Uzalendo ndio huu, Dar-New York kwa B787-8 gharama ya mafuta ni TZS 267M

Unataka watu wasahau kwani watasahau lini kutwa wanakumbushwa,

Mwandishi namsifu amekuja na utetezi wa hoja,

CCM sihami mpaka nakufa tunahazina kubwa,

Karibu Samia nitakuja airport kesho
Kweli nimeamin majina na tabia za watu hufanana
 
Acheni pambio bei ya First class mtu moja sio chini ya USD 12,000 zidisha mara idadi ya watu aliyoenda nayo
 
Kwani marais waliokwenda pale hawana hizo video?

Wivu wa kijinga huu.
Nimeuliza, na nauliza tena, ni kipi alichoenda kufanya huko ambacho hakingeweza kufanywa kwa video conferencing? Kwani kuuliza imekuwa wivu siku hizi?
 
Kumbe mfuta ya ndege ni cheap kuliko ya magari thus its cheap kutumi ndege kuliko gari
 
Napenda akili za kiwango hiki,

Nikweli gharama za kwenda na ndege NY nikubwa sana hata kama angeeda na watu 100,

Rais Samia ni aina nyingine ya Nyerere nakubaliana na hii hoja,

Mungu ampe afya na Maarifa zaidi,
Daah kwa hesabu za kiusafiri tu hapo kwa hao watu 50, tayari ameshafika zaidi ya 140m. Kuna wambea waliandika kuwa ameenda na watu kama 100 hivi, sasa sijui amejumlisha wanausalama na wafanyabiashara! Na jamaa amepiga hesabu ya economy class, sina hakika kama alisafiri hivyo, na hao wafanyabiashara kama walisafiri hivyo, baadhi ya senior staff waliokuwepo nao walisafiri economy?

Hivi daktari wake huwa anabaki nyumbani au anasafiri naye?

Hivi vi-per diem na vyenyewe si sehemu ya safari? Malazi na makulaji?

Watu 10 tu wangetosha kwakweli!

Fashionista wake hakwenda? Safari hii hatujaambiwa amebadili nguo mara ngapi kwenye huo mkutano!

Pengine ndege zetu bado hazijapata kibali cha kimataifa, labda!
 
Kwa kufanya hivi, kweli anastahili pongezi Sana. Ila alikosea kutoenda na mkaliman wa kiswahili. Angeongea kiswahili ingekuwa Bomba Sana maana kila mtu lazima ajivunie na chake.....

English tunapo iongoea tunawapa vichwa sana wazungu.
 
WaTzn ni watu walalamishi Sana sijui ingekuwa kama Hawa Angola ingekuaje? 😂😂

Linganisha gharama za Rais wa Angola alizotumia na Rais wetu👇

Screenshot_20210927-080437.png


Screenshot_20210927-080506.png
 
Tanzania ya Samia ni noma,

Umeme bei Chee EAC
Petrol bei Chee EAC
Disel bei Chee EAC
M|taa bei Chee EAC
Data (MB) bei Chee EAC
Maji bei Chee EAC
 
Wee Mataga umesahau kuweka namba ya simu,unaweza ukalamba teuzi kimzaha mzaa,endelea kuwa CHAWA.

Na Raisi wa Zambia H.H asemeje? angeenda na wasaidizi wake 3,alafu wewe unasema Raisi wetu ameenda na watu 50!
Kwa taarifa zilizopo alienda na watu zaidi ya 100. Kwa hiyo hakuna alichosave hapo. Rais wa Zambia kaenda na watu watatu tu.
 
Wee Mataga umesahau kuweka namba ya simu,unaweza ukalamba teuzi kimzaha mzaa,endelea kuwa CHAWA.

Na Raisi wa Zambia H.H asemeje? angeenda na wasaidizi wake 3,alafu wewe unasema Raisi wetu ameenda na watu 50!
Mlinzi mmoja.
Katibu wa Rais
Msemaji wa Ikulu.

Hao tu kaenda nao.
 
Back
Top Bottom