Dar: Mtoto Zuhura Ayubu, apigwa, achomwa na kifaa cha moto na baba yake mzazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Salaam Wakuu,

Kuna tukio la kusikitisha sana limetokea leo Kawe Ukwamani katika Wilaya ya Kinondoni.

Mtoto Zuhura (13) wa darasa la Sita Shule ya Msingi Kawe, kapigwa kwa fimbo, kachomwa moto na chuma kilicho chemka kiasi kwamba hata alipo hawezi kuongea Vizuri.

Ayubu Ruwa baada ya tukio kaenda zake kwenye kazi zake bila kuchukua hatua yoyote ya kuhakikisha mtoto anapewa huduma ya kwanza. Majirani ndo sasa Wanahangaika kuwasaidia.

Hii nmeileta hapa kama taarifa kwa wanaohusika na Utetezi wa Watoto (CDF), haki za Wanawake na Jeshi la Polisi ili waweze kuchukua hatua.

Huu ni unyanyasaji wa kijinsia haukubaliki.

Inanilazimu kuweka picha baadhi ili waone umuhimu wa kulifuatilia hili swala

Kisa kilikuwa hivi

Jana alifua nguo za shule, usiku mtoto mwenzake alianua, ilipofika asbh baada kuangalia saa alienda chumba cha jirani kuomba sare zake za shule.

Nyumba jirani ilikuwa na mtoto wa kike wa rika sawa na Zuhura, alipotoka kule baba yake akawa anamuuliza ametoka wapi mtoto akasema alienda kufuata sare zake

Ndipo kipigo kikaanza hadi kufikia hatua hiyo.

Stay tuned

IMG_20210121_110759_327.jpg
IMG_20210121_110753_370.jpg
IMG_20210121_110748_212.jpg
IMG_20210121_110741_778.jpg
IMG_20210121_104109_832.jpg
IMG_20210121_104105_800.jpg
IMG_20210121_104058_110.jpg
 
Alitaka kuua ila hasira ni shetani mbaya sana..sasa hivi huyo mzazi anahaha..mahali alipo anaweza akatokomea moja kwa moja.
 
Depression ni mbaya sana.Haya matukio yamezidi sasa.Unaweza kufikiri kuwa nchi ipo vitani!
 
Akikamatwa na kueleza kisa ntajua nichangie nini, ila nimeshaanza kuhisi huyo baba mtu ni mtu wa aina gani,this is too much...
Akamatwe na wamshughulikie/wamkomeshe kadri watakavyoona inafaa. Sina hata haja ya kujua kisa gani kimepelekea afanye ukatili huo
 
Back
Top Bottom