Dar: Polisi Wamekamata yale Magari na Pikipiki Zilizoibwa, Watuhumiwa 60 watiwa Korokoroni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,054
2,000
1624965528123.png
Oparesheni kali iliyotangazwa dhidi ya majambazi, wanaotumia silaha na wahalifu wengine imefanikisha kupatikana kwa silaha mbili aina ya Bastola ambazo zote zilikuwa zikitumika kutendea vitendo vya kihalifu

Oparesheni hii inajumuisha vikosi vyote vya Jeshi la Polisi na matokeo yake yamezidi kuonekana.

Tarehe 27/06/2021, Polisi Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wananchi walifanikiwa kuipata silaha bastola aina ya Glock 17 yenye namba AMP 490 ikiwa na risasi moja.

Silaha hii ilikuwa imefichwa na wahalifu kichakani maeneo ya Chanika Nguvukazi Wilaya ya Ilala.

Silaha nyingine iliyopatikana ni bastola aina ya Glock DUT 614 yenye namba NE 00079357 iliyotengenezwa nchini austria.

ambayo uchunguzi ulionesha iliibwatarehe 26/06/2021 saa 12 jioni eneo la Hospitali ya Hindu Mandal wilaya ya Ilala kutoka kwa JABI MOHAMED MWASHA (55), Mkazi wa Kinondoni .

Upatikanaji wa silaha hiyo ulitokana na ufuatiliaji mkali unaendelea dhidi ya wahalifu na wahalifu hao wakahamua kutelekeza kwenye ofisi za Posta zilizopo tawi la Kariakoo .

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na msako mkali wa kuwasaka wahalifu wote waliokuwa wanazitumia silaha hizi kufanya vitendo vya uhalifu na kwamba watakamatwa popote walipo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 60 WA MAKOSA MBALIMBALI YA UHALIFU JIJINI DAR ES SALAAM.

Sambamba na mafanikio ya upatikanaji wa silaha aina ya Bastola mbil, Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 60 wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu hapa jijini

Watuhumiwa hawa walikamatwa na vielelezo mabalimbali kama ifuatavyo:-

Magari 03 yenye namba za usajili T 730 BCT Toyota RAV 4 na T 677 DRJ Toyota IST

Pikipiki 04 zenye namba za usajili MC 801 CNG, MC 875 BUR, MC 932 CTE na MC 665 CVD zilikuwa zimeibiwa.

TV 01 aina ya LG NCH 32, FRIJI 01 aina ya HISENSE Simu 05 za aina mbalimbali na LAPTOP 01 aina ya DELL.

MULIRO J.MULIRO - ACP

KAMANDA WA POLISI,

KANDA MAALUM,

DAR ES SALAAM
 

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,096
2,000
msako mkali uendelee

hawa watu hawafai nashangaa kuna watu wanalea kwa kuwatetea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom