Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

Durban port
1628678609585.png

1628678632308.png

1628678655894.png

1628678695005.png
1628678715692.png

Port ya Taifa
1628678772417.png

1628678815144.png

Watanzania tunahitaji bandari kubwa kuliko hiyo ya Durban, tuna faida kubwa ya kijiografia kuzungukwa na 6 zisizo na bandari kabisa.

Beira Mozambique
1628678951324.png
1628678971718.png
1628678993250.png
1628679022279.png
 
Hapa nauona na kuushangaa utukufu wa mtu mweupe kwa kutengeneza hilo dubwana.TPA hawana maajabu yoyote.
 
Lakini unapotoka tu mbele na kusema "Mchina anataka asamehewe kodi" ni rahisi sana wananchi kuamini kwamba kumbe zile VAT, Import Tax, Excise Duty n.k zote hizo zinaenda kwa Mchina; jambo ambalo si kweli!!
Asante sana kwa kuniweka sawa. Bahati iliyoje baada ya kurudia tena kusoma posts ulizonijibu nimejua sasa kumbe mktaba haukuwepo, bali ilikuwepo framework of agreement. Na hii agreement imeisha expire.

Kwa hiyo siyo valid inatakiwa itupwe jalalani. Sasa, ili kukata kiu yangu na wengine ya kuongeza uelewa, unaweza kutusaidia kupata nakala ya hiyo expired framework of agreement kabla hawajaitupa jalalani? Hii itasaida kumkoma nyani giladi walio sema mradi ni mradi wa win-loose na wale wa win-win.

Natanguliza shukrani.

Ulishawahi kuona au kusikia pande mbili zinasaini mkataba, halafu hapo hapo wanatangaza wanaendelea na majadiliano kwa sababu hawajafikia makubaliano?! Hushawahi kusikia kitu kama hicho?!

Sina shaka wewe ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea nchini! Je, ipo siku yoyote uliyowahi kusikia kwamba SERIKALI IMEVUNJA MKATABA wa Ujenzi wa Bandari?
Hapa umenishauri nitafakari peke yangu. Nimefanya hivyo.
 
Ndio series yake yapo 11 EVER GREEN halafu bado kuna MAERSK nae ana vyuma bandari ya bongo haziingii
Du.... Kumbe ni balaa...

Kumbe tusianze kujisifu mapema... Bado madude yenyewe hayajatia nanga....
 
View attachment 1887764

View attachment 1887765

Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuzivutia kampuni kubwa za usafirishaji duniani, baada ya meli kubwa ya kisasa ikiwa na shehena kubwa zaidi ya magari kuwahi kutia nanga bandarini hapo.

Meli hiyo ya TRANQUAIL ACE (IMO: 9561253) inayomilikiwa na Kampuni ya Mitsui ikitokea moja kwa moja nchini Japan, imetia nanga ikiwa na magari 3,743 ambayo ni mengi zaidi kuwahi kusafirishwa kuja nchini kwa mara moja.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi amesema kuwa meli hiyo imeandika historia mpya kutokana na kubeba shehena kubwa ya magari.

Meli hiyo iliyotengenezwa mwaka 2009 ina urefu wa mita 199.9 na upana mita 32.2 kwenda chini, ambapo imetia nanga chini ya nahodha, Diardado Garate.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2021 katika Bandari ya Dar es Salaam, Hamissi amesema kuwa meli hiyo imetia nanga Agosti 9, 2021 na kuanza shughuli ya ushushaji ambao unatarajiwa kumalizika kesho jioni.

Meli kubwa kuwahi kutia nanga nchini na ailiyokuwa imebeba shehena kubwa ya magari ilitia nanga bandarini hapo mwaka 2018 ikiwa na magari 2600.

"Leo ni siku nzuri sana katika historia ya TPA kwa kuweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa na iliyobeba shehena kubwa zaidi kuja nchini. Hii haijawahi kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kubwa zaidi meli hii imetoka moja kwa moja Japan kuja nchini bila kupitia bandari nyingine.

View attachment 1887766

"Kwa hiyo ni jambo jema dunia inakafahamu kwamba, Tanzania tuna bandari bora na ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli zote na ikazihudumia kwa wakati,” amesema Hamissi na kuongeza: “Katika inayoendelea kushushwa, magari yatasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda nchi jirani na mengine 798 yanabaki hapa nchini.

"Mtaona ni jinsi gani sasa nchi zetu za jirani zinazotuzunguuka zimeenza kutuamini, kati ya magari yaliyoingia asilimia 65 yanakwenda kwenye nchi hizo."

Meneja Kampuni ya Inchcape Shipping Services, John Massawe amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba magari 5,200 na kwamba imetumia siku 20 ikiwa safari hadi kuwasili.

"Tumekuwa tukihudumia kampuni ya magari kwa miaka zaidi ya 20, na hii ni meli ya kwanza hivyo tunatarajia huu ni mwanzo wa kuleta meli nyingine kubwa zaidi," amesema Massawe.
Meli imetoka mombasa kuja dar
Kwenye maelezo tunaongopewa imetoka japan moja kwa moja dar.....
 
Bandari Ina changamoto sana kiutendaji kuanzia storage facility, handling equipment, parking na system.

Humu Kuna raia Wana thubutu kulinganisha Dar Port na Durban Port
Wana wazimu hao.......bandari ya bongo inaendeshwa kilocal zaidi na sio kimataifa.....international
 
Mkuu sisi time na efficiency hatujaweka kipaumbele.
Kama waandishi wa habari wamethubutu kuandika na kutangaza habari ya ujio wa meli na idadi kubwa ya Magari katika bandari ya Dar.

Basi Hiyo meli ikimaliza kushusha waandike habari au taarifa ya meli kushusha Magari mengi kwa muda uliotumika ili tujue efficiency, delay zilizotokea na changamoto ili tuone uwezo wa bandari yetu.

Hii habari nakuhakikishia hawatoandika hata kwenye kurasa za ndani, Bora warudie Ile ya mkuu wa wilaya kukataza wanaume kunyonya maziwa ya wake zao.
Mdau iyo meli imetumia shift nne kuimaliza magari yote 3743
 
Mnaosema bandari ya Dar haiwezi himili meli kubwa uongo wenu umeanza kuonekana
Maerks wana meli zinabeba tani 40,000 na zaidi. Kuna meli kibao zinabeba kontena zaidi ya 20,000 tena zinaenda meli kumi bandari moja. Wewe unakuja sema meli ya magari 3,000 tena moja kwa bandari nzima
 
Mdau iyo meli imetumia shift nne kuimaliza magari yote 3743
Mkuu performance tunacheki masaa/siku ukisema shift 4 maana yake ni masaa 33 na dakika 20 au siku 1 na masaa 9 dakika 20.

Kiutendaji tunaanza kuhesabu muda gari la kwanza lilipotoka na muda gari la mwisho lilipomaliza kushuka melini. Ndani ya shift 4 Kuna muda kazi ilikuwa inasimama (delays) huo muda lazima utolewe na ujulikane ndipo tunapata muda sahihi kazi ilipofanyika.

Mpaka muda nasoma sms Yako saa 1610HRS Local Time, hapa kwenye simu yangu nimetrack naiona hiyo meli bado ipo Bandari
 
Sisi wananchi wagonga ulimbo tunafaidikaje kuwasili kwa meli hiyo?
 
Siku moja nitaenda kutalii bandarini, nione hizo meli zinavyofanana, kwa kweli sikuwahi kufikiri kama meli inaweza kubeba magari mengi kiasi hicho
Mimi nilisikia meli inabeba makontena elfu16 nikabaki kushangaa tu
 
View attachment 1887928
Huyo bwana mkubwa anasema imetoka moja kwa moja Japan, mbona inaonyesha kuwa imepita bandari kadhaa (ikiwemo kwa majirani) kabla ya kufika kwetu. Halafu kwa wenzetu imekuwa serviced chini ya 20hrs! Tunahitaji kufanya kazi zaidi badala ya kujisifia kila k

View attachment 1887928
Huyo bwana mkubwa anasema imetoka moja kwa moja Japan, mbona inaonyesha kuwa imepita bandari kadhaa (ikiwemo kwa majirani) kabla ya kufika kwetu. Halafu kwa wenzetu imekuwa serviced chini ya 20hrs! Tunahitaji kufanya kazi zaidi badala ya kujisifia kila kukicha.
brother unazijuwa feeder vessels
 
View attachment 1887764

View attachment 1887765

Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuzivutia kampuni kubwa za usafirishaji duniani, baada ya meli kubwa ya kisasa ikiwa na shehena kubwa zaidi ya magari kuwahi kutia nanga bandarini hapo.

Meli hiyo ya TRANQUAIL ACE (IMO: 9561253) inayomilikiwa na Kampuni ya Mitsui ikitokea moja kwa moja nchini Japan, imetia nanga ikiwa na magari 3,743 ambayo ni mengi zaidi kuwahi kusafirishwa kuja nchini kwa mara moja.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi amesema kuwa meli hiyo imeandika historia mpya kutokana na kubeba shehena kubwa ya magari.

Meli hiyo iliyotengenezwa mwaka 2009 ina urefu wa mita 199.9 na upana mita 32.2 kwenda chini, ambapo imetia nanga chini ya nahodha, Diardado Garate.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2021 katika Bandari ya Dar es Salaam, Hamissi amesema kuwa meli hiyo imetia nanga Agosti 9, 2021 na kuanza shughuli ya ushushaji ambao unatarajiwa kumalizika kesho jioni.

Meli kubwa kuwahi kutia nanga nchini na ailiyokuwa imebeba shehena kubwa ya magari ilitia nanga bandarini hapo mwaka 2018 ikiwa na magari 2600.

"Leo ni siku nzuri sana katika historia ya TPA kwa kuweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa na iliyobeba shehena kubwa zaidi kuja nchini. Hii haijawahi kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kubwa zaidi meli hii imetoka moja kwa moja Japan kuja nchini bila kupitia bandari nyingine.

View attachment 1887766

"Kwa hiyo ni jambo jema dunia inakafahamu kwamba, Tanzania tuna bandari bora na ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli zote na ikazihudumia kwa wakati,” amesema Hamissi na kuongeza: “Katika inayoendelea kushushwa, magari yatasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda nchi jirani na mengine 798 yanabaki hapa nchini.

"Mtaona ni jinsi gani sasa nchi zetu za jirani zinazotuzunguuka zimeenza kutuamini, kati ya magari yaliyoingia asilimia 65 yanakwenda kwenye nchi hizo."

Meneja Kampuni ya Inchcape Shipping Services, John Massawe amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba magari 5,200 na kwamba imetumia siku 20 ikiwa safari hadi kuwasili.

"Tumekuwa tukihudumia kampuni ya magari kwa miaka zaidi ya 20, na hii ni meli ya kwanza hivyo tunatarajia huu ni mwanzo wa kuleta meli nyingine kubwa zaidi," amesema Massawe.
Habari nzuri sana,haya ndio maendeleo,yasiohitaji tochi,tunayaona kwa macho yetu.
 
Back
Top Bottom