Dar: RC Amos Makalla amepiga marufuku michango yote inayochangishwa shuleni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,240
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh Amos Makala amepiga marufuku uchangishaji wa michango yoyote katika shule za mkoa wake.

Makala amesema kama ni michango basi itaamuliwa na wananchi wenyewe na kuidhinishwa na serikali kabla ya kuanza kuchangishana.

Chanzo: Clouds Media
-----
makalla.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amepiga marufu michango inayotozwa kwa wazazi wa wanafunzi wa shule za Serikali mpaka hapo atakapotoa kibali chake.

Ametoa agizo hilo leo Jumatano Septemba 1, 2021, kwenye mwendelezo wa kusikiliza kero za wakazi wa mkoa huo ambapo leo ni zamu ya Wilaya ya Ilala na mkutano huo unafanyika viwanja vya Ghana Buguruni.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mmoja wa wananchi, aliyejitambulisha kwa jina la Abinani Lukwale, kueleza kuwa michango imezidi kuwa mingi shuleni na mengine wasipotoa watoto wao hurudishwa nyumbani au kunyimwa kufanya mitihani ambapo kila siku hutakiwa kutoa Sh300 na Jumamosi Sh1,000.

Akilitolea maagizo Makalla amesema kuanzia sasa anapiga marufuku michango hiyo mpaka pale itakapopata ridhaa yake.

"Kama shule ina wanafunzi 2,000 ina maana shule inakusanya Sh600,000 na hapo bado Sh1,000 ambazo wanazikusanya kila Jumamosi kwa watoto hao.

"Ukweli ni kwamba michango hiyo huwaongezea mzigo wazazi wakati serikali ishaamua kutoa elimu bila malipo,hii sitaikubali ndani ya uongozi wangu," amesema.

Kutokana na hilo amesema kuanzia sasa michango yoyote lazima iidhinishwe na yeye mwenyewe na hii ni baada ya kikao cha wazazi na uongozi wa shule kama ambavyo muongozo wa elimu unavyoelekeza.

Katika hatua nyingine amekataza biashara zinazofanywa pembezoni mwa shule ili kuwawekea mazingira mazuri watoto kusoma.

Badala yake ametaka kuwekwa utaratibu wa watu watakaotambulika na uongozi wa shule kufanya biashara zao ndani ya shule.

Ameagiza watendaji kulisimaamia hilo kwa kutoa elimu na kuweka vibao vya makatazo.

Chanzo: Mwananchi
 
bado DSM inahitaji RC makini zaidi.
Binafsi sijaridhishwa kivilee na Makala, bado sijaona mikakati yake ya kubadilisha Jiji.
Changamoto bado ni nyingi wakati spidi yake ni ndogo sana ya kuzishughulikia.
nikama vile anaelemewa!!
Tunamuomba ajipange vyema ili kuleta mabadiliko ktk mkoa wa DSM.
1. Aongeze spidi zaidi.
2. ma DC wake wanatakiwa wachangamke
3. watendaji wake wote ktk mkoa wachangamke.
Ukali ni muhimu sana ktk Jiji hili maaana kuna wapigaji kila kona.
 
The usual brain that creates the problem will certainly not capable enough to solve therein
 
Ondoeni malori kariakoo
Yanachelewesha maendeleo,
Kariakoo imekuwa kama gereji tu
Haina cha mipango miji wala nini kazi ni kuzulumiana tu,
Ukipaki kidogo unapigwa faini, ila milori inatoa sijui nini imejazana kama yote
Bora tuhame dodoma tu
Tuwaachie jimji lao lifilie mbali
 
Back
Top Bottom