Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 255
Ni imani yangu kuwa mtaniunga mkono kwa hoja zangu kuwa Dar ni eneo hatarishi kuliko maeneo yote nchini TZ. Ni eneo la hatari sana kwa sote kwa maana kwamba wale wenye nazo na kina sisi wakeshaohi. Haya ni mambo yanayofanya Dar kuwa si mahali salama:
- kuwa na vishawishi vingi vyenye kuvutia mahusiano ya ngono matokeo yake HIV
- Kuwepo kwa wimbi kubwa la vibaka na wezi, matapeli nk
- Uchafu wa mazingira uliotukuka
- Harufu mbaya takribani maeneo yote yakiongozwa na Kwatumbo, Gaitimaji UDSM, Kivukoni karibu na Waziri mkuu nk
- hadha kwa wanafunzi wanaosoma day
- Msongamano wa magari na huduma za jamii hasa bank ya NMB
- Mgao wa umeme (kwa Dar ni hatari zaidi kwakuwa watu wengi hutegemea umeme)
- Rushwa na kutofatwa kwa sheria
- uwepo wa dawa za kulevya na watumiaji wengi
- Ombaomba wegi na vichaa na wehu
- kuna magonjwa ya milipuko hasa kipindupindu Buguruni ikiwa inaongoza
- Minara mingi ya simu ambayo husambaza mionzi hatarishi
- kuwepo bidahaa feki kwa wingi vikiwemo vyakula
- ukosefu wa utawala bora kwa kulemewa na miundombinu
- ..............