Dar: Polisi waua watu wawili wakamatwa, wamekamata risasi zaidi ya 162

Wanatumia boiler plate explanation ya mtiririko ule ule kwa sababu ni waongo.

Utaanzaje kulifuatilia na kulizingira gari suspect ambalo hujaangalia namba zake? WAONGO!
Unataka namba zitajwe ili mwenye mali aingie mitini? Hiyo ni funika kombe tu..

Bawacha tatizo akili hamna..
 
Binafsi katika uzoefu wangu wa kupita pita njiani sijawahi kuona mark ii rangi ya blue tangu nizaliwe, labda hizi za matoleo mapya lakini sijaona bado, labda waliamua kubadili rangi kuwa ya blue, najau haiwezekani majambazi watumie rangi ambayo unique yaani adimu mtaani, sasa inabidi tufahamishane ni mark ii generation ya ngapi hiyo toyota walio amua kuweka rangi ya blue. Manake toyota mark ii ambazo ni maarufu ni grande ht na chaser ht.
 
Unataka namba zitajwe ili mwenye mali aingie mitini? Hiyo ni funika kombe tu..

Bawacha tatizo akili hamna..

Okay, kwa hiyo namba za gari polisi wanazo lakini wamesema hawana.

Basi niko sahihi, polisi ni WAONGO!

Eti wakitaja namba ya gari majambazi watakimbia, kwa hiyo sasa hivi majambazi wako bar wanakula bia, wakisia tu namba zao zimetajwa wanakula tunda, wanajificha. Una mashudu gani kichwani wewe mtu?

Hakuna tukio kama hilo lililotokea. Huwezi kulifuatilia gari na kulizingira bila kuangalia namba ya kibao. Otherwise walilishuku gari kwa kuangalia nini, rangi ya body au walisoma VIN namba kwenye engine?

Polisi ni waongo na wanajua kwamba wako suspect hawaaminiki ndio maana kila la ukweli linalotokea huwa wanajaribu kwa udi na uvumba kuonyesha evidence. Leo Kamanda Mambosasa ameonyesha sefu ya hela iliyoibiwa Prime Attorneys na majina kamili ya majambazi. Ukiona hawana evidence, hawana jina, hawana chochote, ujue UONGO!

Tumeli trace jambazi sugu, tumelipiga risasi ya magoti, likakubali makosa, likataja wenzie, likasema lenyewe ndio mastermind wao wote, Kibiti, CRDB, Stakishari, Mwanza, lilipomaliza tu kusema likavuja damu nyingi, lika drop dead, njia panda Muhimbili. Jina Ukwaju! Unamuuzia nani hadithi kama hiyo?
 
Hao waliowakamata Dar utaja sikia kuwa ndiyo waliohusika na jaribio la kutaka kumwua Tundu Lissu kule Dodoma!

Aisee hawa Polisi wetu imekuwa shidaaa.....
kweli unaweza kuskia eti jambazi flani lililofariki tumebaini ndiye aliyemtupia lissu risasi. tunaendelea kubaini wengine... askari mnatupa mizuka ipo siku ya...
 
Kazi ya upelelezi ngumu sana au maelezo yamepungua? Wahalifu walikua kwenye gari, wakasimamishwa wakaanza kurushiana risasi, baadhi wakajeruhiwa na wamefariki wakiwa njiani kupelekwa kwenye matibabu.

Mnalifuatilia gari lenye wahalifu baada ya kutonywa na wasamaria wema, mnalizingira na kuanza kufyatuliana risasi. Baadae mmoja anatoroka na hilo gari

Namba za gari hazijajulikana....
Walisimamishwa ina maana walishuka?
Kama hawakushuka iweje mwingine afanikiwe kukumbia bila wenzio?
September 19, 2017 Mariam Mallya

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwaua Majambazi watatu na kuwakamata wengine wawili huko Vingunguti-Becco katika Mkoa wa kiporisi Ilala.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP L.B Mambosasa alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo.

Kamishina Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua na kuwakamata majambazi hao kutokana na taarifa zilizotolewa na wasamalia wema juu ya uhalifu uliopangwa kufanyika kwenyw moja ya maghara eneo la Tazara.

Katika taarifa yake, Kamishina Mambosasa amesema kuwa mnamo saa kumi na moja na dakika ishirini jioni Polisi walifanikiwa kuweka mtego na kulisimamisha gari aina ya Toyota Mark II lenye rangi ya bluu (namba zake hazikufahamika). Baada ya Majambazi kugundua kuwa waliosimamisha gari walikua Askari, majambazi hao walianza kuwashambulia askari kwa risasi hivyo askari kujibu mapigo na kuwajeruhi majambazi watatu.

Aidha, taarifa inasema kuwa majambazi hao wamegundulika kuwa ni wahalifu Sugu waliokwisha fanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika jiji la Dar es salaam. Mmoja amejulika kwa jina moja la SHAFI, huyu alikua akitumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa unyang’anyi wa kutumia silaha, wa pili ni Babu Jaffari ambae pia ameshiriki matukio mbalimbali kwa kutumia silaha na wa tatu ni Mbegu Maloni ambae ndie mtafutaji wa kazi za kwenda kupora (MasterPlan) likiwemo tukio hilo la Tazara.

Katika eneo hilo la tukio kumekutwa Bastora moja aina ya Browning, Risasi tatu ambapo moja ilikuwa chemba tayari kwa kufyatuka, maganda matatu ya Risasi zilizofyatuliwa kutoka katika Bastora ya Majambazi. Majambazi hao walifariki wakati wakipelekwa Hospital ya Muhimbili kwa matibabu baada ya kuvuja damu nyingi. Hata hivyo msako mkali unaendelea kumsaka jambazi alietoroka na gari hilo lililotumiwa na majambazi hao.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM katika tarehe ya 16.09.2017, majira ya saa kumi na moja na dk hamsini jioni huko Makaburi ya Wangazija, Upanga limewakamata Rahma Almas@Baby miaka 37, mkazi wa Temeke Mkuranga B, Mohamed Maganga miaka 61, mkazi wa Pugu ambae pia ni Mlinzi na mfanya usafi katika makaburi hayo. Watuhumiwa hawa wamekamatwa wakiwa na Bunduki mbili aina ya UZIGUN na RIFFLE, Bomu la kurusha kwa mkono, risasi 162 za silaha aina ya Uzigun na risasi tano za Riffle.

Baada ya mahojiano mtuhumiwa Rahma Almas@Baby alikiri kuhifadhi silaha hizo zilizotumika ktk matukio mbalimbali a kihalifu ikiwemo mauaji ya WAYNE DERRICK LOTTER Mkurugenzi wa Palm Conservation Foundation, miaka 52 raia wa Afrika kusini alieuawa mwezi uliopita Masaki akitokea airport ya JNIA.

Katika tukio jingine Polisi Kanda maalum ya DSM wamewakamata watuhumiwa watano wa uvunjaji wa Ofisi ya Mawakili ya Prime attorneys iliyovunjwa tarehe 12.09.2017 na kuibiwa kasiki iliyokuwa na pesa Tsh.3,700,000/=, Laptop mbili na nyaraka mbalimbali za ofisi na za wateja. Prime attorneys ndio waliokuwa watetezi wa Yussuph Manji wakati wa kesi iliyokuwa ikimkabiro ya uhujumu Uchumi ambayo pia imefutwa tayari.

Watuhumiwa hao waliokamatwa sehem mbalimbali za Jiji la DSM baada ya msako mkali ni:-
1. Said Idrisa Salehe (47), mkazi wa Mbezi Luis.
2. Mustapha Ibrahim Said (35) mkazi wa Magomeni Mwembechai.
3. Somfi Uliza Somfi (52) mkazi wa Mahomeni Mapipa.
4. Iman Mbago Mhina (36) mkazi wa Kimara Mwisho.
5. Hussein Haji Suleiman (45) Mkazi wa Kigogo Mbuyuni.
Baada ya mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuhusika na tukio hilo na kuonesha kasiki la fedha pamoja na mitungi mitatu ya gesi iliyotumika kukatia kasiki hilo. Upelelezi unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wengine walioshiriki tukio hilo.

Kamishina Mambosasa katika taarifa yake amesema kuwa Polisi Kanda maalum ya DSM kupitia kikosi chake cha usalama barabarani wameendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 15.09.2017 hadi tarehe 18.09.2017 kama ifuatavyo:-

Jumla ya Magari yaliyokamatwa 13,784
1. Pikipiki zilizokamatwa 392
2. Daladala zilizokamatwa 5,387
3. Magari mwngine binafsi na malori 8,397
4. Bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa kutovaa Helmet na kupakia abiria mishikaki 22.
Jumla ya makosa yote yaliyokamatwa ni 14,176.
Pesa za tozo zilizopatikana ni Tsh. 424,620,000/=
 
Huyo akiyekua akitumikia miaka 30 jela alitokaje akaja kufanya tukio?
 
Back
Top Bottom