BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Jeshi la Polisi limewakamata watu wanne (4) kwa tuhuma za kujaribu kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanesco ikiwemo Nyaya aina ya Copper kwa lengo la kuziuza.
Watuhumiwa hao; ni OMARY ALLY, miaka 28, Mkazi wa Tegeta na mwenzake JUMA SULLEIMAN, Miaka 30, Mrangi, mkazi wa Wazo na wanunuzi wa vifaa hivyo ni AMOS JOHN, miaka 30, mkazi wa Tegeta na MOKOLO MACHAGE, miaka 26, mkazi wa Bunju walikamatwa tarehe 10/04/2022.
Watuhumiwa wote hawa wamehojiwa kwa kina na kukiri kuhusika katika matukio ya namna hiyo. Baada ya kupekuliwa maeneo yao walikutwa na viroba vinne vya Nyaya za Copper zilizochunwa.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa onyo kali kuwa halitamvumilia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma na atakayejaribu atakamatwa na mifumo ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria itazingatiwa.
Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.