DAR: Polisi yapiga marufuku mazoezi ya kukimbia 'Jogging' barabarani bila kupata vibali

Asante Mungu.. Hakuna kitu kinakera kama hawa ndugu zetu wanapita asubuhi na makelele mengiii watu weekend ndio tunapumzika.. Nilikuwa naudhika sana..

Pita kimya kimya fika uwanjani au baharini fanya mazoezi ukimaliza rudi kwenu... Watu wanaacha uwanja temeke wakuja posta mazoezi gani hayo.
 
Huu ni ujinga mwingine. Wewe kamanda jiongeze vhukua fursa kuongea na Makamu wa Rais. Mazoezi miji mikuu yafanyike wapi? Kukataza pekee ni ujuha na subordination kwa boss wako.

Mzee hujawahi kutana na hivi vikubdi vimeziba njia na wewe unataka wahi kazini. Tuulize wakazi tunaotumia njia ya Ununio ukibahatika kukutana na hawa waungwana foleni yake.
 
Sawa kabisa. Hawa watu huwa siwaelewi ujue! Huwa shida yao ni kufanya mazoezi au ku capture public attention?

Maneo ya wazi yako mengi sana sasa yanini kuhatarisha uhai kufanya mazoezi kwenye barabara ambazo ziko busy magari 24/7.

Acheni hizo show off kwenye masuala ya msingi
Ubarikiwe. Sana. Mtu unawahi halafu majobless tupu kiburi kingi kunakipindi na ugonvi huku mjini..wengine watoto.. Madili f tena wako nje ya majumbani mwao wanakuwa machokoraa tuu..

Watu wanatoka temeke keko wanapita barabara zamjini humu full vurugu.. Wanaacha viwanja chungu mbovu huko watokako mashuleni, mwembe Yanga, uwanja wa taifa.. Na naamini kila sehemu wanaviwanja kwann wasiende huko?!
 
Waruhusiwe tu ila watumie service roads na kule ambako hakuna service Road watumie barabara ambazo sio njia kuu ya magari
 
Sheria zetu zipo wazi kabisa.. kusanyiko lolote lazima liwe na kibali, na hii hizi taratibu zipo toka zamani sema watu walikuwa wanaleta mazoea kwenye Taratibu na Sheria
 
Mkuu hayo maeneo mengi ya wazi unayosema ni yepi?
Naomba yataje baadhi!
Halafu huwa inategemeana na convenience ya Mtu , mfano mwingine atokapo kazini jioni huwa anarudi nyumbani Kwa njia ya Mazoezi !
Na makazi ya watu yametawanyika!
Nitajie Public Gaderns Za Mazoezi Kama zipo!
Mkuu kila kitu kinapaswa kufanywa kwa wakati na mahali pake. Mazoezi kama sehemu nyingine yoyote ya shughuli za kila siku zinapaswa zifanywe katika maeneo elekezi

Ni kweli serikali inataka tufanye mazoezi.. Ila hamaanishi tusifuate utaratibu. Ili kukusanyika kwa namna yoyote ile na kundi ni kubwa tunahitaji kutoa taarifa.. Ili mamlaka zifahamu.

Lakini pia kwa hao wanakusanyiko kuna dharura.. Ajali nk ikiwa mamlaka zinajua inakuwa na uhaisi wa kupata msaada Wa dharura unapohitajia na mamlaka zinakuwa zinajua tentatively zinadeal na kundi kubwa kiasi gani

Tukirejea kwenye mazoezi ..wanasayansi wanakubaliana nami naposema kufanya mazoezi katika njia kuu za magari ni hatari kwa afya yako.. Mwili wako wakati wa mazoezi unahitaji hewa nyingi zaidi na mbaya ni kuwa hewa inayokuzunguka kwa wakati upo barabarani so hewa salama inapochangamana na moshi wa motokaa.

Kweli tunataka kuboresha afya za watanzania ila ni lazima kama serikali tuzijali pia. Tumepata taarifa itakayosaidia maboresho tunaifanyika kazi.. Maana serikali inawapenda watu wake.

Hatari zingine ni pamoja na ajali..zinazoweza kutokea wakati wa maandamano haya ya kimichezo.. Utayari wao kukabiliana na hatari hizi ..je kindi moja Liwe na ukubwa gani?! Ni baadhi ya concern tunazopaswa kuzijua ili kuepusha majanga huko mbeleni.

Kwa Kamanda wetu anayo haki ya kuwatetea watumiaji wa barabara .. Kwa kujua kwake taarifa kama ukubwa na kundi, muda utakaotumika kupitia Barabara zetu, barabara gani zitatumika.. Anapata wasaa wa kupangilia na kusimamia Magari na waenda kwa miguu hawa na wakati mwingie anaweza kuwapa alternative routes zinakazo punguza usumbufu kwa watumiaji wa magari na hawa waenda kwa miguu.

Swali lako LA viwanja naomba niseme.. Viwanja vipo viiiingi sana .. Kuna fukwe nyiiingi sana.. Karibia kila shule ya msingi inavyoviwanja.. Shule za sekondari zinavyo viwanja.. Tuanzie hapo. Kila mtu asogee shule ya msingi uliyopo karibu yake.

Lakini kama unaona huko hapakubariki basi sogea viwabja vya zakhiem, kibasila, uwanja wataifa, mchicha Kule kupita reli kama ubaenda kwa limboa vipo viwanja.. Panga gari njoo mpaka Pwani ya Aghakhan , Coco, leaders, Biafra, shule ya msingi Magomeni, mlimani na Ardhi university, viwanja vya posta kijitonyama, huko ubungo ndo mapori kila kona.. Mazoezi mfanye tu hata kwako nyumbani inawezekana.

Tukianzia huko mkuu.. Hayo maeneo tunaanza kuuona umuhimu wake yaliyoibwa tutayadai.. Na tunakoenda kuanzisha makazi mapya tutayaweka yaliyobora zaidi. Kwa mapungufu tutayaona na tutaanza kuyarekebisha.

Wasalaam
 
Afadhal ata nakumbuka walinifany nihame mtaa fulani pale mabibo,sa 11 asubuh wanapuliz vuvuzela kuamshana af mbaya zaid n karib na dirisha la chumba changu.
Ukiwakuta barabaran wanatia mbwembwe ili watu wawaangalie lkn hawana chochote kipya ujinga tu km n mazoez waende uwanjan.
 
Jogging zenyewe unafanya unavuta moshi wa magari unajaa kwenye mapafu...woooiii

Mara kumi wafanyie eneo la wazi lenye hewa safi
 
Jambo jema sana ila waangalie na haya magari ya kuzoa taka yaani ni shida kweli siku likizoa taka mchana wanafunga kabisa bara bara yaani ni shida
 
Back
Top Bottom