waachwe madalali wenyewe na wewe kama unaweza pia acha kutumia madalali kama ni rahisi, nina nyumba na nina dalali wa kudumu mpangaji akaihama namvutia waya, mie nataka changu tu watakacho kubaliana huko hakinihusu..
 
Kiama cha madalali mkoa wa Dar es Salaam kimewadia. Madalali Dar es Salaam wanachangia kuwaongezea wakazi ugumu wa maisha kutokana na kupandisha kodi za vyumba. Hivyo serikali mkoa wa Dar itawalazimisha kuunda chama na kuwasajili.
Wakati mwingine mawazo ni finyu sana, madalali wa nyumba sio kama wa makari au wa wapi, madalali wa nyumba hawahusiki kabisa sawa la bei ya nyumba ya kupanga, anaepanga bei ya nyumba ni mwenye nyumba, dalali yeye anachotaka apate ya mwezi mmoja, ndio mana madalali wakati mwingine wanamshawishi mwenye nyumba apunguze bei ya nyumba ili apate ya ule mwezi
 
Ana nyumba za kuwapangishia wanaohitaji ili wasiende kwa madalali? Huyu jamaa bwana ajikite kwanza kusafisha jiji maana linatia aibu kwa uchafu mambo ya nyumba za watu hayawahusu, wasiotaka madalali wasubiri nuymba za NHC.
Punguza hasira, hawa mbwa ni wa hovyo sana. DOGS, walafi sana.
 
Habari wana jamvi!

Nimeona leo kulizungumzia japo kwa ufupi kuhusu swala potofu juu ya madalali wa nyumba za kupanga, kumekua na malalamiko mengi kuhusu madalali wa nyumba/vyumba kupandisha bei halisi ya nyumba au chumba ili kupata cha juu, niwaambie tu dalali yoyote wa nyumba ya kupanga hahusiki kabisa kwenye bei ya pango, dalali wa kupanga si kama wa kiwanja, nyumba ya kuuza au magari nk. Dalali wa nyumba yakupanga anachoangalia ni mteja kuingia apate ile ya mwezi mmoja kulingana na bei ya nyumba kwa mwezi, wakati mwingine dalali anahusika kumshawishi mwenye nyumba ili ampunguzie mteja kama mteja kafikia kiwango flani, na wakati mwingine anamwambia mwenye nyumba kwa bei yako nyumba itaka sana ni heri upunguze, chukulia mfano nyumba ni ya 300k mteja ana 280k mimi ninachoangalia ni mteja kupanga ili nipate ile ya mwezi, hapo lazima nitaungana na mteja kumwambia mwenye nyumba hali ni mbaya mpunguzie mteja, kwaniyo nyumba ya 300k hata siku moja dalali hawezi kukuambia ni ya 400k hilo sahau, Dalali anatamani nyumba ya 300k mwenye nyumba ashushe 200k ili apate wateja haraka, kumbuka madalali wako wengi, kama ni mteja wa uhakika nisipomshawishi bosi apunguze mteja alipie, badae dalali mwingine akileta nakosa hata ile, kwahiyo swala la kwamba dalali anahusika kwenye swala la kupanga bei halipo, naamini wenye nyumba tunakibaliana na hili na madalali pia,

Wengi wamekua na kawaida sana ya kuwatukana na kuwaponda madalali ila kumbuka wengi wamekua msaada kwa watu kupata nyumba, kama hutaki kuwatumia madalali basi nyanyuka kwenye kiti chako ofisini hapo kazunguke mtaa kwa mtaa kutafuta nyumba ambayo ipo wazi upange,

Kumbuka nakubaliana sana na wazo kua ni lazima madalali wasajiliwe ili kufanya kazi kiufanisi na weledi, na pia kutafuta mfumo mzuri ambao hautaleta vikwazo kwa dalali, mpangaji na mwenye nyumba, kwahiyo nakubaliana kabisa na wazo la kuunda vyama vya madalali na kusajiliwa!

Pia nakubaliana na kuwapa pole waliosumbuliwa na madalali, kumbuka sijakataa kama ni kweli wapo matapeli, wazenguaji, pia waswahili, na ni kweli inasikitisha pale dalali anapompamba mteja kua nyumba kali ipo wahiii itaondoka, mteja akija anakuta banda la kuku, hii ni kwasababu wengi hawajaelewa kua wakifanya hii kazi kwa weledi ni manufaa kwao, wengi wamekua wanaangalia tu pesa ya hapa na pale ya kula na si kuboresha kipato!
Kumbuka si wote binadam wanafanyana, kila kitu kina changamoto zake, kikubwa ni kupunguza changamoto!
 
Back
Top Bottom