DAR: Polisi wamkamata watu 106 stendi ya Ubungo kwa kuwabugudhi na kuwaibia raia

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
DAR: Jeshi la polisi limewakamata watu 106 katika stendi ya mabasi Ubungo kwa makosa ya wizi,uvamizi wa abiria na unyang'anyi wa mizigo

Kamanda wa Polisi kanda ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa anasema polisi waliwakamata watu hao baada ya kufanya msako mkali kufuatia kuongezeka kwa uhalifu unaofanywa kwa abiria waendao mikoani

Watuhumiwa 95 walikamatwa kwa makosa ya kuwabugudhi abiria na kuwanyang'anya mali walizonazo

Watu hao wamepekekwa mahakama ya jiji



Chanzo: Global TV
 
Watu au wapiga debe, mbona wale ni kawaida yao kugombania abiria. Hii serikali inapenda media
 
Wamekamatwa leo,wataachiwa kesho na kesho kutwa tutakua nao tena Ubungo umekua ni igizo endelevu.
 
Afadhali wameondolewa wanaudhi sana zoezi hilo liende na stend zingine kama moshi Nyegezi nk
 
Nyambafu zao, nilikuwa nashangaa tokea muda mrefu kwa nini wanawaacha hao wahuni!
Siku moja walinizingua nikawaambia wanitafutie gari naelekea zanzibar, nlichobaki kukisikia ni kwamba walikuwa wakitaja majina ya viungo vya siri vya binadamu tu!
 
Safi xnaa wanatakiwa kufukuzwa wote wanakera kwa kweli wanaeza kukupandisha gari la ajabu usipokua makin
 
Back
Top Bottom