Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Duh. Haya Mambo wakati wa JPM yalianza kuwa history.

Nilikuwa na mpango wakwenda kutoa cash kesho itabidi nifanye utaratibu mwingine.
 
Mbona unatoa habari haijitoshelezi? Unatetemeka? Marehemu ameuwawa hapo ITV? Kwa nini Henry Mabumo ndio aje kuutambua mwili?
Ipo hivi mkuu au labda hata mtoa mada hajui hii.

Mara nyingi waandishi wa habari wanafahamika kwa wananchi na wananchi wengine wana namba za waandishi so likitokea tukio popote wa kwanza anapigiwa anakuja ndipo kupitia huyo mwandishi yeye anapiga simu polisi.

Njia hii inatumiwa na wananchi wengi kuepuka lawama za kukamatana eti utoe ushahidi ilikuwaje wakati na wewe ulikuwa mpita njia.
 
Lakini usiku huo muda mfupi kabla ya tatizo hilo la kukutwa amefariki alikuwa anakunywa pombe na rafiki yake pale sokoni Makumbusho stendi na alikuwa amelewa sana(kulingana na wenyeji sokoni ambapo Blandina naye ni mwenyeji mno hilo eneo kwani aliwahi kuwa na jiko la chakula na ana rafiki yake mpendwa).

Wenyeji wao wanahisi ni ajali ya pikipiki kwa sababu alipokuwa amelewa muda wa usiku aliita pikipiki na baadhi wakamzuia kwamba achukue taxi kulingana na alivyokuwa amelewa na hali yake ya mkono lakini alikataa na kuondoka na pikipiki kwa safari ya Bunju usiku ule. Baada ya muda walipata taarifa ya kuwa amepata ajali na kufariki maeneo ya mwenge.

Hapa polisi wanaweza kuanzia pale alipokuwa anakunywa na wakaongea na rafiki yake na wakaangalia kiwango cha pombe na aina ya majeraha. Nadhani hapo watakuwa wameanza kupata picha kamili ya tukio hilo.

Suala la hao bodaboda waliosema hivyo huenda wamemlinda mwenzao. Wachunguze yote ili wasitokee watu wakahamisha uchunguzi kwa propaganda.

Haya ndio niliyasikia siku ya jana jumapili baada ya kifo chake.
Mtaani tunasikia mengi
 
Lakini usiku huo muda mfupi kabla ya tatizo hilo la kukutwa amefariki alikuwa anakunywa pombe na rafiki yake pale sokoni Makumbusho stendi na alikuwa amelewa sana(kulingana na wenyeji sokoni ambapo Blandina naye ni mwenyeji mno hilo eneo kwani aliwahi kuwa na jiko la chakula na ana rafiki yake mpendwa)...
Kifo cha ajali kinaonekana tu. Jeraha haliwezi kua jichoni pekeyake.
 
Back
Top Bottom