Dar niliingia na mikosi

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari wakuu,

Juzi Ijumaa wakati natoka safari ya mbali nilikua tayari nilishaingia ndani ya jiji la Dar. Basi kama ilivyo ada ya mizunguko yangu kuna jamaa (wa nyumbani) ambae ni boda boda huwaga namtumia sana katika mizunguko yangu ya hapa na pale.

Basi ikafika kipindi nataka kuelekea Kariakoo, ikabidi nimwambia anirushe kituo cha dala dala cha machinga Kigamboni.

Tulipofika bara barani mara paap askari hao hapo wakati huo walikua na operation ya kusaka waliokua hawakuvaa helmet. Na mimi nilikua mmoja wao.

Lakini mda huo nilikua nimeshashuka boda boda kuna vitu nataka kununua.
Ghafla akaja kijana mmoja yupo kiraia akiwa na piki piki ya boxer.
Nikaona ananiita kwa command, lakini nikampuuza.

Pamoja na yote ilibidi nimfate kwa kuhisi mara ananifahamu. Nikamfuate pale alipokuwa. Akawa ananiuliza "kwanini hujavaa helmet?"

Nikaona hili ni swali la kiboya kwangu na ukizingatia hana uniform ilibidi nigeuke kutaka kuondoka akaja traffic na mavazi hapo ndo nikasimama wakanipakia kwenye bajaji pamoja na yule dereva wangu.

Kufika kituo cha polisi nikakutana na watu wengi wamejazana ndani ya chumba, wakati huo mlikua na akina dada kama wanne kwakweli nilisahau kama nipo mikononi kwa polisi ilibidi hisia zangu zote zielekee kwa wale wadada maana walikua watamu balaa hadi raha.

Lakini pamoja na yote, ikabidi nitumie wadhifa wangu nikatoka na kumuacha boda boda ndani. Ila na yeye nilienda kumpigania polisi hawakunielewa.
Maana walinambia tumekuachia wewe usimtoe na mwingine.

Uwezo wa kumtoa nilikua nao kwa kupitia polisi ambae yupo hapo hapo Kigamboni lakini sikutaka kumshirikisha kwa kuwa sikutaka ajue kwamba nimeshafika Tz. Ilibidi wale watu wachukuliwe na coaster mpaka Chang'ombe.
Huko ndo nilifanya utaratibu akatoka. Chombo chake kiliandikwa makosha manne sawa na laki moja na ishirini.

Nilifanya nae mawasiliano akanambia mke wake amekwenda kukopa kapata elfu 80 ila hawakutaka kumtoa mpaka zikamilike. Ikanibidi nimtumie 45 ili akamilishe atoke. Lakini kilichonishangaza kwa polisi wanawapiga faini lakini mbona risiti walikua hawawapi? Au kuna mfumo mpya wa ulipaji?

Embu wataalam wa haya mambo wanijulishe hapa inakuaje kuhusu malipo?


Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom