DAR: Ombaomba 60 wakamatwa, kufikishwa mahakamani

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Jumla ya ombaomba sitini (60) wamekamatwa katika msako wa ombaomba unaoendelea katika jiji la Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Magembe alipokuwa akitoa majibu ya uwepo wa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam licha ya kuwepo kwa operesheni ya kuwaondoa.

“Zoezi la ukamataji wa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam linaendelea na ombaomba sitini wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka, wakiwemo watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao wamepelekwa katika vituo vya watoto yatima kikiwemo kituo cha Kurasini,” alifafanua Dkt. Magembe.

Dkt. Magembe alisema kuwa bado ombaomba wamekuwa wakionekana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kuwepo kwa watu wanaotoka mikoani na kuingia katika makundi ya ombaomba kila siku.

Aidha, aliendelea kwa kusema kuwa kutokana na kuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaotoka mikoani na kujiingiza katika makundi ya ombaomba, uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam unashirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoa elimu mikoani juu ya operesheni ya kuondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam wanaosababishwa na watu wanaokuja kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Mapema Aprili mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alitangaza oparesheni kubwa ya kuondoa ombaomba katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo alilitaka Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ustawi wa Jamii kufanya zoezi la kuwaondoa ombaomba wote waliopo Jijini humo.

Aidha, Mhe. Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa fedha kwa ombaomba kuacha mara moja ili wajitafutie fedha wao wenyewe aidha kwa kufanya biashara au kurudi mikoani na kujishughulisha na Kilimo.

Chanzo: Dewji Blog
 
Sasa hapo si wanaenda kula bure, walikuwa wanaomba ili wapate pesa ya kula. Sasa kiulaini wanapata msosi na sehemu ya kulala tena kwa amani chini ya ulinzi hawana hofu yena kama walivyokuwa wanalala barabarani. Nani kawezwa hapo ombaomba au serikali.
 
Du! mchakamchaka kila siku, wanashtakiwa kwa kuomba au kukosa kazi?! Hapo wangefafanua kidogo sheria imekaaje naona kama mahakimu wanachoshwa bure tu kwa kesi ambazo hazihukumiki.
 
Mganga mkuu yupo wizara ya afya na ustawi wa jamii,jinsia Wazee na Watoto, inamhusu mkuu!
 
.
jana wamesema hawataki mashoga mjini wala mazoea wakati wao wenyewe mashoga wanashinda nao na ni marafiki zao. leo wamewashitaki yatima mahakamani kosa eti kwanini wanaomba msaada na wakati huo hizo hela hawatoi wao.
na sijui kesho watasema nini na watafanya nini.

ila hawa mm nawaona wanachez two short au wanajiribisha kuongoza nchi maskini kama nchi ta kitajiri.
kwasababu nchi maskini ombaomba lazima wawepo.
 
Hizi operation za kuondoa omba omba toka enzi ya Ibrahim Kajembo lakini hakuna mafanikio, zitafutwe sababu au suluhisho la kudumu
 
Mganga Mkuu siku hizi kaacha kazi za kutibu anakimbizana na omba omba duh Tanzania kuna maajabu kila siku jambo jipya linajitokeza.Fikiria muda aliotumia kujifunza namna ya kutibu mwanadamu kama hiyo haitoshi tunamrundikia kazi nyingine wakati wapo maafisa ustawi wa jamii na nk sijui wanafanya nini.
 
Wasiwapeleke mahakamani hao dawa yao ni kwenda kusafisha vyoo vya Hospital zetu kwa wiki nzima au mwezi mzima.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom