Dar: Mwalimu Mkuu wa shule ya Real Hope akamatwa akidaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 100,000

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Temeke, imemkamata Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Real Hope iliyopo Mbagala Majimatitu, Dar es Salaam, Ayubu Mtondo kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa TAKUKURU, Ramadhani Ndwatah, alisema mwalimu huyo alipokea Sh 100,000 ili kumsaidia kumrudisha kazini mtumishi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.

Ndwatah alisema Februari 28, mwaka huu, saa 11 jioni, mwalimu huyo akiwa ofisini kwake, alipokea fedha za mtego ili aweze kumsaidia mtumishi wake aliyesimamishwa kazi kurudi kazini.

Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kushawishi kuomba na kupokea rushwa.
 
Back
Top Bottom