Dar: Naibu Waziri Mhe.William Ole Nasha, azindua Africa Code week 2019

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha, amezindua africa code week 2019, ambayo ni elimu inayotolewa kwa wanafunzi teknohama. Uzinduzi huo ulifanyika hotel ya Sea cliff tarehe 05 September 2019
IMG_20190905_160314_9.jpg

Naye Mkurugenzi wa COSTECH, Dokta Amos Nungu, ameeleza kwamba wanajivunia na kushukuru kuwepo kwa elimu hii ya coding kwa watoto wadogo. Kwani inawezesha Tanzania ijayo kuwa na uwezo wa kushindana kiteknolojia. Kwamba Tanzania ya viwanda inaenda sambamba na teknolojia

Mheshimiwa Balozi Paul Sherlock wa Ireland katika Nchi za Tanzania, Seychelles, Burundi na Comoro, amesema nchi yake itaendelea kuhakikisha watoto wanakuwa na uwezo wa ushindani katika Ulimwengu huu wa Kidigitali kwa kuhakikisha watoto wanawezeshwa kuwasiliana na komputa kuanzia utotoni.


Africa code week inawawezesha watoto kunifunza lugha ya computer. Watoto wanafundishwa kuongea na computa ili waweze kufanya programming itakayowawezesha kutengeneza Application mbalimbali ili kukuza teknolojia nchini.

Malengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na kizazi cha kidigitali ili kukabiliana na ulimwengu ujao.


Dar Teknohama business incubetor (DTBI) na Apps&Girls, Wenye dhamira ya kukuza vipaji na ubunifu wa Ujasiriamali katika teknolojia kujenga uhusiano na vyuo vikuu, vyuo vya kati, vituo vya utafiti na jamii ya Wajasiriamali, ili kukuza ajira na biashara kwa ajili ya maendeleo endelevu na Ustawi wa Jamii ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
 

Attachments

  • Apps & Girls - ACW.pdf
    980.3 KB · Views: 6
Naona tatizo kwa kizazi chenyewe kwenye matumizi ya teknolojia husika..
 
Back
Top Bottom