johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,777
- 141,645
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Amos Makala amepiga marufuku uchangishaji wa michango yoyote katika shule za mkoa wake.
Makala amesema kama ni michango basi itaamuliwa na wananchi wenyewe na kuidhinishwa na serikali kabla ya kuanza kuchangishana.
Chanzo: Clouds Media
-----
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amepiga marufu michango inayotozwa kwa wazazi wa wanafunzi wa shule za Serikali mpaka hapo atakapotoa kibali chake.
Ametoa agizo hilo leo Jumatano Septemba 1, 2021, kwenye mwendelezo wa kusikiliza kero za wakazi wa mkoa huo ambapo leo ni zamu ya Wilaya ya Ilala na mkutano huo unafanyika viwanja vya Ghana Buguruni.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mmoja wa wananchi, aliyejitambulisha kwa jina la Abinani Lukwale, kueleza kuwa michango imezidi kuwa mingi shuleni na mengine wasipotoa watoto wao hurudishwa nyumbani au kunyimwa kufanya mitihani ambapo kila siku hutakiwa kutoa Sh300 na Jumamosi Sh1,000.
Akilitolea maagizo Makalla amesema kuanzia sasa anapiga marufuku michango hiyo mpaka pale itakapopata ridhaa yake.
"Kama shule ina wanafunzi 2,000 ina maana shule inakusanya Sh600,000 na hapo bado Sh1,000 ambazo wanazikusanya kila Jumamosi kwa watoto hao.
"Ukweli ni kwamba michango hiyo huwaongezea mzigo wazazi wakati serikali ishaamua kutoa elimu bila malipo,hii sitaikubali ndani ya uongozi wangu," amesema.
Kutokana na hilo amesema kuanzia sasa michango yoyote lazima iidhinishwe na yeye mwenyewe na hii ni baada ya kikao cha wazazi na uongozi wa shule kama ambavyo muongozo wa elimu unavyoelekeza.
Katika hatua nyingine amekataza biashara zinazofanywa pembezoni mwa shule ili kuwawekea mazingira mazuri watoto kusoma.
Badala yake ametaka kuwekwa utaratibu wa watu watakaotambulika na uongozi wa shule kufanya biashara zao ndani ya shule.
Ameagiza watendaji kulisimaamia hilo kwa kutoa elimu na kuweka vibao vya makatazo.
Chanzo: Mwananchi