Dar: Polisi waua watu watatu wanaodhaniwa kuwa Majambazi, wakamata silaha

Askari walijibu mapigo na walifanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu OMARI ATHUMANI, FULLSABA NA BABU SHOBO sehemu mbalimbali za miili yao na mmoja aitwaye DOGO SIDE alifanikiwa kukimbia kusikojulikana, majeruhi wote walikimbizwa hospitali ya taifa Mhimbili kwa matibabu lakini baada ya Daktari kuwapima alithibitisha kuwa wameshafariki dunia.
mzee tafakari yako inaukakasi, ila usijali ndivyo ilivyo hahahahaha wahenga tumekuelewa
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
Waharifu huwa hawakubali kukamatwa, wanafyatua risasi kwa polisi. Polisi akizubaa tu anauawa yeye then mharifu anakimbia. Ndio hivyo polisi wakiona jambazi halitaki kujisalimisha, wanawahi kumlamba shaba.

Unaona wengine wakifungwa, wanaachiwa wanarudi tena kufanya uharifu kama ilivyoelezwa hapo.
 
hongera jeshi la polisi,majambazi sio wa kuwavumilia hata kidogo
uwa na penda sana zile movie za kuwapeleka porini kuonyesha silaha ,kinachofuata ni kukimbia na kujibizana risasi na hamjawai kukosea hata kidogo
good job
 
Kama mimi ndiye DOGO SIDE, hakika ningemrudia Mungu wangu mara moja na kuachana kabisa na huo ujambazi au hata kuhusishwa nao tu! maana hizi filamu za polisi wa awamu hii ni za kutisha kweli kweli, hasa unapofika lile eneo la tukio kuwaonesha hizo silaha au wenzako unaoshirikiana nao.
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
Acha ujinga wewe , umeshaambiwa hapo watu wanakamatwa wanatoka kwa rufaa halafu wanaiba tena wengine wanaua kabisa raia .. dawa yao ni kuuawa pia .. acha kuleta siasa.
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
Una mkataje mtu anakurushia risasi Mkuu? Ile kitu sio mchezo. Ukijichanganya umekwenda na jambazi anaendelea kula bata mtaani,ikitokea mazingira ya hivyo atakae muwahi mwenzie ndio anapona.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
POLISI YAZUIA TUKIO LA UJAMBAZI
KUKAMATWA SILAHA MBILI AINA YA SHORTGUN, BASTOLA PAMOJA NA KUUWAWA MAJAMBAZI WATATU (3)

Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam mnamo tarehe 25/08/2019 majira ya tatu na nusu usiku huko maeneo ya Pugu, lilifanikiwa kukamata silaha mbili aina ya Shortgun na bastola.

Katika ufuatiliaji alikamatwa mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la OMARY ATHUMANI @ DANGA MIAKA (39), mkazi wa mkuranga amabaye pia alikuwa anatafutwa kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha, katika mahojiano ya kina mtuhumiwa alikiri kujihusisha na matukio mbalimba ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kuwa amewahi kufungwa miaka 30 na alitoka kwa rufaa na kujiunga na kundi lingine la ujambazi.

Mtuhumiwa huyo pia alieleza kuwa kuna wenzake watatu ambao anashirikiana nao pia wamepanga wakavamie na kupora duka la M-pesa lililopo maeneo ya Pugu shuleni hivyo yuko tayari kuwapeleka Askari eneo la tukio, kikosi kazi wakiwa na mtuhumiwa waliweka mtego na ilipofika muda huo eneo la Pugu washirika wake walijitokeza toka kwenye kichaka wanakoficha silaha mara wakagundua kuwa wanafuatiliwa na askari maeneo hayo ghafla majambazi hao walianza kurusha risasi kuelekea kwa Askari na mtuhumiwa alianza kupiga kelele na kujaribu kuwakimbia askari.

Askari walijibu mapigo na walifanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu OMARI ATHUMANI, FULLSABA NA BABU SHOBO sehemu mbalimbali za miili yao na mmoja aitwaye DOGO SIDE alifanikiwa kukimbia kusikojulikana, majeruhi wote walikimbizwa hospitali ya taifa Mhimbili kwa matibabu lakini baada ya Daktari kuwapima alithibitisha kuwa wameshafariki dunia.

Baada ya upekuzi majambazi hao walipatikana na silaha mbili No. YA- 1547 aina ya SHORTGUN iliyo katwa kitako na mtutu, Ikiwa na risasi tatu, ganda moja la risasi na BASTOLA moja iliyo futwa namba ikiwa na risasi mbili na maganda mawili(2) ya risasi.

Aidha silaha tajwa aina ya Shortgun ilibainika kuwa iliporwa tarehe 13.04/2019 saa nne na nusu usiku kesi ya unyang’anyi ilifunguliwa kituo cha Ukonga na silaha hiyo ilikuwa mali ya kampuni ya ulinzi iitwayo ALEMS SECURITY CO.LTD iliyopo njia panda Segerea Dsm na ilitumika kupora kiasi cha pesa Tsh 6,000,000/= huko MARKAZ Gongo la mboto kwa mfanyabiashara aitwaye JUSTINE CHAULA, pamoja na simu 5 za aina mbalimbali.

Awali mtuhumiwa alikiri kuwa yeye na wenzake wamewahi kushtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha zaidi ya kesi 6 ambazo zilikuwa mahakamani kabla ya kutoka kwa rufaa mwaka 2017.

Tukio lingine mwezi wa 6, 2019 walipora maduka ya M-pesa, Tigo pesa maeneo ya mazizini Ukonga, mbezi juu wilaya ya ubungo na walipora Tsh 800,000/= kwa mfanyabiashara wa mchanga, maeneo ya Machimbo wilaya ya Mkuranga. Pia polisi wilaya ya mkuranga ilifanya upekuzi nyumbani kwa marehemu OMARY ATHUMAN@DANGA na kufanikiwa kukamata risasi 7 za silaha aina ya Shorgun na jalada la shauri hili linapelelezwa.

Kikosi kazi kinaendelea na msako mkali ili kuhakikisha jambazi aliyetoroka kwenye eneo la tukio anakamatwa haraka na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Wananchi wazidi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuliweka jiji letu la Dar es salaam katika hali ya amani na utulivu ili raia wema waendelee kufanya kazi za kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla.

KUKAMATWA KWA JAMBAZI MMOJA, ALIYEKIMBIA KWENYE TUKIO LA UJAMBAZI, KUPATIKANA SILAHA MOJA, RISASI TATU NA VIFAA MBALIMBALI
Katika tukio la pili, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kumkamata jambazi mmoja aitwaye ELIA MATAYO KITULI (55) mkazi wa Kivule, wilaya ya Ilala jijini DSM aliyekuwa anatafutwa, Baada ya kukimbia kwenye tukio la ujambazi lililotokea tarehe 04/07/2019 ambapo majambazi wawili waliuwawa na kupatikana silaha mbili aina ya bastola huko Kitunda machimbo ambapo nilitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Jambazi huyo alikamatwa akiwa na silaha moja aina ya Rifle yenye namba MK3-90893 ikiwa na risasi 3 ndani ya kasha(magazine) na vifaa mbalimbali vilivyoporwa maeneo mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Ipad mbili aina ya Samsung na Apple
2. Smart phone nane(8) aina ya INFINX, Samsung, Nokia, Huawei, Techno na Iphone.

3. Saa moja ya mkononi aina ya Seiko 5 rangi ya dhahabu
4. Kisu kimoja
5. Digital camera moja aina ya Sony
6. Lap top moja aina ya Toshiba
7. Head phone moja na charger mbalimbali za simu

Mtuhumiwa aliendelea kuhojiwa kituo cha Polisi mara aliugua ghafla na kupelekwa hospitali ya taifa Muhimbili na baadaye alifariki dunia kwa maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Baadhi ya wahanga waliofanyiwa matukio ya uporaji wamefanikiwa kutambua vifaa vyao ambapo simu 2 aina ya Iphone na Samsung moja zilitambuliwa.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
29/08/2019
Silaha wanapandikiza baada ya kuua, hawa jamaa PEPO WAISAHAU
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
Siku ikikutokea kwako ndo utajua,ila kwa waliokwisha ibiwa Something is right
 
story ya kwanza nimeipenda polisi walikuwa na jambazi omary wakaenda nae mpaka kwenye maeneo ya matukio pugu shuleni walipoweka mtego washirika wake walijitokeza toka kwenye vichaka walipojua kuna maaskari wakaanza kurusha risasi. eti mtuhumiwa alipiga kelele na kuwakimbia askari. swali huyu omary ni jambazi mmemkamata kwa nini hamkumuwekea ulinzi na hata hamkumfunga pingu?? na mbona mara nyingi eti majambazi huwanza kuwarushia risasi askari na haohao askari hawapati madhara huwa wapo salama
 
Wauwawe wakufe wote...yani once you smell harufu ya jambazi Dawa ni kuuliwa tu.

Mnaotetea hamjakumbwa na kadhia ya kuwindwa NA majambazi.

Nimeshawahi lala DUKANI ndani one week nawindwa nitoke niwahishwe kwa baba..

Nikiskia majambazi yameuwawa DAR napumua eti
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
Sidhani kama unaweza kumkamata mtu anayekutupia risasi za moto,zaidi ya wewe kujibu ili usalimishe maisha yako Na katika hali kama hiyo sijui kama utaweza kchagua wapi pa kupiga.Huo huwa ni wakati mgumu sana kwa Polisi...
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
ndugu yangu sio kama napinga ila hebu rudia tu kusoma hapo juu wengine walishapelekwa mahakamani na wakatoka wanavyojua wao na wakaja kudhuru tena jamii yetu siungi mkono lakini some how iko sawa naamini ipo siku yakikukuta ya hawa mabwana vya bure utakua wa kwanza kushadadia walazwe haraka haraka sikia tu jambazi kavamia
 
Hivi hamkumbuki Mkuu aliwaambia Polisi pale Biafra kwamba majambazi wawanyang'anye silaha harakaharaka? Jambazi sio mtu wa kucheza nae, dakika sifuri anakutangulizi wewe. Ndio maana polisi hawafanyi 'betting' na hao jamaa wakipata chansi wanatandika tu risasi
 
Stori za majambazi
Eti akatupeleka porini
Wenzake wakaanza rusha risasi
Mtuhumiwa akaanza piga kelele na kuwakimbia polisi
Wakapelekwa Muhimbili


Wanaua watu afu stori zao kila siku ni hizi hizi.

Huyo Athuman aliuawa Polisi waliwajuaje hao wengine majina yao?
Mambo mengine ni ya kiusalama.
Akili yako ndogo sana kuyajua.
We tulia kula ugali askari wapambane kivyao. Mengine hayakuhusu.

Siku majambazi wakiua ndugu yako na kumpora ndo utauliza vzri.
 
story ya kwanza nimeipenda polisi walikuwa na jambazi omary wakaenda nae mpaka kwenye maeneo ya matukio pugu shuleni walipoweka mtego washirika wake walijitokeza toka kwenye vichaka walipojua kuna maaskari wakaanza kurusha risasi. eti mtuhumiwa alipiga kelele na kuwakimbia askari. swali huyu omary ni jambazi mmemkamata kwa nini hamkumuwekea ulinzi na hata hamkumfunga pingu?? na mbona mara nyingi eti majambazi huwanza kuwarushia risasi askari na haohao askari hawapati madhara huwa wapo salama
Kwa hiyo unataka mpaka askari wajeruhiwe ndo waonekane wanafanya kazi?
Jinga kabisa ww
 
Kwa nini Polisi wanaua kila anayedhaniwa jambazi Kwa nini hawawakamati kuwapeleka mahakamani
Something is not right somewhere
Ninashaka na ufikiri wako, sorry lakini.mtu anakurushia risasi unamkamataje labda?.kwenye matukio yote hayo mbona yako wazi hao ni majambazi.ongea tu ila omba kama unakibiashara chako kimekuwa wakakuvamia.
Hongera jeshi la polisi kanda maalum Dar
 
Kwani una hakika wote ni majambazi?
Polisi yetu Hii ya kubambikizia watu kesi
Unajuaje hivyo wanavyosema wamewakuta navyo vimewekwa kujustify zoezi zima
Jamii yetu imekua na wajuaji wengi sana.
Hivi unajua kuna “wahalifu wa akiba”??
Hivi unajua asilimia kubwa ya wanaokamatwa kwenye Haya matukio ni matokeo ya taarifa zilizopatikana muda sana kwenye matukio mengine ya nyuma??sio kua mtu anadakwa hapo hapo tu.
Kuna uwezekano Polisi wakakosea ila sio kwa kiwango mnachiwafikiria.Ukipambana na majambazom siku moja utaelewa kwanini ni muhimu mno “KUWANYANG’ANYA SILAHA HARAKAHARAKA”
 
Back
Top Bottom