Dar: Polisi wapiga marufuku disko toto katika kumbi za starehe Sikukuu ya Eid El Fitr

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameeleza namna polisi walijipanga kuimarisha ulinzi sikukuu ya Eid el Fitri.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 12, 2021 Kamanda Mambosasa amesema wamepiga marufuku disko toto katika kumbi za starehe sambamba na kuimarisha usalama.

Sikukuu ya Eid inatarajiwa kuwa kesho na keshokutwa kulingana na mwandamo wa mwezi.

“Tunawaasa wananchi wa Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria. Polisi imejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada, fukwe na kumbi za starehe.”

“Pia tutaimarisha ulinzi katika maeneo mengine yote yatakayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu,” amesema Mambosasa.

Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao hawatembei peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu na wasiwaruhusu kuogelea peke yao, akisema hatua hiyo itazuia vifo vya vinavyotoka na watu kuzama kwenye maji.

Katika hatua nyingine, Mambosasa amesema polisi imefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi katika maeneo ya Mbagala karibu na ukumbi wa Dar Live baada ya kurushiana risasi na polisi.

Amesema kuwa majambazi hao wakiwa na pikipiki walijiandaa kufanya uhalifu katika maduka na vibanda vya miamala ya fedha lakini kabla hawajatimiza azma yao ya polisi kupitia kikosi maalumu kilithibiti hali hiyo.

“Wakiwa kwenye pikipiki walipewa amri ya kusimama lakini walikaidi na kuanza kuwarushia askari risasi. Askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao na kufariki dunia papo hapo,” amesema Mambosasa.


Chanzo: Mwananchi
 
“Wakiwa kwenye pikipiki walipewa amri ya kusimama lakini walikaidi na kuanza kuwarushia askari risasi. Askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao na kufariki dunia papo hapo,” amesema Mambosasa
Most of the time inakuaga fiction
 
Kuna hawa ndugu zetu wameswali leo! Kamanda anajua hili? Vema nyakati za futlraha wananchi waachwe wafurahi..Tanzania sio Guantanamo bay
 
Back
Top Bottom