Dar: Rais Magufuli anaongoaza Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais Magufuli anaongoza Mkutano huo unaoendela katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe

==============

Rais wa Tanzania, John Magufuli ametaja baadhi ya sababu zinazofanya wakandarasi wa ndani kushindwa kupewa miradi mikubwa ili kuitekeleza.

Miongoni mwa sababu hizo ni kukosa umoja na ushirikiano kati yao, kuendeleza vitendo vya rushwa, wakandarasi kuwa wazito kuomba zabuni ya kutekeleza miradi mikubwa inayotangazwa nchini na wengine wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi wasio waadilifu wa serikali kuomba zabuni.

Magufuli amebainisha hayo leo Jumatano ya Septemba 4, 2019 katika mkutano uliowakutanisha watumishi wa bodi tatu zilizo chini ya wizara hiyo ikiwemo, Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) jijini Dar es Salaam.

Amesema mwaka jana nakumbuka tulitangaza mradi wa barabara ya kutoka Chamwino kwenda mjini Dodoma na nilitegemea kabisa kilomita 20 zitaombwa na kampuni za wazalendo wala hawakuomba. “Kuna miradi mingine midogo tu ya kuongeza mita 500 kama ile ya uwanja wa Dodoma, wazalendo hawakuomba, ninaweza nikataja miradi mingi na hapa unaweza ukajiuliza, hawa wazalendo kampuni zao hazijui kuomba kazi, hawana utaalamu wa kufanya au tatizo liko wapi,” amesema Magufuli amesema wakati mwingine hata miradi ya ndani midogo kabisa ambayo alidhani kampuni za ndani zitaomba hazifanyi hivyo.

“Lakini wakati mwingine kupata zabuni mmekuwa mkishirikiana na wafanyakazi wasio waadilifu wa serikali, bado ndani ya serikali kuna watendaji wasio waadilifu na ndiyo maana wakati mwingine makadirio ya fedha inayowekwa kwenye miradi inakuwa iko juu sana.” “Kukosa ujuzi wa kusimamia miradi kwa baadhi ya wakandarasi wa ndani imekuwa ikichangia baadhi yao kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati, kutekeleza miradi chini ya kiwango na gharama zao kuwa juu sana,” amesema

Magu1.jpeg

Magu2.jpeg
 
Rais Magufuli anaongoza Mkutano huo unaoendela katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe

Vipi hawezi Kuwaomba hao ' Wataalam ' watutengenezee / watuundie Ndege mpya ili tuachane na ile iliyopo Sebuleni kwa Mkulima Herman Steyn na Sisi tuweze ' Kumkomoa ' kama Yeye alivyotufanyia kama siyo Kutuaibisha Taifa Kubwa hili na Yeye akiwa kama Mwenyekiti ' Mbichi ' kabisa wa SADC?
 
Mwenyezi mungu bana huwa ana mitihani yake.Yaan unapewa Uenyekiti wa SADC halafu nchi mwanachama inakamata ndege yako,Muda huo huo raia wako na nchi wanachama wanauwawa katika nchi hiyo hiyo.Inaishia kupongezwa bungeni kwa ku ukwaa uenyekiti mpya.Basi bana mdomo koma hebu nitafute video ya GWAJI BOY njikumbushe.
 
Umenifurahisha sana kwa maneno yako
Mazito yenye nguvu na ya ujasiri mbele ya
Mpendwa Rais wetu uliyoyanena .
Mungu akubariki nimetoa machozi ya furaha maana umenigusa kabisa.
Asante sana.Mungu amekutumia kwa ajili ya wengi walioumizwa.Mungu akuinue zaidi juu kabisaaa.
 
Jamani nimebahatika tu ndo anasimama kuomba kwenye huo mkutano wamashauriano wa wadausekta ya ujenzi Tz sijaweza kurecord.
 
Rais ni kama ameishiwa kazi za kufanya sasa ni kutafutiza tafutiza tu mara watendaji kata baadaye ataita hata nyumba kumi ikulu.
 
Kule Uganda ma Engineer wanaomaliza vyuo vikuu Museveni uwawezesha wanaoungana nakuunda umoja katika sector ya ujenzi inaitwa ENTANDIKWA YAANI CHANZIO (Initial Capital ).Kwa kuwa hakuna hajira na shughuri za ujenzi wanapewa jeshi vijana wengi hawana ajira ingefaa tuinge mfano wa Museveni kuwawezesha ma Engeneer wachanga wawezi kujiendeleza katika fani zao
 
Vipi hawezi Kuwaomba hao ' Wataalam ' watutengenezee / watuundie Ndege mpya ili tuachane na ile iliyopo Sebuleni kwa Mkulima Herman Steyn na Sisi tuweze ' Kumkomoa ' kama Yeye alivyotufanyia kama siyo Kutuaibisha Taifa Kubwa hili na Yeye akiwa kama Mwenyekiti ' Mbichi ' kabisa wa SADC?
Sikujua ndege hujengwa kwa Zege haya ni maajabu ya bongo tu😂😂😂
 
"Ili mtumbwi ule uweze kuelea ...law of flotation ni sector ya ujenzi ile"
 
Back
Top Bottom