Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
5,206
2,000
Lakini usiku huo muda mfupi kabla ya tatizo hilo la kukutwa amefariki alikuwa anakunywa pombe na rafiki yake pale sokoni Makumbusho stendi na alikuwa amelewa sana(kulingana na wenyeji sokoni ambapo Blandina naye ni mwenyeji mno hilo eneo kwani aliwahi kuwa na jiko la chakula na ana rafiki yake mpendwa).

Wenyeji wao wanahisi ni ajali ya pikipiki kwa sababu alipokuwa amelewa muda wa usiku aliita pikipiki na baadhi wakamzuia kwamba achukue taxi kulingana na alivyokuwa amelewa na hali yake ya mkono lakini alikataa na kuondoka na pikipiki kwa safari ya Bunju usiku ule. Baada ya muda walipata taarifa ya kuwa amepata ajali na kufariki maeneo ya mwenge.

Hapa polisi wanaweza kuanzia pale alipokuwa anakunywa na wakaongea na rafiki yake na wakaangalia kiwango cha pombe na aina ya majeraha. Nadhani hapo watakuwa wameanza kupata picha kamili ya tukio hilo.

Suala la hao bodaboda waliosema hivyo huenda wamemlinda mwenzao. Wachunguze yote ili wasitokee watu wakahamisha uchunguzi kwa propaganda.

Haya ndio niliyasikia siku ya jana jumapili baada ya kifo chake.
Mtaani tunasikia mengi
Kuna kitu kimoja sijaelewa hata kama ni hao wauwaji wa kwenye Noa kama inavyosemekana ndio waende watupe mwili kwenye sehemu ambayo wao boda boda wanapaki piki piki zao!!???
hii haiingii akilini mara nyingi wauwaji hutupa miili sehemu ambazo hawaonekani!!??
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,376
2,000
EastAfricaTV’s_Instagram_post:_“#PICHA_Ibada_ya_kuaga_mwili_wa_aliyekuwa_mtangazaji_wa_@itvtz_...jpg


Huyu mama ameokotwa Mkoani Dar es Salaam njia panda ya ITV akiwa kauliwa, wewe Mambosasa ni RPC wa kanda Maalum , tunaamini unao uwezo wa kuwasaka wauaji na kuwakamata kama ufanyavyo kwa wahalifu wengine, ama basi toa kauli ili tufahamu unachokifahamu kwenye hili.

Marehemu Lwajabe alipokutwa Mkoa wa Pwani huko Mkuranga huku mwili wake ukiwa umetundikwa juu ya mti ukiwa ndani ya jezi mpya ya timu ya Chelsea , ambayo hakuwahi kuwa nayo nyumbani kwake.

Kamanda Mambosasa ulijitokeza na kutoa Taarifa kwamba Ndugu Lwajabe alijinyonga, tena wala haikupita muda mrefu japo tulishangaa kwanini taarifa ile hakutoa RPC wa Pwani ila ukatoa wewe! sasa leo kuna jambo ndani ya eneo lako kabisa yaani lakini ni kama haupo, tunaomba maelezo yako mkuu kama ulivyoyatoa kwingine.

Ni hayo tu kwa leo
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,338
2,000
Hivi hujui kuwa Mungu pia ni nafsi? Vp naye ataonja mauti???

Toka huko gizani mkuu!

YESU NI MWOKOZI
Hizi Imani hizi ni vema kila mtu akaamini kivyake...., Hivi kwa mujibu wa Kitabu chako Yesu Hakusurubiwa ? Yaani it is written kwamba alikufa siku ya tatu Akafufuka ?, Au wewe ulielewaje ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom