Dar: Polisi waua watu saba wanaodaiwa ni Majambazi eneo la Mwenge

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Leo Kamanda wa Polisi Kanda maaalum ya DSM SACP Lazaro Mambosasa atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Polisi central kuanzia saa saba Kamili.

Nitawaletea Update:

Karibuni sana.


======

UPDATES. 1302hrs

Kuuawa kwa majambazi saba na kupatikana na Silaha moja bastola yenye risasi tatu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUUAWA KWA MAJAMBAZI SABA NA KUPATIKANA NA SILAHA NDOGO BASTOLA AINA YA BERETA IKIWA NA RISASI TATU NDANI YA KASHA (MAGAZINE)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola aina ya BERETA ikiwa na risasi tatu ndani ya kasha (magazine) na silaha za jadi.

Mnamo tarehe 25.05.2020 majira ya saa sita na dakika kumi usiku huko maeneo ya Mwenge Coca Cola majambazi saba wakiwa kwenye gari namba T 956 BYA Toyota Noah Rangi ya fedha (Silver) wakielekea kufanya uhalifu katika ghala la GS Group Limited linalohifadhi vifaa vya pikipiki, kabla hawajafanikiwa kufanya uhalifu huo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na ujambazi lilipata taarifa kutoka kwa msiri na kufika mara moja eneo la Mwenge Cocacola na kulibaini gari hilo, ambapo kikosi kazi hicho kilipojaribu kulifuata gari hilo la majambazi liliongeza mwendo na kuchepuka barabara ya vumbi na ghafla majambazi hao walianza kulishambulia gari la Polisi kwa risasi na ndipo askari wakajibu mapigo na kufanikiwa kupiga tairi gari la majambazi hao, majambazi hao wakashuka na kuanza kukimbia huku wakirusha risasi ovyo lakini askari Polisi kwa umahiri wa hali ya juu walifanikiwa kuwajeruhi majambazi wote saba na kufanikiwa kuwakamata wote.

Aidha katika upekuzi wa awali ndani ya gari la majambazi hao kuilikutwa na mitungi miwili ya gesi na mipira yake, Mapanga matatu, Kamba za katani (kudu) na baada ya kumpekua jambazi mmoja alikutwa na silaha ndogo Bastola aina ya BERETA ikiwa na risasi tatu ndani ya kasha (Magazine).
Majambazi wote saba walikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na walipofikishwa hospitalini hapo daktari alithibitisha kuwa wameshafariki dunia na miili yao imehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi.

TATHIMINI YA HALI YA USALAMA KATIKA KUISHEREKEA SIKUKUU YA EID EL-FITRI JIJI DAR ES SALAAM.

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limefanikiwa kuimarisha usalama kipindi chote cha kusherekea sikukuu ya Eid-El-Fitri Jijini DSM na kwamba hakuna tukio lolote la uhalifu lililoripotiwa au ajali mbaya ya barabarani iliyoripotiwa.

Sikukuu hiyo ya Eid-El-Fitri iliyosherekewa Tarehe 24.05.2020 na kuendelea tarehe 25.05.2020.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM limejipanga kikamilifu kuhakikisha inasherekewa kwa amani na utulivu maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam na linawataka wananchi kuendelee kufuata sheria za Nchi ili kumalizia kusherekea sikukuu hii kwa amani na utulivu.

Imetolewa na
Kamanda wa Polisi,
Kanda Maalum ya Dar es Salaam,

SACP-Lazaro Mambosasa,
25/05/2020

IMG_20200525_132113_781.jpg
IMG_20200525_131211_128.jpg
 
update (aya ya kwanza): kuuawa kwa majambazi saba
updta (aya ya pili kutoka mwisho): majambazi wote saba walijeruhiwa.

tuweke sawa hapo tafadhali.
 
Leo kamanda wa Polisi Kanda maaalum ya DSM SACP Lazaro Mambosasa atakua na mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Polisi central kuanzia saa saba Kamili.

Nitawaletea Update:

Karibuni sana.


======

UPDATES. 1302hrs

Kuuawa kwa majambazi saba na kupatikana na Silaha moja bastol yemye risasi tatu.

Majmbazi hayo yameuawa 25 Mei 2020 majira ya saa sita usiku Maenel ya Mwenge Cocacola, Majambazi 7 wakiwa kwenye Noah wakielekea kufanya iharifu kwenye ghara la GS Limited

Askari walipata taarifa kutoka kwa msiri. Walifuatilia gari hilo kulingana na taarifa.

Majambazi baada ya kuona wanafuatiliwa na wapelelezi wa kanda waliongeza mwendo. Gari ya polisi iliongeza mwendo pia.

Walikuwa wamejihami na wakaanza kufyatua risasi. Polisi wakajibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wote saba.

Wakakamatwa na kukutwa na mitungi miwili ya gesi ya kuvunjia Milango.

Walipofikishwa Hospital Daktari akasema wamekata roho.

Mambosasa amewataka kila mmoja kufuata sheria ya nchi.

Hali ya jiji la Dar ipo Vizuri, na watu wapo huru kutembea popote hadi kwenye fukwe.

Nawapongeza wananchi wanaoishi kwa kufuata sheria. Nawashukuru wote wanaotoa habari za Uharifu.

Hivi juzi pale Tegeta kuna Mama alipigwa risasi na hawa wahuni.

Kuhusu Mchekeshaji Idris hayupo Kanda maalumu ya Dar Es Salaam, Mujlizeni DCI kwa afande Misime ndiye anaweza kuliongelea.
View attachment 1459171View attachment 1459172
Asanteni sana POLISI kwa kazi nzuri, kwanza mnafanya kazi ya hatari sana, you will always be our hero!
Tunawapenda sana, hatuna cha kuwalipa isipokuwa Mungu awajalie zaidi na zaidi, ninyi na familia zenu
 
Mimi Nina wasiwasi na Jeshi la polisi,hili tamko haliko sawa.

1.Majambazi saba wana bastola Moja na wote wameuawa,katika saba hakuna aliyetaka kujisalimisha?unauaje wote saba bila kubakiza hata mmoja kusaidia upelelezi au kujua chanzo cha uhalifu?

2.Wakijeruhiwa wote,na wote kufika hospital wakafa?

Hii haijakaa sawa,labda ingekuwa inawezekana kusikia na watu Wa karibu na hawa majambazi tungejua ukweli tofauti na hivyo bado sijalielewa Jeshi la polisi na majambazi kuuawa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Nina wasiwasi na Jeshi la polisi,hili tamko haliko sawa.

1.Majambazi saba wana bastola Moja na wote wameuawa,katika saba hakuna aliyetaka kujisalimisha?unauaje wote saba bila kubakiza hata mmoja kusaidia upelelezi au kujua chanzo cha uhalifu?

2.Wakijeruhiwa wote,na wote kufika hospital wakafa?

Hii haijakaa sawa,labda ingekuwa inawezekana kusikia na watu Wa karibu na hawa majambazi tungejua ukweli tofauti na hivyo bado sijalielewa Jeshi la polisi na majambazi kuuawa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jambazi ni wa kuua kabisa, waliowahi kuvamiwa, kujeruhiwa, kuibiwa mali zao, kupoteza viungo vya mwili au kupoteza wapendwa wao wanaelewa watanielewa kabisa! Jambazi hana huruma hivyo hapaswi kuhurumiwa wala kuachwa aishi

Sent using kidole gumba
 
Leo Kamanda wa Polisi Kanda maaalum ya DSM SACP Lazaro Mambosasa atakua na mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Polisi central kuanzia saa saba Kamili.

Nitawaletea Update:

Karibuni sana.


======

UPDATES. 1302hrs

Kuuawa kwa majambazi saba na kupatikana na Silaha moja bastol yemye risasi tatu.

Majambazi hayo yameuawa 25 Mei 2020 majira ya saa sita usiku Maenel ya Mwenge Cocacola, Majambazi 7 wakiwa kwenye Noah wakielekea kufanya iharifu kwenye ghara la GS Limited

Askari walipata taarifa kutoka kwa msiri. Walilifuatilia gari hilo kulingana na taarifa.

Majambazi baada ya kuona wanafuatiliwa na wapelelezi wa kanda waliongeza mwendo. Gari la Polisi iliongeza mwendo pia.

Walikuwa wamejihami na wakaanza kufyatua risasi. Polisi wakajibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wote saba.

Wakakamatwa na kukutwa na mitungi miwili ya gesi ya kuvunjia Milango.

Walipofikishwa Hospitali, Daktari akasema wamekata roho.

Afande Mambosasa amewataka watanzania kila mmoja kufuata sheria ya nchi.

Hali ya Usalama

Hali ya jiji la Dar ipo Vizuri, na watu wapo huru kutembea popote hadi kwenye fukwe.

Nawapongeza wananchi wanaoishi kwa kufuata sheria. Nawashukuru wote wanaotoa habari za Uhalifu.

Hivi juzi pale Tegeta kuna Mama alipigwa risasi na hawa wahuni.

Kuhusu Mchekeshaji Idris hayupo Kanda maalumu ya Dar Es Salaam, muulizeni DCI kwa afande Misime ndiye anaweza kuliongelea.

View attachment 1459171View attachment 1459172
Sina imani na jeshi letu.Wakikupimia una ela wanakubadilisha jina fasta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asanteni sana POLISI kwa kazi nzuri, kwanza mnafanya kazi ya hatari sana, you will always be our hero!
Tunawapenda sana, hatuna cha kuwalipa isipokuwa Mungu awajalie zaidi na zaidi, ninyi na familia zenu
Safi sana umejitahidi si unaona siku hizi nawewe unajua ung'eng'e.
 
Back
Top Bottom