Dar mpaka Moshi: Abiria wapandisha mizuka hatari

Mkuu;
Watanzania wengi wana macho na masikio!

Kuna baadhi ya watu wanadhani Rais Magufuli ni ''mshamba'' wa kisiasa lakini kama ukichunguza kwa undani utagundua ni kati ya wanasiasa wanaojua kulishika kundi la wananchi wa kipato cha chini ambao kwa Tanzania ndio wengi!

Wanasiasa wa upinzani kama hawatalishika hili kundi la wananchi wa ''hali ya chini'' hata ajenda zao sijui za kufanya maandamano au migomo hawatafanikiwa!

Kumbuka wananchi wengi sio wanasiasa bali wanachopenda ni kuona angalau serikali inaonyesha nia ya kutatua changamoto na matatizo yao hata kama haiyatatui yote.

Kama unatembea katika maeneo mengi hasa huko vijijini nadhani utakubaliana na angalizo langu!
 
Hmm...ina maana usafiri wa hizi treni unabamba sana au ni propaganda tu?

Kuna njia moja tu ya kulijua hilo.

Itabidi nami nipande moja ya hizi treni kabla mwaka haujaisha.

Naona sasa hata ‘Wachaga’ wanamkubali Anko Magu 🤣



Kwa basi kwenda mikoani ni mtihani mkubwa, vile vile inachosha na nafasi ni ndogo ukilinganisha na treni. Hawa hawa Wachaga walikuwa wanalia Ukanda yaani ni kuchafuana tu bila hata kuangalia nini kinajiri. JPM anafanya kazi kubwa kuondoa matatizo ya Tanzania kwenye usafiri na miundo mbinu, tuombe uzima tu hadi akimaliza muda wake. Hapa Kazi tu mimi nasubiri safari za ATCL ulaya.
 
Kwa basi kwenda mikoani ni mtihani mkubwa, vile vile inachosha na nafasi ni ndogo ukilinganisha na treni. Hawa hawa Wachaga walikuwa wanalia Ukanda yaani ni kuchafuana tu bila hata kuangalia nini kinajiri. JPM anafanya kazi kubwa kuondoa matatizo ya Tanzania kwenye usafiri na miundo mbinu, tuombe uzima tu hadi akimaliza muda wake. Hapa Kazi tu mimi nasubiri safari za ATCL ulaya.

Kusema ukweli mabasi mengi yanayosafiri masafa marefu yana leg room ndogo sana.

Tutaona huu usafiri wa treni utavyokuwa maana kuna wakati flani hivi ni kama ulikufa kabisa.
 
Ni kweli kabisa.

Rais Magufuli siyo mshamba kivile ambavyo baadhi ya watu wangependa tuamini.

Tukielelea 2020, Magufuli ana mtaji mkubwa sana wa kisiasa.

Na mtaji huo ni hao watu wa ‘hali ya chini’.
Mkuu;
Jaribu kufikiri kama mambo yaliyofanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu yangefanyika kabla ya 2015 unadhani kungetokea nini? Nakuhakikisha wananchi wangepambana na serikali na wasingekubali.

Wanasiasa wa vyama vya upinzani kwa sasa hawana mtaji wa kundi la wananchi ''walalahoi'' ambao ''hawana cha kupoteza katika maisha yao''.

Kwa sasa huwezi kuwahamasisha vijana wa vijiweni, wafanyabiashara ndogondogo na bodaboda waandamane wakati wanaona serikali inafanya juhudi za kutatua matatizo na changamoto zao.

Kundi linalopiga kelele kwa sasa ni kundi la wananchi ambao ''wana cha kupoteza katika maisha yao'' na kwa mantiki hiyo hawawezi kujitokeza barabarani kwa sababu kuwekwa ndani ni kupoteza hata kile walichonacho katika maisha yao!
 
Back
Top Bottom