Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

View attachment 1887764

View attachment 1887765

Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuzivutia kampuni kubwa za usafirishaji duniani, baada ya meli kubwa ya kisasa ikiwa na shehena kubwa zaidi ya magari kuwahi kutia nanga bandarini hapo.

Meli hiyo ya TRANQUAIL ACE (IMO: 9561253) inayomilikiwa na Kampuni ya Mitsui ikitokea moja kwa moja nchini Japan, imetia nanga ikiwa na magari 3,743 ambayo ni mengi zaidi kuwahi kusafirishwa kuja nchini kwa mara moja.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi amesema kuwa meli hiyo imeandika historia mpya kutokana na kubeba shehena kubwa ya magari.

Meli hiyo iliyotengenezwa mwaka 2009 ina urefu wa mita 199.9 na upana mita 32.2 kwenda chini, ambapo imetia nanga chini ya nahodha, Diardado Garate.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2021 katika Bandari ya Dar es Salaam, Hamissi amesema kuwa meli hiyo imetia nanga Agosti 9, 2021 na kuanza shughuli ya ushushaji ambao unatarajiwa kumalizika kesho jioni.

Meli kubwa kuwahi kutia nanga nchini na ailiyokuwa imebeba shehena kubwa ya magari ilitia nanga bandarini hapo mwaka 2018 ikiwa na magari 2600.

"Leo ni siku nzuri sana katika historia ya TPA kwa kuweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa na iliyobeba shehena kubwa zaidi kuja nchini. Hii haijawahi kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kubwa zaidi meli hii imetoka moja kwa moja Japan kuja nchini bila kupitia bandari nyingine.

View attachment 1887766

"Kwa hiyo ni jambo jema dunia inakafahamu kwamba, Tanzania tuna bandari bora na ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli zote na ikazihudumia kwa wakati,” amesema Hamissi na kuongeza: “Katika inayoendelea kushushwa, magari yatasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda nchi jirani na mengine 798 yanabaki hapa nchini.

"Mtaona ni jinsi gani sasa nchi zetu za jirani zinazotuzunguuka zimeenza kutuamini, kati ya magari yaliyoingia asilimia 65 yanakwenda kwenye nchi hizo."

Meneja Kampuni ya Inchcape Shipping Services, John Massawe amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba magari 5,200 na kwamba imetumia siku 20 ikiwa safari hadi kuwasili.

"Tumekuwa tukihudumia kampuni ya magari kwa miaka zaidi ya 20, na hii ni meli ya kwanza hivyo tunatarajia huu ni mwanzo wa kuleta meli nyingine kubwa zaidi," amesema Massawe.
urefu viwanja viwili vya mpira, Endeleeni kupambana na CHADEMA, kuja kufika huku labda YESU atakuwa kisharudi
 
Mkuu performance tunacheki masaa/siku ukisema shift 4 maana yake ni masaa 33 na dakika 20 au siku 1 na masaa 9 dakika 20.

Kiutendaji tunaanza kuhesabu muda gari la kwanza lilipotoka na muda gari la mwisho lilipomaliza kushuka melini. Ndani ya shift 4 Kuna muda kazi ilikuwa inasimama (delays) huo muda lazima utolewe na ujulikane ndipo tunapata muda sahihi kazi ilipofanyika.

Mpaka muda nasoma sms Yako saa 1610HRS Local Time, hapa kwenye simu yangu nimetrack naiona hiyo meli bado ipo Bandari
Huo muda ndio gari ya mwisho inatoka melini kumbuka kuna kujaza clearance hapo kusachi stowaway kufunga lamp pilot nae apande melini ili iondoke ni kazi lisaa lizima mbele
 
Mkuu TUJITEGEMEE,

I hope ulisoma ule uzi wangu kuhusu Bandari ya Bagamoyo!!

Uzi ule ulibeba findings za research kuhusu Belt & Road Initiative ya China ambayo ndiyo imezaa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, na Infrastructure Projects zingine kadhaa za Mchina kote duniani!!

Kama unakumbuka, nilisema wazi kwamba moja ya changamoto ambayo tuliipata kwenye ile research ni ukiritimba wa watu kugoma kuonesha official docs!! Na linapokuja suala la mikataba, we all know serikali wamekuwa wagumu sana kuitoa... hili suala limekuwa likilalamikiwa na wabunge miaka nenda rudi!!!

Jambo ambalo tulifanikiwa kupata ni kile kile kinachofanywa siku zote! Kwamba, baadhi ya watendaji walikuwa tayari kuongea off-records lakini sio kutoa docs!! Yaani ingawaje doc yenyewe ilikuwa imesha-expire lakini bado ilikuwa treated, na bila shaka bado inakuwa treated as confidential doc!!

So, no one was ready to reveal it to Beberu (An American Researcher)!!

Lakini ingawaje hatukupata hizo doc but through off-record, lakini tuliweza kufahamu mambo ya msingi yaliyokuwa highlighted!!!

Ujinga wa hili jambo, hata mimi mwenyewe nashindwa kulielezea kwa undani, na ndo maana ingawaje hii research ilikuwa way back in 2016 lakini nilishindwa kusema lolote hadi 2021, na ndipo angalau nikasema machache kutokana na Strict NDA ambayo nimesaini!!
 
Huo muda ndio gari ya mwisho inatoka melini kumbuka kuna kujaza clearance hapo kusachi stowaway kufunga lamp pilot nae apande melini ili iondoke ni kazi lisaa lizima mbele
Mkuu naongelea operation time tu, muda uliotumika kutoa gari ya kwanza mpaka ya mwisho. Mambo ya kusaini documents, booking pilot,search for stowaway na kufungua meli hatuweki kwenye operation tutakuja kuweka kwenye ship dwell time.

Kiufupi meli imetumia muda mrefu kushusha hizo unit 3784 za magari kwa muda wa saa ~33 either kuwe na sababu kama manpower( idadi ndogo ya madereva,makarani, inspection, security n.k), baadhi ya gari kuja na mechanical fault ambazo zinahitaji technicians au msaada wa kuboost au kuvutwa, stowage allocation na sababu nyingine ambazo hatuzijui.

Hesabu hazidanganyi mkuu, kama waweza weka minimum/maximum manpower (idadi ya drivers waliofanya kazi per shift) kisha tukokotoe hapa tupate Makadirio ya wastani ya gari zilizoshuka Kwa saa/shift.

Kwa hayo masaa performance ni ya kawaida Sana.
 
Siku moja nitaenda kutalii bandarini, nione hizo meli zinavyofanana, kwa kweli sikuwahi kufikiri kama meli inaweza kubeba magari mengi kiasi hicho
Bado hiyo ni ndogo... Kuna zinazobeba zaidi na ukubwa wake ni kama viwanja vinne vya mpira
 
Hivi unajua utofauti wa ukubwa wa meli?!

Chukua tu mfano wa ile meli ambayo hivi karibuni ilikwama Suez Canal...

Sasa hizo 1300-foot ni sawa na meter ngapi, kisha linganisha na hiyo yenye urefu wa 200m!

Lakini hata hiyo yenye urefu wa 396m, haipo katika Top 10 Largest Ships duniani; what about hiyo ya "kwetu" yenye urefu wa 200m?

Halafu binafsi nafuatilia sana issues za cruise ships kwa sababu niliwahi kupokonywa tonge kinywani kwenye mchango wa kufanya kazi kwenye hizo meli!! Cruise ship inayoshikilia nafasi ya 10 kwa ukubwa, ina urefu wa zaidi ya 300m!!

Again, linganisha na hiyo yenye urefu wa 200m ambayo baada ya kuambiwa ni "meli kubwa" ndo ukadhani ni miongoni meli kubwa zaidi duniani!

Hapa unatakiwa kutofautisha kati ya big ships na mega-ships ambazo zina uwezo wa kubeba zaidi ya makontena 20K!!
Kuna yenye urefu wa mita 458 ambayo ni kama nusu kilomita
 
Mbona hii meli imewahi kuja Bandari ya hapo hapo Dar es Salaam kipindi cha nyuma ?

Nini kimebadilika mpaka iwe habari ?

Naomba ufafanuzi tafadhali !
Kilichobadilika ni kwamba imebeba magari mengi tu basi......
 
Itabidi maza ashughulike hiyo kero kwa kuwawajibisha wahusika.
Ndugu hakuna mahala paajabu kama port kunakulindana kwa hali ya juu, lakini asikufiche mtu pangepata mtu mahususi ni mahala pangeingiza kipato kikubwa sana serekalini mwetu kwakweli.
Usafi,huduma,uangalizi bora,vifaa vinafujwa kiasi ukiona unaweza kulia, Fork lift ikiwashwa mwanzo wa shift mpaka iishe haijazimwa mafuta yanaungua tu hata ikiwa stand by, siku ukikuta machine zimeoshwa jua Raisi anakuja port.
Pale ni zaidi ya shamba la bibi.
 
Inakua Bandari ya kwanza duniani kupokea magari mengi kwa wakati mmoja. Hongera sana
 
Meli haitii nanga bandarini acheni ujinga nanga unatosa nje anchorage ukiwa unasubiri kuingia bandarini na ukiingia bandarini unafunga kamba kwenye gati au berth mfano;berth no;1,2,3 au 5 nakuendelea kutegemea na aina ya meli mfano magari ,container,tanker,car carrier n.k.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom