Dar: Ndege ya kijeshi ya Marekani kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA)

Ni ndege aina ya C-17 Globemaster imeonekana terminal 3 ya JNIA tarehe 1 July 2021....
Amini hilo.
Sio mara ya kwanza kuja .

Kuna ambayo kabla ya kuja lilipita gari likitoa matangazo ya kujiadhari na kelele (mlio mkubwa)wa ndege itakayo wasili baada ya masaa 3 kwa kweli nilikuwa pale airwing pamoja na uziefu wangu wote nilishtuka manaa kilishuka kitu sijawahi ona ndege ya kijeshi kubwa vile na ule mlio tuu na upepo nyie acheni tuu
 
C-17 Globemaster inayo uwezo wa tani 76 za mzigo. Kwa hesabu za haraka tani 76 za chanjo zinachanja umati wa Afrika nzima mara 9.23. Nadhani shehena ni zaidi ya chanjo , nahisi breakfast cereals na kadhalika+etc za ubalozi.:cool:
 
19 Jun 2018
Let us show you what's inside a C-17 Globemaster as seen at Berlin's 2018 ILA...

Source : Simply Aviation
 
Kumekuwa na taarifa kuhusu ujio wa ndege ya jeshi la Marekani nchini Tanzania iliyotua uwanja wa ndege wa mwl Nyerere. Habari hizi zilienea kwenye mitandao na watu wakawa wanajiuliza kulikoni?

Hasa kwa kuwa ujio huu umetokea kipindi ambacho kumekuwa na habari ya Tanzania kuruhusu chanjo ya corona. Je Marekani ndo inatuletea hizo chanjo sasa au? Ikizingatiwa kuwa Marekani ilishatangaza kugawa chanjo takriban bilioni moja wakati wa mkutano wa G7!! Inaelekea hawa jamaa "wakarimu" sana.

Ila kama wangetuuliza kipau mbele chetu tungesema tupatiwe pesa za kumalizia reli standard gauge haraka na kumalizia mradi wa kufua umeme wa bwawa la Mwl Nyerere (Stigler's Gorge).

Kuhusu corona tumeithibitishia dunia kuwa tunaweza kupambana nayo wenyewe kwa kumtanguliza Mungu na kwa kutumia tiba mbadala kama nyungu nk. Hata hivyo kwa hali inavyoonekana kuna matumaini makubwa sana kuwa Mungu ameshatujalia herd immunity, hata makaburu wanajua hivyo japo hawawezi kusema wazi chanjo zao zisije kudoda.

Vinginevyo bila herd immunity tungekuwa kama India!! Na hakuna ugonjwa na vifo vinavyoweza kufanywa siri! Utukufu kwa Mungu.

Baadaye Marekani walidai kuwa ndege hiyo imeleta vifaa kwa ajili ya balozi zao!! Mungu anajua.
 
Baada ya ujio huu tutaona!! Kama ukitokea mlipuko wa corona muda mfupi baada ya ujio huu tutajiuliza mara mbili!! Mbona haukutokea kabla? Mungu apishe mbali!
 
Back
Top Bottom