Dar ni eneo hatarishi

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,401
1,500
Ni imani yangu kuwa mtaniunga mkono kwa hoja zangu kuwa Dar ni eneo hatarishi kuliko maeneo yote nchini TZ. Ni eneo la hatari sana kwa sote kwa maana kwamba wale wenye nazo na kina sisi wakeshaohi. Haya ni mambo yanayofanya Dar kuwa si mahali salama:
 1. kuwa na vishawishi vingi vyenye kuvutia mahusiano ya ngono matokeo yake HIV
 2. Kuwepo kwa wimbi kubwa la vibaka na wezi, matapeli nk
 3. Uchafu wa mazingira uliotukuka
 4. Harufu mbaya takribani maeneo yote yakiongozwa na Kwatumbo, Gaitimaji UDSM, Kivukoni karibu na Waziri mkuu nk
 5. hadha kwa wanafunzi wanaosoma day
 6. Msongamano wa magari na huduma za jamii hasa bank ya NMB
 7. Mgao wa umeme (kwa Dar ni hatari zaidi kwakuwa watu wengi hutegemea umeme)
 8. Rushwa na kutofatwa kwa sheria
 9. uwepo wa dawa za kulevya na watumiaji wengi
 10. Ombaomba wegi na vichaa na wehu
 11. kuna magonjwa ya milipuko hasa kipindupindu Buguruni ikiwa inaongoza
 12. Minara mingi ya simu ambayo husambaza mionzi hatarishi
 13. kuwepo bidahaa feki kwa wingi vikiwemo vyakula
 14. ukosefu wa utawala bora kwa kulemewa na miundombinu
 15. ..............
ndg, ebu ongezea
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,468
2,000
misafara ya jk KILA KUKICHA
+ misafara ya magereza+ kuwapo kwa mbu wengi hasa wale waliozalishwa katika viwanja vya jangwani.+ kuwepo na kuzagaa kwa mabomu yaliyochimbia arhini ktk makazi ya watu.+ kuwepo kwa wageni wengi.......................................
 

kijana makini

Member
Nov 5, 2010
47
95
kila baada ya nyumba bars na guest houses kibao na zote zajaa kuanzia j3 mpk j3 hapo ndipo utakaposhangaa..
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,321
2,000
- MBOGA ZA MAJANI MABONDENI HASWA MSIMBAZI KUMWAGILIWA MAJI TAKA TENA YENYE KINYESI..............
-WATOTO WADOGO KUUZA MIILI HUKU WAZAZI WANAKENUA MENO TUU KISA WANALETEWA MSHIKO WA KIJINGA.....
-GUEST BUBU NA BAR KILA MAHALI MPAKA KWENYE MAENEO YA SHULE.
-MATAPELI WA KILA AINA ANZIA WA MADINI FEKI(papaa naniliu) mpaka wanaouza cheni na hereni feki mitaani,
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,468
2,000
Askari jeshi kutandika wananchi bila serikali kuhoji.
Polisi kuua raia kwa risasi za moto.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom