Dar: Mtoto wa miaka 17 ampiga risasi mtoto mwenzake na kumsababishia kifo

Muuaji miaka 17
Marehemu miaka 10

Walikuwa wanacheza. Miaka 10 ni umri wa darasa la nne au tano, huyu wa kidato cha 3
 
Hii kesi ikiwa kwa Rumanyika J. dogo ana wakati mgumu. Yule mzee anakwambia matendo ya kiutu uzima yakifanywa na mtoto huyo ni mtu mzima

Sasa kwa dogo kazi anayo
 
Ila bado yawezekana huyu mtoto amejifyatulia mwenyewe kwenye harakati za kuchezea akijua ni toy

Yawezekana pia huyo mtoto alikuwa anamnyang'anya dogo kwenye hizo harakati ikamfyatukia

Yawezekana mambo mengi sana

Yawezekena pia huyu dogo kitendo cha kumchukua na kumpeleka kwao kilitokana na uoga na kusema ni shot ya umeme yawezekana ni uoga au pia inawezekana na yeye hakuwa anajua kilichotokea

Labda alikuwa chumbani kwake akasikia mlio/kishindo akawaza ni shot ya umeme, pengine alimuacha dogo akiangalia Tv sebuleni ivyo ni raisi kuhusi ni shot dogo labda kagusa gusa nyaya.

Kusema huyu mtoto kampiga mwenzie risasi ni jambo la ajabu ikiwa hakuna aliyeshuhudia tukio. Ingetosha kusema mtoto afa kwa risasi Dar. Kisha iwekwe iyo stori sasa.

Mambo ni mengi pengine dogo alikuwa hata hajui kama baba yake ana mkwaju/bastola.

Kwani zilipita dakika ngapi tangu mlipuko hadi dogo kuletwa na aliyemleta alikuwa kwenye hali gani na je bastola imekutwa wapi na tukio lilitokea eneo gani hapo nyumbani?

Kama bastola imekutwa ndani inaweza ikawa sababu ya dogo kutokufanya ilo tukio maana angeenda kuificha hiyo bastola si kashasema ni shot ya umeme, kwanini ushahidi ubaki wazi wazi?.

Anyway tuishie hapa kwanza.
 
Akianza shule (darasa la 1)na miaka 7 atamaliza darasa la 7 akiwa na miaka 13

Ataanza kidato Cha Kwanza akiwa na miaka 14 then 16 atakuwa kidato Cha tatu

At ceteris peribus
Anaanza la kwanza akiwa na miaka 7, lakini anamaliza la kwanza akiwa na miaka 8
 
Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Ilala linamshikilia Juma Shamata kwa kushindwa kuhifadhi eneo salama bastola yake, hali iliyosababisha mtoto wake wa miaka 17 kuitumia kwa kumpiga risasi mtoto mwenzie Ikhissan Abdilahi (10) na kumsababishia kifo.

Jeshi hilo pia linamshikilia mtoto huyo wa kidato cha tatu kwa tuhuma za mauaji.

Tukio hilo lilitokea Aprili 2 katika mtaa wa Viwege kata ya Pugu nyumbani kwa Shamata ambako Ikhissan alikwenda kucheza.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya Ikhissan kuingia kwenye nyumba hiyo walisikia kishindo na punde mtoto aliyefanya tukio hilo alitoka akiwa amembeba na kumrejesha nyumbani kwao akieleza kuwa amepigwa na shoti ya umeme.

Shangazi wa marehemu aitwaye Aisha Hussen alisema; “Nilikuwa nimekaa kwenye kibaraza hapa nje, Ikhissan alikuwa anaendesha baiskeli, alipofika pale (kwenye nyumba aliyopigwa risasi) akaingia ndani, baada ya muda mfupi tukasikia mlio mkali, lakini hakuna aliyehisi kwamba inaweza kuwa risasi.

“Ghafla akatokea mtoto wa nyumba ile akiwa amembeba Ikhissan na kumleta hapa nje ya geti akamuacha akisema kwamba amepigwa na shoti ya umeme, nilimkimbilia nikamchukua kumuingiza ndani kwa ajili ya huduma ya kwanza maana alikuwa akivuja damu,” alisema Aisha.

Baada ya kumchunguza kwa dakika kadhaa waligundua kuwa alikuwa na tundu kifuani ambalo lilitokeza upande wa pili ndipo walipomuwahisha hospitali ambako waliarifiwa kuwa ameshafariki dunia.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Moses Fundi alisema yupo mtoto aliyekuwa anacheza na mwenzake kisha kumjeruhi na risasi iliyopelekea kupoteza maisha.

Kamanda Fundi alisema jeshi hilo linamshikilia mwanafunzi huyo na baba yake kwaajili ya mahojiano ili kujua ukweli wa tukio hilo.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa kulikuwa na uzembe katika uhifadhi wa silaha hiyo, jambo lililosababisha mtoto kuifikia.

Alisema kuwa silaha haiwezi kuhifadhiwa sehemu kama juu ya kabati, kama mtu anamiliki silaha utaratibu wa kuhifadhi unafahamika, ikiwamo kuifungia kwenye sanduku la chuma.

“Tumegundua silaha inamilikiwa kihalali, lakini inawezekana kuna uzembe katika utunzaji wa silaha hiyo, kama mtoto anaweza kuichukua ina maana hata mwizi angekuja angeweza kuichukua,” alisema kamanda Fundi.
 
Ndiyo hii wakati midogo ilikuwaga mijunior. Kuna mitoto huwa ni mitundu hadi kero. Kila kitu linataka kujaribu, halijali matokeo wala nini. Inapokua ndiyo inakuwa mi antisocial na mi psychopath.
 
Mtoto Huyo aliwezaje kuikoki na kuifyatua kumlenga mwenzie? Nahisi mmiliki WA silaha ndiye muuaji ila kamsingizia dogo kwa hofu ya kesi
 
Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Ilala linamshikilia Juma Shamata kwa kushindwa kuhifadhi eneo salama bastola yake, hali iliyosababisha mtoto wake wa miaka 17 kuitumia kwa kumpiga risasi mtoto mwenzie Ikhissan Abdilahi (10) na kumsababishia kifo.

Jeshi hilo pia linamshikilia mtoto huyo wa kidato cha tatu kwa tuhuma za mauaji.

Tukio hilo lilitokea Aprili 2 katika mtaa wa Viwege kata ya Pugu nyumbani kwa Shamata ambako Ikhissan alikwenda kucheza.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya Ikhissan kuingia kwenye nyumba hiyo walisikia kishindo na punde mtoto aliyefanya tukio hilo alitoka akiwa amembeba na kumrejesha nyumbani kwao akieleza kuwa amepigwa na shoti ya umeme.

Shangazi wa marehemu aitwaye Aisha Hussen alisema; “Nilikuwa nimekaa kwenye kibaraza hapa nje, Ikhissan alikuwa anaendesha baiskeli, alipofika pale (kwenye nyumba aliyopigwa risasi) akaingia ndani, baada ya muda mfupi tukasikia mlio mkali, lakini hakuna aliyehisi kwamba inaweza kuwa risasi.

“Ghafla akatokea mtoto wa nyumba ile akiwa amembeba Ikhissan na kumleta hapa nje ya geti akamuacha akisema kwamba amepigwa na shoti ya umeme, nilimkimbilia nikamchukua kumuingiza ndani kwa ajili ya huduma ya kwanza maana alikuwa akivuja damu,” alisema Aisha.

Baada ya kumchunguza kwa dakika kadhaa waligundua kuwa alikuwa na tundu kifuani ambalo lilitokeza upande wa pili ndipo walipomuwahisha hospitali ambako waliarifiwa kuwa ameshafariki dunia.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Moses Fundi alisema yupo mtoto aliyekuwa anacheza na mwenzake kisha kumjeruhi na risasi iliyopelekea kupoteza maisha.

Kamanda Fundi alisema jeshi hilo linamshikilia mwanafunzi huyo na baba yake kwaajili ya mahojiano ili kujua ukweli wa tukio hilo.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa kulikuwa na uzembe katika uhifadhi wa silaha hiyo, jambo lililosababisha mtoto kuifikia.

Alisema kuwa silaha haiwezi kuhifadhiwa sehemu kama juu ya kabati, kama mtu anamiliki silaha utaratibu wa kuhifadhi unafahamika, ikiwamo kuifungia kwenye sanduku la chuma.

“Tumegundua silaha inamilikiwa kihalali, lakini inawezekana kuna uzembe katika utunzaji wa silaha hiyo, kama mtoto anaweza kuichukua ina maana hata mwizi angekuja angeweza kuichukua,” alisema kamanda Fundi.
Nilipokia na miaka 11 tayari nilikua mkubwa
 
Back
Top Bottom