DAR: Polisi yakusanya zaidi ya milioni 600 ndani ya siku 8

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limekusanya kiasi cha TZS 657 milioni kutoka na faini mbalimbali za makosa ya barabarani.

Sirro alifafanua kwamba mapato hayo yamekusanywa ndani ya muda wa siku nane kati ya tarehe 5 hadi 12 mwezi January, mwaka huu, kutokana na jumla ya makosa 21,902.
 
Juzi wamenikamata mitaa ya mwandege kwenye saa tano yani ukiona copies za fomu zao za kuandikia makosa unajua hawa jamaa hawapo kazini ila wametumwa kuwakomoa wananchi. haiwezekani kwa kipindi hicho wawe wamewaadhibu wananchi kiwango hicho. ukiwaulizia receipt wanasema unafika Mkuranga ukachukue huko au uje uchukue baadae maana mhasibu yupo ofisini basi hasira zinakuchemsha maana kwa usawa huu elfu thelathini au zaidi ni kuumizana
 
sawa wamekusanya watuambie zinatumikaje ndo cha msingi ajali nyingi barabarani zinasababishwa na ubovu wa barabara muda mwingine dereva unatanua kwa kua njia mbovu . na wakati mwingine ni kosa la kuelekezwa tu wao wanapiga pesa sehemu nyingi barabara hazina alama wao ni kupokea pesa na kujisifia bila kutuambia matumizi ya hayo makusanyo
 
Kuna Mtu aliniambia akikutana na Defender la Mateja au La Polisi wa Doria Usiku basi atakimbilia kwny defender la Mateja mpaka Leo sijajua kwanini alichagua vile
 
Back
Top Bottom