Dar: Mfanyabiashara kutoka Tabata afikishwa Mahakamani kwa kusafirisha binadamu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,374
8,110
Mfanyabiashara na mkazi wa Tabata Mawenzi, Mohamed Masoli (34) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, akikabiliwa na shtaka moja la usafirishaji haramu wa binadamu.

Masoli amefikishwa mahakamani leo, Oktoba 31, 2022 na kusomewa shitaka lake na wakili wa Serikali, Caroline Materu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.

Akimsomea hati ya mashtaka, wakili Materu amedai Masoli anakabiliwa na kesi ya jinai namba 168/2022 na alifanya kosa hilo Juni 11, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA), akidaiwa kumsafirisha Rahma Yusuph kwa ahadi ya kumpatia ajira nje ya nchini.

Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka linallmkabili, alikana na upande wa mashtaka wamesema kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

"Mheshimiwa hakimu, kwa kuwa upelelezi umekamilika, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomewa hoja za awali (PH) mshtakiwa huyu," amesema wakili Materu.

Kwa upande wao mawakili wa mshtakiwa huyo, Douglas Mmari na Mohamed Majaliwa, waliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe ya karibu kwa kuwa mteja wao afya yake siyo nzuri na amekaa polisi kwa muda mrefu.

Hakimu Rugemalira baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, alimueleza mshtakiwa kuwa shtaka la kumsafirisha binadamu halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Baada ya maelezo hayo, hakimu Rugemalira aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14, 2022 itakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomea hoja za awali na kisha kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka linalikukabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Mwananchi​

Naomba kufahamishwa,ikitokea mtu umemhitaji kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa ajili ya kumpatia kibarua, ni wakati gani utahesabika umeasafirisha binadamu na ni wakati gani hutahesabika hivyo!?
Kuna agents wanahusika kumpatia ajira mtu na hawa wanatambulika na serikali kwa kuwa ndio kazi yao hivyo wanapokupeleka sehemu tayari unakuwa umesaini mikataba na unajua ajira unayoenda kufanya pamoja na stahiki zako ikiwemo makazi nk.

Ni ngumu kutambua mtu anayesafirisha binadamu kimakosa lakini Kuna viashiria vingi ikiwemo umri wa anayesafirisha, uhusiano nk.

Unakuta pale airport unamhoji mtu anakuambia ninapoenda sikujui na Wala hajui anaenda kufanya kazi gani au anakuambia anaenda kufanya kazi za ndani na anasafirishwa akiwa na mtu ambaye ndio anampeleka. Hii maana yake unausafirishaji haramu.

The only people wanaoruhusiwa kupatia ajira watu ni employment agency pekee ambao wanatambulika kisheria otherwise unakuwa imefanya kosa la human trafficking.

Hata wale wanaotutafutia mahousegirla, wauza duka au kijana wa shamba Ile no kosa sema wanakaushiwa tu kibongobongo.
 
Hapo nami Niko empt ngoja tumiite wakili msomi MALCOM LUMUMBA aje atudafulie hili swala la kusafirisha binadamu

Mnk akinitafutia dad wa Kaz kwa kumtoa mbeya na Kisha kumleta dar hyo Ni usafirishaji
 
Dah,,,hivi mtu anasafirishwa kwani yeye ni kifurushi?

Ukiwa na bahati mbaya huna kwa kukwepa.
 
Wao hawana kazi za kuwapa wananchi wao, na wakipambana kivyao pia wanazuiwa kwa visingizio vya kishamba tu
 
Kuna agents wanahusika kumpatia ajira mtu na hawa wanatambulika na serikali kwa kuwa ndio kazi yao hivyo wanapokupeleka sehemu tayari unakuwa umesaini mikataba na unajua ajira unayoenda kufanya pamoja na stahiki zako ikiwemo makazi nk.

Ni ngumu kutambua mtu anayesafirisha binadamu kimakosa lakini Kuna viashiria vingi ikiwemo umri wa anayesafirisha, uhusiano nk.

Unakuta pale airport unamhoji mtu anakuambia ninapoenda sikujui na Wala hajui anaenda kufanya kazi gani au anakuambia anaenda kufanya kazi za ndani na anasafirishwa akiwa na mtu ambaye ndio anampeleka. Hii maana yake unausafirishaji haramu.

The only people wanaoruhusiwa kupatia ajira watu ni employment agency pekee ambao wanatambulika kisheria otherwise unakuwa imefanya kosa la human trafficking.

Hata wale wanaotutafutia mahousegirla, wauza duka au kijana wa shamba Ile no kosa sema wanakaushiwa tu kibongobongo.
Nimekusoma kwa kurudia na kurudia bado sikuelewi kabisa, ngoja nikuambie hizi zote ni signs za police state, ni wajibu wa immigration officer baada ya kujiridhia kuwa msafiri ana passport halali huwezi kumzuia kusafiri, ni wajibu wa immigrations huko anakokwenda ambao wataamua kumruhusu msafiri au la sio uhamiaji wetu, human trafficking ni mbaya yes ,ila huyu amepewa hii kesi na maadam tunaishi in a pithole country eti haina dhamana!,Tanzania tumepotea kama nchi, tuhuma zote kuanzia murder LAZIMA ziwe na dhamana maana ni suspect, upo huru na haki zote hadi courts of law iamue vinginevyo, mapapa wa human trafficking bado wanapeta sana na tuelewe kwa kila wahebeshi 10 wanaokwenda SA,8wamepitia Tanzania kwa syndicates hizi hao ndio wa ku deal now maana wameingia nchi yetu kwa kuruka dirishani!
 
Kuna agents wanahusika kumpatia ajira mtu na hawa wanatambulika na serikali kwa kuwa ndio kazi yao hivyo wanapokupeleka sehemu tayari unakuwa umesaini mikataba na unajua ajira unayoenda kufanya pamoja na stahiki zako ikiwemo makazi nk.

Ni ngumu kutambua mtu anayesafirisha binadamu kimakosa lakini Kuna viashiria vingi ikiwemo umri wa anayesafirisha, uhusiano nk.

Unakuta pale airport unamhoji mtu anakuambia ninapoenda sikujui na Wala hajui anaenda kufanya kazi gani au anakuambia anaenda kufanya kazi za ndani na anasafirishwa akiwa na mtu ambaye ndio anampeleka. Hii maana yake unausafirishaji haramu.

The only people wanaoruhusiwa kupatia ajira watu ni employment agency pekee ambao wanatambulika kisheria otherwise unakuwa imefanya kosa la human trafficking.

Hata wale wanaotutafutia mahousegirla, wauza duka au kijana wa shamba Ile no kosa sema wanakaushiwa tu kibongobongo.
Mkuu kisheria inaruhusiwa kuhojiwa Airport wakati ana safari wakati ametimiza vigezo vyote vya kusafiri nje ya nchi? Mkuu uluvyo muuliza mwaswali majibu aliyokupa unaushaidi majibu ni sahihi?,Mfano mimi na safiri kwenda Uingereza nipo Airport nianze kuulizwa maswali kama ya huyo uliyekuwa una muuliza mimi nitajibu kama huyo alivyo kujibu tu, maana mpaka nimekata Visa, Passport na tiketi ya ndege ina maana ninajua ninapo kwenda na ninachoenda kukifanya.
 
Back
Top Bottom