Dar - Polisi kizimbani kwa kubaka mtoto akiwa kituoni kikazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar - Polisi kizimbani kwa kubaka mtoto akiwa kituoni kikazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Dec 30, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Polisi aliyedhalilisha watoto ashitakiwa

  Jeshi la Polisi limemfikisha mahakamani askari wake, D5882 Koplo Richard Singano wa kituo cha Gongo la Mboto, kwa tuhuma za kubaka mtoto wa miaka tisa kisha kuwadhalilisha watoto wengine wawili kwa kuwashika shika sehemu za siri wakiwa kituoni na kuwaletea maumivu makali.

  Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kituo kidogo cha Polisi cha Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam. Alisema watoto watatu wa familia mbili tofauti waliokuwa wameokotwa na wasamalia wema walifikishwa hapo kwa nia ya kuhifadhiwa mpaka hapo wazazi wao watakapojitokeza ndipo ilipodaiwa kuwa wakiwa kituoni hapo walifanyiwa kitendo hicho cha kikatili na askari huyo.

  Akielezea tukio hilo, alisema Desemba 24, 2011, walipata taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa jiji pamoja na maofisa wa Ustawi wa Jamii wakieleza kuwa kuna watoto wamebakwa wakiwa katika kituo hicho, ndipo alipoamua kufuatilia suala hilo kwa kina. “Tulipofuatilia suala hilo, tuligundua kuwa, watoto wao wawili wakiwa ni wa familia moja waliletwa kituo cha Gongo la Mboto na wasamalia wema, ambapo ilidaiwa kuwa Desemba 21, mtoto mkubwa ambaye ndiye aliyebakwa alikutwa akiwa amelala katika kibaraza huko Pugu ndipo wasamalia wema hao walipomchukua na kumpeleka kituoni hapo, ambapo watoto wengine nao walikuwa wamepotea ndipo wakapelekwa hapo,” alisema Shilogile.

  Alisema kuwa katika uchunguzi wa awali ilionyesha mtoto mkubwa amekuwa na kawaida ya kuokotwa mara kwa mara na kupelekwa katika vituo mbalimbali vya polisi, ambapo katika kituo cha Gongo la Mboto aliwahi kupelekwa hapo Desemba 13, 2011 na baadaye kuondoka. Alisema Desemba 22 na 23 watoto hao walipelekwa kituo kikubwa cha Ukonga Stakishali ambapo walishinda huko kwa muda wa siku mbili na siku iliyofuata Desemba 24, walipelekwa katika ofisi za Ustawi wa Jamii. Kamanda Shilogile alisema maofisa wa Ustawi wa Jamii waliamua kuwapeleka watoto hao katika kambi ya watu walioathirika na maafa ya mafuriko kwa utambuzi zaidi kwa wazazi wao, ambapo walipelekwa katika kambi iliyopo Shule ya Uhuru Mchanganyiko.

  Alisema Desemba 25, wazazi wa watoto hao walifika katika kambi hiyo kwa nia ya kuwasaka na walipowaona walizungumza nao ndipo walipogundua kuwa watoto wao walifanyiwa kitendo cha udhalilishaji, ambapo walitoa taarifa kwa maofisa wa Ustawi wa Jamii waliokuwepo eneo hilo ndipo ulipotolewa uamuzi wa kwenda kutoa taarifa kituo cha Msimbazi. “Kuanzia hapo ndipo sisi tulipopigiwa simu ambapo tuliamua kulifuatilia suala hilo kwa kina na tukatoa uamuzi wa kwenda kufanya gwaride la utambulisho kwa askari wote waliokuwa zamu siku hiyo, ambapo watoto wawili kati ya hao watatu waliweza kumtambua koplo Singano na hivyo tukamtia hatiani,” alisema.

  Alisema kuwa tayari askari huyo jana alifikishwa mahakamani, baada ya taratibu za kijeshi kufuatwa ikiwemo wa kufikishwa katika Mahakama ya Jeshi na kufukuzwa kazi. Kesi ya askari huyo inatarajiwa kufikishwa tena mahakamani Januari 17, 2012.

  Nipashe
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hii habari haipo kwenye jukwaa stahiki!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sorry, hatukuangalia awali kuwa makini kuliweka panapohusika, ila kazi za polisi hata hapa ni jukwaa lake pia kwa vile zinagusa maisha ya kila siku watu katika masuala ya kisiasa. Labda we polisi hupenda watu wajue madudu yafanywayo na vyombo vya usalama wa raia?
   
 4. K

  Kijinga Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pumbavu! Inaonekana ww huna mtoto hta wa kusingziwa!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wenye nafasi wanapenda mambo yanapowatokea yaendeshwe kisirisiri ili tusijue, lakini mambo kama haya yangempata kabwela parapanda ingelia na kusikika mbali hata kwa wanyama pori.
   
 6. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwacheni akajifunze kazi mpya ya useremala. Babu Seya atampokea..
   
 7. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa ww ulitaka jukwaa gani?Ni vema ungelitaja ili wadau next time wajifunze kitu,ingawaje na hapa ni jukwaa sahihi.Sheria itaamua jambo hili la pongo kubaka.
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hili si jukwaa la habari na hoja machanganyiko au alitaka uiweke wapi
  we ni sawa na mtu anaona nyumba inaungua badala ya kuzima moto unaanza kuuliza nani kawasha huo moto

  huyo polisi ana bahati kama angeletwa kwangu angekiona cha mtema kuni
  kama ushahii uko tight hakuna la zaidi ya kifungo cha maisha cha muhimu ushahidi ujitosheleze
  wapime DNA pia na wahakikishe kulikuwa na michubbuko sehemu za huyo mtoto,na ithibitike kuwa uume wake uliingia kwa huyo dogo na kusiwe na doubt kuwa kituoni alikuwa peke yake wengine walikuwa wapi pia ithibitike hilo na kama huyo dogo alipiga kelele kusema tu kabakwa na huyo askari haitoshi kwan anaweza kusingiziwa pia.
   
 9. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kumfikisha mahakama ya kijeshi na kumfukuza kazi halafu bado anapelekwa mahakama ya raia ni uvunjaji wa misingi ya kikatiba ya protection against double jeopardy (kushtakiwa twice kwa makosa yale yale) pamoja na innocence until proven guilty (kama kesha hukumiwa, kesi ya nini).
  .
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hebu nae akalindwe ka alivokua analinda wenzie
   
 11. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mara kubaka mara upotevu wa dolla elfu 50,haya wapi uadilifu
   
 12. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Koplo Richard Singano kama ulikuwa unawabambika watu kesi uraina basi wengine utakukutana nao huko segedance
   
Loading...