Dar: RC Makalla akerwa na ukamataji na faini za ‘wrong parking’

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
- Asema watekelezaji hawana weledi na kusababisha kero na taharuki.

- Aitisha kikao Cha dharuracha Wakurugenzi na TARURA kujadili.

1627044553706.png

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameonyesha kukasirishwa na utaratibu usiofaa wa ukamataji wa magari kwenye maegesho yasiyo rasmi "wrong parking" ambapo ameelekeza kuhitishwa kikao Cha pamoja baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA ili kupatia ufumbuzi Jambo hilo.

RC Makalla amefikia hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko mengi ya Wananchi juu ya utaratibu mbovu unaotumika na kusema Kama kiongozi hawezi kuruhusu Jambo hilo liendelee.

Aidha RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.

Mheshimiwa Makalla amesema hayo wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Jengo la utawala la Manispaa ya Ubungo ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka Watumishi kutoa huduma Bora kwa wabanchi.

Hata hivyo RC Makalla ameipongeza Manispaa hiyo kwa ukusanyaji Mapato Jambo linalopelekea waanze kutekeleza miradi kwa Fedha za ndani na pia kutumia Force akaunti kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasua ikiwemo Jengo hilo la utawala.

Juzi nilimsikiliza mkuu wa hao wakamataji , ni muungwana sana. Aliomba wakamataji wajikite kutoa elimu zaidi kuliko kutisha walioegesha vibaya. Pia alitaka viongozi wa dini wasikamatwe.

Hawa wapuuzi wana mkwara wao ''Mpeleke yard huyo'' ujue hapo wanaandaa mazingira ya kukupiga.
 
Asema watekelezaji hawana weledi na kusababisha kero na taharuki.

- Aitisha kikao Cha dharuracha Wakurugenzi na TARURA kujadili.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameonyesha kukasirishwa na utaratibu usiofaa wa ukamataji wa magari kwenye maegesho yasiyo rasmi "wrong parking" ambapo ameelekeza kuitishwa kikao cha pamoja baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA ili kupatia ufumbuzi Jambo hilo.

RC Makalla amefikia hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko mengi ya Wananchi kuhusu utaratibu mbovu unaotumika na kusema kuwa yeye Kama kiongozi hawezi kuruhusu Jambo hilo liendelee.

Aidha RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.

Makalla amesema hayo wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la utawala la Manispaa ya Ubungo ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka Watumishi kutoa huduma Bora kwa wabanchi.

Hata hivyo RC Makalla ameipongeza Manispaa hiyo kwa ukusanyaji Mapato Jambo linalopelekea waanze kutekeleza miradi kwa Fedha za ndani na pia kutumia Force akaunti kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasua ikiwemo Jengo hilo la utawala.
 
Juzi nilimsikiliza mkuu wa hao wakamataji , ni muungwana sana. Aliomba wakamataji wajikite kutoa elimu zaidi kuliko kutisha walioegesha vibaya. Pia alitaka viongozi wa dini wasikamatwe.

Hawa wapuuzi wana mkwara wao ''Mpeleke yard huyo'' ujue hapo wanaandaa mazingira ya kukupiga.
Cha muhimu ni watu wafuate sheria. Kama mtu anapaki sehemu isiyoruhusiwa inatakiwa ..... elimu peke yake haiwezi kusaidia epecially kwa sisi wabongo. Labda tatizo ni jinsi gani sheria au adhabu inasimamiwa.
 
Wale jamaa ni Wahuni sana sana, usiombe Mungu ukutane nao, rushwa hao kama umepaki Lori ni kuanzia laki tatu!
Wanapendelea sana mitaa ya Maji Chumvi, Mabibo Mwisho, NIT, Mahakama ya ndizi, Loyola, Kigogo na baadhi ya maeneo pale jangwani.

Hawa wana deal na malori zaidi, wanakodisha Noah wanajifungia humo wanakuwa wanakuvizia tu.

Ni zaidi ya mbwa, ni washenzi wa kutupwa. Pia wanapemdelea Morogoro road wakikuta Lori limepata breakdown kwao ni furaha!

Usiombe ukutane nao
 
Hawa wenye magari ndiyo anawapigania na wale tuliolalamika alichotufanyia kule Mbezi anaona siyo kero, this is double standard ya namna ya kushughulikia malalamiko, wanyonge wakilalamika "no action" wenye magari na uwezo wakilalamika "vikao kujadili kero mara moja" I stand to be corrected, huyu RC si muungwana hata kidogo, ninawasihi watanzania wenzangu tumpigie kelele, tunaoteseka mbezi terminal ni wengi zaidi kuliko wanaolalamikia wrong parking.
 
Mnateseka na nini mbezi terminal mkuu?
 
- Asema watekelezaji hawana weledi na kusababisha kero na taharuki.

- Aitisha kikao Cha dharuracha Wakurugenzi na TARURA kujadili...
Aidha RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.
 
Aidha RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.
Wale jamaa wana njaa balaa,na hawana ubinadamu hata kiduchu mbwa wale
 
Hawa wenye magari ndiyo anawapigania na wale tuliolalamika alichotufanyia kule Mbezi anaona siyo kero, this is double standard ya namna ya kushughulikia malalamiko, wanyonge wakilalamika "no action" wenye magari na uwezo wakilalamika "vikao kujadili kero mara moja" I stand to be corrected, huyu RC si muungwana hata kidogo, ninawasihi watanzania wenzangu tumpigie kelele, tunaoteseka mbezi terminal ni wengi zaidi kuliko wanaolalamikia wrong parking.
Watu wanaonewa sn
 
Wengine wapo nje ya hospitali ya muhimbili hao ni bala wanatumia bajaji na bodaboda.
 
Back
Top Bottom