Dar: Polisi waua watu watatu wanaodhaniwa kuwa Majambazi, wakamata silaha

Ninashaka na ufikiri wako, sorry lakini.mtu anakurushia risasi unamkamataje labda?.kwenye matukio yote hayo mbona yako wazi hao ni majambazi.ongea tu ila omba kama unakibiashara chako kimekuwa wakakuvamia.
Hongera jeshi la polisi kanda maalum Dar
Wote wanazisikia kwenye Filamu tu.wasamehe
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
hujakutana bado na hekaheka za majambazi wewe! hawanaga huruma wakikukuta wanakufagia unazikwa! We weka Mpesa yako ukonga iwe hata na milion 1 halafu waje! ndio utajua kumbe jogoo jina tu
 
Kwani una hakika wote ni majambazi?
Polisi yetu Hii ya kubambikizia watu kesi
Unajuaje hivyo wanavyosema wamewakuta navyo vimewekwa kujustify zoezi zima
MM nipo pamoja na wewe ,maana nakumbuka kesi ya ujambazi wa madini lakini mwisho wa siku kuna kiongozi alikutwa na kesi ya kujibu na yupo ndani

Nashindwa kuelewa yaani tayari mtu mnaye mkononi na anawapeleka mpaka kwenye tukio la ujambazi then anauliwa?Ni wapi ujuzi na waledi wa polisi mpaka inafikia hapa kwa kutekeleza mauaji haya
Ni kweli jambazi ni mtu hatari sana lakini wakamatwe na kupelekwa mahakamani wahukumiwe kwa mujibu wa sheria siyo kuua .
kumbuka Abdala Zombe
 
Niwapongeze sana jeshi la polisi kwa awamu ya tano ukweli wanafanya kazi na watu siku hizi tunalala usiku jamani. Hatutakaa tumsahau Omari Mahita mzee wa kujengewa nyumba na vitega uchumi. Pia na Abdalah Zombe. Mbele za Maulana mtajibu.
 
Yaani akikamatwa Jambazi ninaomba apigwe cha moto na kufa tu maana wakipelekwa mahakamani majambazi wenzao wanajichanga wanahonga wanaachiwa. Hawa watu wako na mtandao wao na wanasaidiana sana. Hivyo ili kuwapunguzia nguvu ni kuwapunguza kwa Shaba tu. Yaani akishaungama dhambi na kuwataja wengine wakikamatwa ni lazima amalizwe tu. Hakuna kuremba na jambazi ambalo akikuvamia ni kufa au kubaki na ulemavu. Futilia mbali hawa criminals.
 
Una mkataje mtu anakurushia risasi Mkuu? Ile kitu sio mchezo. Ukijichanganya umekwenda na jambazi anaendelea kula bata mtaani,ikitokea mazingira ya hivyo atakae muwahi mwenzie ndio anapona.
Hii kitu mimi nimesha wahi kuiexpirience majambazi walikua wanavamia nyumba moja hivi pale pugu selemala polisi wakafika unaambiwa ishu ilikua kama muvi yaani piga nikupige.

Sema mtu ambae hajawahi kushuhudia tukio kama hili anaweza kuchukulia poa.

Watu tulikua ndani ya nyumba lakini hizo risasi zinavyo lia watu mnajificha uvunguni unahisi inaweza toboa ukuta.

Harafu wakati huo huo we unaogopa askari wapo uso kwa uso na majambazi utafikiri wanacheza basket ball.

Mambo mengine ni zaidi ya ushujaa polisi wapewe hongera zao.

Mimi mwenyewe nilikuaga naskia tu polisi wamepambana na majambazi arafu nachukulia poa.

Ila siku ile ndo nilijua polisi wanajiweka rehani kwa usalama wetu kiasi gani.

Asubuhi tukasikia wameua majambazi watatu,kuna nyumba walikua wanaenda kuvamia;hii kitu isikie tu.

Polisi wapewe hongera zao maana siku ile ya tukio mtaa mzima ulikua kimyaa watu tumejifungia majumbani kwetu hakuna mwanaume au mwanamke aliyetoka kusaidia polisi,yaani pale mtaani kuna wanajeshi kibao wanakaa kule ila wote walikaa kimyaaa.

polisi peke yao huko nje walikua wanapambana yani risasi ikipigwa kama imepigwa mlangoni aisee ilikua balaaaaaaaaa.Polisi wanaume aisee asikwambie mtu.

Asubuhi tukasikia majambazi watatu wameuawa.Kongole kwa polisi aisee.
 
Askari walijibu mapigo na walifanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu OMARI ATHUMANI, FULLSABA NA BABU SHOBO sehemu mbalimbali za miili yao na mmoja aitwaye DOGO SIDE alifanikiwa kukimbia kusikojulikana, majeruhi wote walikimbizwa hospitali ya taifa Mhimbili kwa matibabu lakini baada ya Daktari kuwapima alithibitisha kuwa wameshafariki dunia.
Alafu anakamatwa ELIA MATAYO wakati aliyetoroka Siku ya tukio walimtambua Kwa jina la DOGO SIDE.
 
K
Askari walijibu mapigo na walifanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu OMARI ATHUMANI, FULLSABA NA BABU SHOBO sehemu mbalimbali za miili yao na mmoja aitwaye DOGO SIDE alifanikiwa kukimbia kusikojulikana, majeruhi wote walikimbizwa hospitali ya taifa Mhimbili kwa matibabu lakini baada ya Daktari kuwapima alithibitisha kuwa wameshafariki dunia.
Kweli kabisa. Anayeweza kuthibitisha kwamba mtu aliyeletwa hospitalini amekwisha kufa ni daktari tu. Hivyo mgonjwa hata kama keshakufa, bado atakuwa anaishi hadi hapo Daktari atakapothibitisha tena kwa maandishi kwamba "dead on arrival" (DOA) yaani huyo mgonjwa alifikishwa hapo hospitalini akiwa tayari mfu.
 
Tena hadi majambazi wengine "wanaugua ghafla na kufariki" kwa maradhi yaliyokua yanawasumbua
Huo pia ni ukweli. Katika mikikimikiki ya mapambano majambazi huugua maradhi ambayo kwa kawaida huwa yamejificha. Na hivyo wakipelekwa hospitalini madaktari huthibitisha kwamba tayari wamekwisha kufa.
 
MM nipo pamoja na wewe ,maana nakumbuka kesi ya ujambazi wa madini lakini mwisho wa siku kuna kiongozi alikutwa na kesi ya kujibu na yupo ndani

Nashindwa kuelewa yaani tayari mtu mnaye mkononi na anawapeleka mpaka kwenye tukio la ujambazi then anauliwa?Ni wapi ujuzi na waledi wa polisi mpaka inafikia hapa kwa kutekeleza mauaji haya
Ni kweli jambazi ni mtu hatari sana lakini wakamatwe na kupelekwa mahakamani wahukumiwe kwa mujibu wa sheria siyo kuua .
kumbuka Abdala Zombe
Umewahi kukaa ndani walau kwa siku moja??ukisikia walioyafanya hawa unaowatetea na wanavyoendelea ku influence watu huko ndani utabadili mawazo.Sio kila anaeuawa leo kapatikana leo!(sijui hata kama kauli itaeleweka)
 
story ya kwanza nimeipenda polisi walikuwa na jambazi omary wakaenda nae mpaka kwenye maeneo ya matukio pugu shuleni walipoweka mtego washirika wake walijitokeza toka kwenye vichaka walipojua kuna maaskari wakaanza kurusha risasi. eti mtuhumiwa alipiga kelele na kuwakimbia askari. swali huyu omary ni jambazi mmemkamata kwa nini hamkumuwekea ulinzi na hata hamkumfunga pingu?? na mbona mara nyingi eti majambazi huwanza kuwarushia risasi askari na haohao askari hawapati madhara huwa wapo salama
kila siku lazima usikie majambazi walijitokeza kichakani na kuanza kuwarushia risasi polisi alf majambazi wanakufa wakipelekwa hosp duh!

hao majambazi ina maana hawakujua kama mwenzao kakamatwa huo mpango wao wa kwenda kuvamia uhairishwe?

kuna kitu hakipo sawa ukisoma vzuri kama movie vile
 
Back
Top Bottom