Dar: Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA, uamuzi wa rufaa ya kina Mdee, Bobi Wine yupo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,306

Halima Mdee na wenzake 18 wakiwa chumba maalum kilichoandaliwa wakisubiri kusikilizwa kwa rufaa zao kupinga kufukuzwa unachama. Rufaa hizo zinasiiilizwa na wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA, Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Wamesema wako tayari kwa lolote.

Subpost%202%20-%20Tuko%20ndani%20tayari%20kwa%20kazi%20ya%20chama%20na%20Nchi.%20(%20480%20X%2...jpg

Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba kile kikao kikubwa kabisa cha maamuzi Kikatiba cha CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), leo 11/5/2022 kinafanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kikao hiki ni cha kawaida cha chama hicho na ambacho hufanyika angalau mara moja kwa mwaka, ndani ya kikao cha leo ajenda kadhaa zitajadiliwa ikiwemo Dira ya Chama hicho kuelekea 2025, pamoja na suala Muhimu la KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI, limo pia suala dogo la Rufaa za waliokuwa wanachama wa chama hicho WALIOFUTWA UANACHAMA NA KAMATI KUU KUTOKANA NA USALITI

Tayari Wajumbe wamekwishaingia ndani ya Ukumbi huku wengine wakiendelea kumiminika , Ulinzi wa VIP PROTECTION ni wa Uhakika .

FB_IMG_1652258695861.jpg

Maajabu ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kurusha matukio hayo moja kwa moja , ikiwemo Clouds TV , jambo ambalo ni jipya mno kwa siasa za Tanzania.

msg-1395784623-15763.jpg
Wabunge 19 Wakuja kusikiliza hatma yao

Endelea kufuatilia Taarifa za Baraza hili Muhimu hapa hapa JF

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Viongozi wa dini wakiongozwa na Askofu Emmaus B Mwamakula, Mwenyekiti wa ACTwazalendo, Juma Duni, wachambuzi wa siasa, Jenerali Ulimwengu na mwanasiasa Hashim Rungwe wameshawasili ukumbini.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameongozana na mgeni wake ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) wameshawasili.

Jenerali Ulimwengu anazungumza:
“Chadema ni mojawapo ya nguzo muhimu ya demokrasia katika nchi hii, imejipambanua na vyama vingine kwa kufanya siasa ya kweli, siasa ya kweli ni kuzungumzia masuala yanayowahusu wananchi.

“Wakati mwingine wanakosoa watawala, wafanyabiashara au hata wahuni tu wa mtaani, pamoja na kuonyesha njia.

Juma Duni, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo:
"Safari ya vyama vya siasa nchini ni moja na lengo ni kupata mabadiliko chini ya katiba mpya na tume huru.”

"Sote vyama vya upinzani kwa pamoja tuna nguvu ya pamoja inayotusukuma kudai katiba mpya na tume huru, hatuna haja kutengana katika hili.

"Tunaposema People's power hiyo power sio yetu sisi viongozi, bali ni power inayotoka nyuma ya watu wetu na hao ndio wanaotaka katiba mpya.”

"Vyama vya siasa tukiwa wamoja dola itatusikiliza, tukitengana dola itatucheka, nina miaka 30 katika siasa, nikipigania katiba mpya na tume huru. Tuwe wamoja.

Bobi Wine anaungumza
Bobi Wine.jpg
"Nisisahu kujitambulisha kwenu kuwa, mimi ndiye Rais wa Uganda ambaye nilichaguliwa na watu wa Uganda.

"Pamoja na kuwa katika maeneo tofauti ya kijiografia lakini mambo tunayoyapitia katika siasa yanafanana.

"Kwa mara ya kwanza ilibidi mgombea urais nchini Uganda katika uchaguzi mkuu nchini humo kuvaa kifaa cha kuzuia risasi, na ni uchaguzi uliomwaga damu nyingi za raia wema.

"Timu yangu ya kampeni iliyokuwa na watu takribani 130 walizingirwa na kukamatwa na kukaa jela kwa miezi 7. Pamoja na mazingira hayo yote ulikuwa ni uchaguzi ambao watu wa Uganda walishinda.

"Nawapa salamu kutoka kwa watu wa Uganda, ambao hawajakata tamaa na hawataacha kupaza sauti kwa mambo ambayo hayaendi sawa. Nadhani hilo halina tofauti sana na hapa Tanzania.

"Kama hauwezi kujifunza kwa yaliyotokea huko nyuma, huwezi kutengeneza njia nzuri huko mbele unapokwenda."

"Wakati Rais Yoweri Museveni anachukua madaraka kwa mara ya kwanza, mimi (Bob Wine) nilikuwa nina miaka minne, na sasa nina miaka 40 huku Rais Museveni akiwa hana mpango wa kustaafu.

"Pamoja na yote yanayoendelea Uganda lakini tuna katiba nzuri ambayo naweza kusema kuwa ni moja ya katiba bora Afrika lakini haiheshimiwi.

"Hata inapotokea Museven amekuwa akibadilisha mara kwa mawa katiba lakini bado ipo vizuri, sheria za Uganda ni nzuri zikiwa kwenye makaratasi tu.

Freeman Mbowe anazungumza
Hatupaswi kulia na kulalamika, siku zote nimehubiri hatupaswi kujenga kisasi, bali yatupaswa kujengwa nguvu iliyojengwa kutokana na uonevu.

“Tunakumbuka Oktoba 2020 wakati wa uchaguzi ndipo ilikuwa kilele cha ubatiri na ukatiri wa uhuru wetu, miaka ya nyuma tulizoea kuibiwa kura lakini hiyo Oktoba 2020 tuliibiwa mfumo wa uchaguzi kwa jumla.

“Wakati tukilia na kulalamika, Mungu wetu alikuwa nan jia zake za kuonyesha utukufu wake, yaliyotokea mwaka 2021 yalipaswa kutokea ili kudhihirisha ukuu wa Mungu juu ya maisha yetu.

“Uchafuzi uliofanyika 2020 ilikuwa ni kielelezo cha juu cha baadhi ya mambi yafanyie ili tuutafute mwanzo mpya, ilibidi CCM waibe uchaguzi ule ili taifa na Dunia wajue CCM ni watu wa aina gani.

“Ilibidi wengine watangulie mbele ya haki ili wainusuru Tanzania na udiktekta, Ilibidi kiongozi mmoja wa mhimili kuropoka ili kuifikirisha umma kuhusu wajibu wa mhimili huo.

“Spika anakwenda anaropokwa manno ya hovyo japo ni ya ukweli, yakambeba nay eye kutuondolea kizingiti kikubwa katika demokrasia ya nchi yetu, ilibidi Mbowe na walinzi wake wakaishi gerezani ili kuibua mijadala ya uhuru, haki na demokrasia ya maendeleo katika taifa hili.

“Nimeona mengi kule gerezani, yana nafasi yake, naishukuru familia yangu, iliunganika na kusimama na mimi, nawashukuru mawakili, wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA.

"Nilivyotoka gerezani niliitwa na Rais mapema kwa kuwa alikuwa anasafiri, hata ningeitwa na IGP Sirro ningeenda. Nilimwambia Rais kuwa taifa letu lina tatizo kubwa.

MBOWE APIGA MARUFUKU VIONGOZI CHADEMA KUTUKANA WAPINZANI MITANDAONI
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho kuacha kutumia mitandao kutoa maneno ya kudhalilisha na kuwatukana wanachama wa vyama vingine vya upinzani, badala yake amewataka waheshimu kutofautiana kwao.

Amewataka kuwa viongozi wa CHADEMA kuwa wanyenyekevu na kuheshimu mitazamo ya vyama vingine, pia wametakiwa kuacha tabia hiyo mara moja kwa kuwa tofauti ya kimtazamo ndio demokrasia yenyewe.

“Inaweza msipende maneno yangu lakini lazima niwaambie ukweli, nafasi ya chama chetu leo ni chama kikuu cha upinzani Nchini, haina maana nafasi hiyo tukawa nayo milele, yawezekana kesho ikawa chama kingine chochote,” - Mbowe

MBOWE: WANASEMA NIMEPEWA TSH. BILIONI 6 KUMUONA RAIS
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewaambia wanachama wa chama chake kuwa kuacha dhana ya kuamini kila mpinzani anayepata mwaliko wa Ikulu anakuwa amenunuliwa kama ambavyo kuna maneno kuhusu yeye upewa fedha baada ya kuonekana Ikulu mara mbili hivi karibuni.

“Nchi yetu imejengwa kutoamiaminiana kwa miaka mingi, akionekana mpinzani ameenda Ikulu wanasema kuna biashara, mwingine akasema Mbowe amevuta bilioni 6 kwenda kumuona Rais, hayo ni mambo mepesi,” - Mbowe.

UPDATES
==========

RASMI : BARAZA KUU limetupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kuvuliwa uanachama baada ya kusaliti chama chao kwa kukubali kuapishwa kwenye gereji ya Bunge kuwa wabunge wa viti maalum wa Chadema kinyume cha Sheria , Baraza Kuu limebariki maamuzi yalifanywa na Kamati Kuu mwaka mmoja uliopita ya KUWAVUA UANACHAMA NA KUWATIMULIA MBALI .

Mungu ibariki Chadema .
 
Kikao kisicho na dira Wala mwelekeo leo ndiyo chadema wanaenda kujivua nguo Bora wawahoji kwenye vyumba hao kina mdee wakiwahoji hadharani ni aibu kwa mbowe na wenzake maana wanaenda kusema ukweli wa wakiowapeleka
 
Kikao cha baraza kuu kina mambo ya msingi mengi sana , wewe unazungumzia jambo dogo mno ! kwamba Mbowe aliweza kumtoa mfungwa jela ili akaapishwe bungeni ? kuamini hili unapaswa kuwa huna akili hata moja kichwani .
 
View attachment 2220248

Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba kile kikao kikubwa kabisa cha maamuzi Kikatiba , cha CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) , leo 11/5/2022 kinafanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City .

Kikao hiki ni cha kawaida cha chama hicho na ambacho hufanyika angalau mara moja kwa mwaka , ndani ya kikao cha leo ajenda kadhaa zitajadiliwa ikiwemo Dira ya Chama hicho kuelekea 2025 , pamoja na Suala Muhimu la KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI , limo pia suala dogo la Rufaa za waliokuwa wanachama wa chama hicho WALIOFUTWA UANACHAMA NA KAMATI KUU KUTOKANA NA USALITI

Tayari Wajumbe wamekwishaingia ndani ya Ukumbi huku wengine wakiendelea kumiminika , Ulinzi wa VIP PROTECTION ni wa Uhakika .

View attachment 2220249

Maajabu ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kurusha matukio hayo moja kwa moja , ikiwemo Clouds TV , jambo ambalo ni jipya mno kwa siasa za Tanzania .

View attachment 2220254

Endelea kufuatilia Taarifa za Baraza hili Muhimu hapa hapa JF
Fukuzeni Halima na genge lake pelekeni akina Hilda Newton
 
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba kile kikao kikubwa kabisa cha maamuzi Kikatiba cha CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), leo 11/5/2022 kinafanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kikao hiki ni cha kawaida cha chama hicho na ambacho hufanyika angalau mara moja kwa mwaka, ndani ya kikao cha leo ajenda kadhaa zitajadiliwa ikiwemo Dira ya Chama hicho kuelekea 2025, pamoja na suala Muhimu la KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI, limo pia suala dogo la Rufaa za waliokuwa wanachama wa chama hicho WALIOFUTWA UANACHAMA NA KAMATI KUU KUTOKANA NA USALITI

Tayari Wajumbe wamekwishaingia ndani ya Ukumbi huku wengine wakiendelea kumiminika , Ulinzi wa VIP PROTECTION ni wa Uhakika .

Maajabu ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kurusha matukio hayo moja kwa moja , ikiwemo Clouds TV , jambo ambalo ni jipya mno kwa siasa za Tanzania.

Endelea kufuatilia Taarifa za Baraza hili Muhimu hapa hapa JF

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Viongozi wa dini wakiongozwa na Askofu Emmaus B Mwamakula, Mwenyekiti wa ACTwazalendo, Juma Duni, wachambuzi wa siasa, Jenerali Ulimwengu na mwanasiasa Hashim Rungwe wameshawasili ukumbini.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameongozana na mgeni wake ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) wameshawasili.
Cdm ndio wenyewe kwa fashion show. Kwenye siasa wameishiwa kabisa.
 
Kikao cha baraza kuu kina mambo ya msingi mengi sana , wewe unazungumzia jambo dogo mno ! kwamba Mbowe aliweza kumtoa mfungwa jela ili akaapishwe bungeni ? kuamini hili unapaswa kuwa huna akili hata moja kichwani .
Kumbuka ukiwa ccm akili unaacha mlangoni( uko ulikotoka) unaingia na fuvu tu ambalo haliko connected na mdomo
 
JENERALI ULIMWENGU : CHADEMA NI NGUZO MUHIMU NCHINI TANZANIA

Jenerali Uliimwengu : Imani ya People's Power naikubali ndiyo tunapo kuwa pamoja ingawa mimi siyo mwanaCHADEMA. People's Power ndiyo msingi wenyewe wa wananchi kuiongoza nchi ktk mwelekeo wao ... na siyo kupelekeshwa na kikundi cha viongozi wachache ...

Jenerali Ulimwengu naamini ktk nguvu ya umma suala la madaraka ya nchi yatakuwa ktk mikono ya wananchi wenyewe, pia nakubali hili la CHADEMA kupeleka madaraka ya nchi kupitia ugatuzi / Devolution.... CHADEMA muendelee kuzungumzia hili bila kuchoka kwa wananchi kuwa na uamuzi wao wenyewe kwa kuamua mambo yao wenyewe kama taifa, mkoa, wilaya , tarafa , vijijini hadi mtaani na hili liwemo katika katiba ...
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom