Dar: Mikutano ya ana kwa ana ya SADC kusitishwa ili kudhibiti maambukizi ya Coronavirus

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wameshauri kusitishwa kwa vikao vyote vya ana kwa ana vya jumuiya hiyo hadi mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu wa corona utakapodhibitiwa.

Hatua hiyo imefikiwa wakati kunatarajiwa kufanyika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC jijini Dar es Salaam Machi 16 hadi 17, ukiwashirikisha mawaziri kutoka nchi zote 16.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipozungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, uliofanyika baada ya kikao cha dharura cha mawaziri wa afya wa SADC Ummy ambaye ni Mwenyekiti wa mawaziri wa afya wa Jumuiya hiyo, alisema wameshauri mikutano yote katika SADC ya ana kwa ana kusitishwa.

“Hivi sasa tunaweka nguvu zaidi katika kukinga kuliko kusubiri kutibu baada ya madhara kuingia. Tumekubaliana hata kama hakuna magonjwa, tudhibiti” amesema Ummy.

Alisema wamekubaliana kutoka katika utayari na kuingia katika hatua ya kuukabili Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya, Ummy alisema Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka vituo kwa washukiwa wa corona na sasa inajenga kituo cha kudumu katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea na kutibu washukiwa wa corona.

Hospitali hiyo ya Mloganzila ni sehemu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika mkutano huo wa waandishi jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Kushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbalo, aliyemwakilisha Profesa Palamagamba Kabudi alieleza kuwa mapendekezo hayo ni sahihi. Dk Ndumbalo alisema suala hilo la kusitishwa kwa vikao vya ana kwa ana, atalipeleka kwa Profesa Kabudi kwa hatua zaidi.

Alisema kwamba nchi 101 duniani zimeathirika na corona na sasa China haina magonjwa wengi kama nchi nyingine. Kwa nchi za SADC Afrika Kusini ndio pekee iliyoathirika na ugonjwa huo hadi sasa.

Aidha, Dk Ndumbaro alisema wanafunzi 504 wa Tanzania, walioko China wapo salama na kila siku wanapokea taarifa zao.

Awali, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya SADC, Stergomena Tax akitoa mapendekezo ya dharura kwa waandishi, alisema mapendekezo hayo yamelenga kuzuia athari na vikao vimeshauriwa kufanyika kwa mtandao.

Alisema pia wameshauri nchi wanachama kuwa na mfumo bora na madhubuti wa afya.

Pia wameomba msaada wa washirika wa kimataifa kusaidia nchi za SADC kukabili corona. Waliipongeza China kwa namna ilivyoukabili ugonjwa huo hatari.

Alisisitiza kunawa mikono, kufanya ukaguzi maeneo yenye mikusanyiko na katika vyombo vya usafiri, kuimarisha mifumo ya usalama katika kila nchi na kupeana taarifa za haraka kwa washukiwa wanaovuka mipaka.

Chanzo: Habari Leo
 
Vipi kule KIA bado wachina wanaingia kupitia huko na kuongeza idadi ya watalii nchini? Waziri Ummy aliangalie na hilo kama kweli ipo nia ya dhati ya kuzuia ugonjwa huo hatari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom